Afrika Kusini na ubaguzi wa rangi, picha hii yazua taharuki

Kwanini mungu alituumba rangi tofaut? Tatizo linaanzia hapo kabla ya kuwalaum wazungu

Sent using Jamii Forums mobile app
Jawabu yake ni Quran 49:13 "Enyi watu Hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezimungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi......
 
Gangs za wazulu zipo South ila hawana kiburi cha kuwafanyia wazungu wenyewe wana deal na waafrika wenzao.

Wale wazungu wenyewe ni vichwa vibovu kuliko mzulu yale makaburu asili yao ni Dutch na Germany ni makatili na hayaogopagi. Ndio maana kwenye xenophobia attack Hayupo mzulu aliegusa Mali zao. Yana machine gun yakinyanyua mpaka magazine iishe.

Sent using Jamii Forums mobile app

😂😂😂😂😂😂
 
Picha mmeshaitengenezea maelezo tayari. Miafrika mtaendelea kuwa hivyo. Wakati mchawi wa mwafrika ni sisi wenyewe.

Umeongea vema. Ukweli ni kwamba sisi wenyewe tuna matatizo makubwa. Angalia kwa mfano Afrika Kusini weusi wanavyowanyanyasa waafrika wenzao mpaka kuwaua watoke nchini mwao. Angalia kwa mfano hapa Tanzania kundi moja linajiona ndo lenye haki na makundi mengine hayana haki na nchi hii. Angalia maeneo mbalimbali tunavyobaguana wenyewe. Lakini kila ttz tunamsingizia mzungu. Siungi mkono mzungu kumbagua mwafrika lakini nasema sisi pia tujitizame vzr matendo yetu tunayoyafanya
 
Tupe maelezo mafupi kuthibitisha point yako

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwanza mungu hataki demokrasia anataka akikalie yeye tu kiti ca enzi milele tumsujudie, shetani ana nguvu ameonyesha nia na uwezo kum_challenge mungu nafasi iyo na yeye inamfaa.
Ubaguzi wa mungu ni kukaa mbinguni anajificha huko kwanini yeye asijichanganye na sisi yaani hataki hata tumuone hii si bora hata hao wazungu wanatubagua ila hua wanakuja afrika tunawaona au hata sisi kwenda huko kwao.
 
Wangekuwa wametengwa na waarabu povu lingewatoka mno, zingefika page 20 mpaka now. Miafrika bhana.

Hoja yako ni nini mbona unaandika upumbafu hapa??? Wewe ni mwarabu au? Na unamaanisha nini maana hapa kinazungumziwa kingine siyo uarabu. Tumia akili jaman
 
Its simple, katika maisha its the one with pen who control the story. Wazungu ndio walikuwa na pen ya kuandika story ya Dunia na Dini hivyo kwao wao Mungu ni babu mmoja wa kizungu anaekaa juu huko kwenye mawingu na shetani yeye ni mweusi tii asie na makazi maalumu na mwisho wa picha Mzungu anatuambia atamkamata shetani mweusi amtupe jehanamu na wafuasi wake.

Hata kama ni wewe lazma ufanye juhudi za kuukimbia ushetani kwa kutoka kwenye uafrika na kukimbilia uzunguni kwa Mungu.

Its pure psychology manipulation.

Sent using Jamii Forums mobile app

Word.
 
Mungu nisaidie sana lakini Kwakweli Wazungu walichowafanya wazee wetu wakati wa ukoloni sioni sababu ya kuwanao karibu. #Nawachukia.
Mama wa mtoto katika shule ya awali ya Laerskool Schweizer-Reneke iliyopo katika jimbo la North West huko Afrika Kusini, amechukizwa vikali baada ya picha inayomuonesha mtoto wake wa kike na watoto wengine watatu wa Kiafrika wakiwa wamekaa peke yao mbali na watoto wengine wa kizungu kwenye darasa lao. Picha hiyo ambayo inasambaa kwa kasi mtandaoni, imesababisha hasira kubwa kwa raia wa nchi hiyo kutokana na kuwa na ishara ya ubaguzi wa rangi.

Picha hiyo ilitumwa kwenye kundi la WhatsApp la shule hiyo na mwalimu wa darasa. "Hii ilipaswa kuwa siku ya kufurahisha kwangu lakini sio,” amesema mzazi huyo. Mama huyo ambaye hakutajwa jina kulinda utambulisho wa mwanae, ameiambia tovuti ya TimesLIVE ya nchini humo kuwa siku ya kwanza katika darasa hilo ilianza vizuri.

