Afrika Kusini na ubaguzi wa rangi, picha hii yazua taharuki


Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Messages
228
Likes
423
Points
80
Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2018
228 423 80
Mama wa mtoto katika shule ya awali ya Laerskool Schweizer-Reneke iliyopo katika jimbo la North West huko Afrika Kusini, amechukizwa vikali baada ya picha inayomuonesha mtoto wake wa kike na watoto wengine watatu wa Kiafrika wakiwa wamekaa peke yao mbali na watoto wengine wa kizungu kwenye darasa lao. Picha hiyo ambayo inasambaa kwa kasi mtandaoni, imesababisha hasira kubwa kwa raia wa nchi hiyo kutokana na kuwa na ishara ya ubaguzi wa rangi.

Picha hiyo ilitumwa kwenye kundi la WhatsApp la shule hiyo na mwalimu wa darasa. "Hii ilipaswa kuwa siku ya kufurahisha kwangu lakini sio,” amesema mzazi huyo. Mama huyo ambaye hakutajwa jina kulinda utambulisho wa mwanae, ameiambia tovuti ya TimesLIVE ya nchini humo kuwa siku ya kwanza katika darasa hilo ilianza vizuri.

Yeye na wazazi wengine waliwapeleka watoto wao na kuambiwa waondoke katika eneo la shule. Saa tatu asubuhi walitumiwa taarifa kutoka kwa mwalimu wa watoto hao kuhusu siku ilivyokwenda kupitia WhatsApp group. Picha hiyo ilionesha watoto 18 wa kizungu wakiwa darasani wamekaa dawati moja lililounganishwa katikati ya darasa, wakati watoto wanne wa Kiafrika wakiwa wamekaa kwenye dawati moja lililowekwa kwenye kona ya darasa hilo. "Nilichoona ni jumbe toka kwa wazazi wa kizungu wakisema asante asante kwenye WhatsApp group, lakini hakuna yeyote aliyesema kuhusu walivyotenganishwa,” alisema mzazi huyo.

Amesema baada ya kujadiliana na mzazi mwingine nje ya WhatsApp group, mzazi huyo aliwasiliana na mkuu wa shule kuuliza kuhusu ukaaji wa watoto hao darasani. TimesLIVE imedai mkuu huyo wa shule alisema hakuwa na taarifa za suala hilo. Wamedai kuwa wanasubiri jibu toka kwa shule hiyo.

Alipoulizwa kuhusu anavyojisikia kutokana na hali hiyo, mama huyo amesema ana matumaini kuwa mwanae mwenye umri wa miaka mitano bado ni mdogo kuweza kutambua kilichotokea.
"Lakini nimechukia,” alisema mama huyo aliyeahidi kuchukua hatua zaidi.

Source: Bongo5
skytanzania-20190109-0001-jpeg.990332
 
Zambotti

Zambotti

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2016
Messages
779
Likes
1,302
Points
180
Zambotti

Zambotti

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2016
779 1,302 180
Na mishule yote iliyopo huko, wao wenyewe ndo wameufuata ubaguzi
White trailer park trash vs Black affluent middle class. Darasa la watoto 21, tatu tu ni Weusi. Hapo Whitey is trying to send a message watoto Weusi hawatakiwi. Wakome kujipendekeza kwa Wazungu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
15,023
Likes
12,851
Points
280
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
15,023 12,851 280
Wazungu wamekuja kuturahisishia Maisha hebu fikirieni leo Wasingekuja Afrika..sorry kwa kusema hivi tungekuwa tunatemba kwa miguu Dar hadi Mbeya
 
C

chilubi

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
4,346
Likes
2,053
Points
280
C

chilubi

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
4,346 2,053 280
Kwanini mungu alituumba rangi tofaut? Tatizo linaanzia hapo kabla ya kuwalaum wazungu

Sent using Jamii Forums mobile app
“Oh men! Behold, We have created you all out of a male and a female, and have made you into nations and tribes, so that you might come to know one another. Verily, the noblest of you in the sight of Allah is the one who is most deeply conscious of Him. Behold, Allah is All-Knowing, All-Aware” (Quran 49:13).