Yeye na wazazi wengine waliwapeleka watoto wao na kuambiwa waondoke katika eneo la shule. Saa tatu asubuhi walitumiwa taarifa kutoka kwa mwalimu wa watoto hao kuhusu siku ilivyokwenda kupitia WhatsApp group. Picha hiyo ilionesha watoto 18 wa kizungu wakiwa darasani wamekaa dawati moja lililounganishwa katikati ya darasa, wakati watoto wanne wa Kiafrika wakiwa wamekaa kwenye dawati moja lililowekwa kwenye kona ya darasa hilo. "Nilichoona ni jumbe toka kwa wazazi wa kizungu wakisema asante asante kwenye WhatsApp group, lakini hakuna yeyote aliyesema kuhusu walivyotenganishwa,” alisema mzazi huyo.

Amesema baada ya kujadiliana na mzazi mwingine nje ya WhatsApp group, mzazi huyo aliwasiliana na mkuu wa shule kuuliza kuhusu ukaaji wa watoto hao darasani. TimesLIVE imedai mkuu huyo wa shule alisema hakuwa na taarifa za suala hilo. Wamedai kuwa wanasubiri jibu toka kwa shule hiyo.

Alipoulizwa kuhusu anavyojisikia kutokana na hali hiyo, mama huyo amesema ana matumaini kuwa mwanae mwenye umri wa miaka mitano bado ni mdogo kuweza kutambua kilichotokea.
"Lakini nimechukia,” alisema mama huyo aliyeahidi kuchukua hatua zaidi.

Source: Bongo5View attachment 990332

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kha inaumiza ...yaani hata kwa kuangalia hao watoto wa kizungu hapo wana furaha halafu wale wengine wanashangaa tu!
 
Kwa akili yako Unadhani hizo Nchi sijatembea ukiona mweusi anaoa huko Oman ujue huyo ni mzawa wenyewe wana waita BULUSHI. Sheria za Nchi hizo unazijua wewe au unafurahisha jukwaani, Mfano Oman sheria yao Mwananchi wa Nchi hiyo huluhusiwi kuoa/kuolewa na Nchi yoyote labla atakaye kuoa/kuolewa awe mlemavu au mzee kuanzia miaka 60 yaani unidanganyi kitu kuhusu hizo Nchi.
Hiyo aliniambia dada mmoja ni muarab wa huku nikajua kejeli tu kumbe kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama wa mtoto katika shule ya awali ya Laerskool Schweizer-Reneke iliyopo katika jimbo la North West huko Afrika Kusini, amechukizwa vikali baada ya picha inayomuonesha mtoto wake wa kike na watoto wengine watatu wa Kiafrika wakiwa wamekaa peke yao mbali na watoto wengine wa kizungu kwenye darasa lao. Picha hiyo ambayo inasambaa kwa kasi mtandaoni, imesababisha hasira kubwa kwa raia wa nchi hiyo kutokana na kuwa na ishara ya ubaguzi wa rangi.

Picha hiyo ilitumwa kwenye kundi la WhatsApp la shule hiyo na mwalimu wa darasa. "Hii ilipaswa kuwa siku ya kufurahisha kwangu lakini sio,” amesema mzazi huyo. Mama huyo ambaye hakutajwa jina kulinda utambulisho wa mwanae, ameiambia tovuti ya TimesLIVE ya nchini humo kuwa siku ya kwanza katika darasa hilo ilianza vizuri.

Yeye na wazazi wengine waliwapeleka watoto wao na kuambiwa waondoke katika eneo la shule. Saa tatu asubuhi walitumiwa taarifa kutoka kwa mwalimu wa watoto hao kuhusu siku ilivyokwenda kupitia WhatsApp group. Picha hiyo ilionesha watoto 18 wa kizungu wakiwa darasani wamekaa dawati moja lililounganishwa katikati ya darasa, wakati watoto wanne wa Kiafrika wakiwa wamekaa kwenye dawati moja lililowekwa kwenye kona ya darasa hilo. "Nilichoona ni jumbe toka kwa wazazi wa kizungu wakisema asante asante kwenye WhatsApp group, lakini hakuna yeyote aliyesema kuhusu walivyotenganishwa,” alisema mzazi huyo.

Amesema baada ya kujadiliana na mzazi mwingine nje ya WhatsApp group, mzazi huyo aliwasiliana na mkuu wa shule kuuliza kuhusu ukaaji wa watoto hao darasani. TimesLIVE imedai mkuu huyo wa shule alisema hakuwa na taarifa za suala hilo. Wamedai kuwa wanasubiri jibu toka kwa shule hiyo.

Alipoulizwa kuhusu anavyojisikia kutokana na hali hiyo, mama huyo amesema ana matumaini kuwa mwanae mwenye umri wa miaka mitano bado ni mdogo kuweza kutambua kilichotokea.
"Lakini nimechukia,” alisema mama huyo aliyeahidi kuchukua hatua zaidi.

Source: Bongo5View attachment 990332
Ningekuwa mie ndio mzazi wangenirudishia fedha ya ada nimpeleke shule yenye walimu wanaojitambua.
 
Back
Top Bottom