Jibu lipo kwenye maandishi mekundu....

Kuna watu watafoka najua
 
C

chilubi

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
4,346
Likes
2,053
Points
280
C

chilubi

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
4,346 2,053 280
Wazungu wamekuja kuturahisishia Maisha hebu fikirieni leo Wasingekuja Afrika..sorry kwa kusema hivi tungekuwa tunatemba kwa miguu Dar hadi Mbeya
Akili kama hizi ndio maisha zitamfanya mwafrika awe mtegemezi mpaka atakufa. Mzungu/mwarabu/mchina/mhindi wamewezaje ata mwafrika ashindwe?
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
15,023
Likes
12,851
Points
280
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
15,023 12,851 280
Akili kama hizi ndio maisha zitamfanya mwafrika awe mtegemezi mpaka atakufa. Mzungu/mwarabu/mchina/mhindi wamewezaje ata mwafrika ashindwe?
Ukweli huwa ni mchungu!..angalia Nigeria Wanamafuta sawa na Kuwait lakini Mnigeria utamkuta ukimbizini South Afrika
 
C

chilubi

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
4,346
Likes
2,053
Points
280
C

chilubi

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
4,346 2,053 280
Ukweli huwa ni mchungu!..angalia Nigeria Wanamafuta sawa na Kuwait lakini Mnigeria utamkuta ukimbizini South Afrika
Hayo ni matokeo ya mentality ya Muafrika, Kusema kuwa bila Mzungu tusingekuwa na gari. Waafrika tunanyanyasana wenyewe kwa wenyewe. Ingekuwa tunapendana, nakuhakikishia, si mzungu, si mwarabu, si mhindi, si mchina, wangekuwa wanatupigia magoti.

Bara limejaaliwa kila aina ya natural resources, ardhi iliyojaa rutuba eti bado tunaomba hela nje!

Badilisha mtazamo wako na ujiamini kama unaweza!
 
KYALOSANGI

KYALOSANGI

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Messages
2,076
Likes
636
Points
280
KYALOSANGI

KYALOSANGI

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2011
2,076 636 280
hivi picha kama hii inaweza kueleza ubaguzi naikaeleweka /kuaminika.Pengine kungekuwa na maelezo ya ziada! unaweza kuona kuna ubaguzi wa Rangi ...kumbe na wewe unatazama hii picha ukiwa na roho ya kibaguzi !
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
15,023
Likes
12,851
Points
280
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
15,023 12,851 280
Bara limejaaliwa kila aina ya natural resources, ardhi iliyojaa rutu
Sasa unatulaumu au unajilaumu au unalaumu...Ukweli ni Mchungu!..Sisi waafrika ndio jamii pekee ambayo utakuta Usiku kucha tunakesha Kurogana Kijiji kinaroga Kinawaroga Kijiji cha Jirani jirani anamroga Jirani mwenzake..
 
James Comey

James Comey

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2017
Messages
3,791
Likes
4,846
Points
280
James Comey

James Comey

JF-Expert Member
Joined May 14, 2017
3,791 4,846 280
Sauzi Africa ni shida tuu. Mandela hakuna alilolifanya ktk suala la ubaguzi
fb_img_15471860188400665-jpeg.991706


Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
15,023
Likes
12,851
Points
280
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
15,023 12,851 280
145523514-612x612-jpg.991713

Mzungu kaja kuturahisishia maisha Ukweli Mchungu!
Sisi uvumbuzi wetu ni huo wa kuweka Bakuli mdomoni ili msaada uje direct ili tuumeze.
 

Forum statistics

Threads 1,250,110
Members 481,224
Posts 29,720,983