Afrika kushabikia ICC ni kama ushamba

Mkuu mtu mweusi ufahamu wake umedumaa kwa viwango vya kusikitisha.

Ni rahisi kumfanya mtu mjinga kuliko kumwambia amefanywa mjinga.

Wanachokiona hao wanaokupinga ni kubinywa kwa maslahi yao binafsi ya muda mfupi na sio future generations ila wangefikiria hilo wasingekupinga ila kwakuwa africans ni wajinga na ushabiki wa vyama pia kufuata mkumbo ndio sababu hawakuelewi.

Yote ni sababu ya maslahi binafsi wanayotaka wananchi wa kiafrika.
China ingekuwa na wananchi kama wa kiafrika basi pale wasingefika.

No wonder why kwa akili hizi tulifanywa watumwa na baadhi ya waafrika kuuza waafrika wenzao.

Sorry kusema hivi lakini hii inaprove kwamba africans ni wajinga.
Na nilikuwa sahihi na kuendelea kuwa sahihi kwamba mwafrika ni ufahamu wake umedumaa.

Nimeandika kama mwafrika na sio kwa itikadi za kisiasa.
 
Miaka yote tulikuwa tunasikia The Hague ila mwaka huu wameconfirm wamepokea vielelezo...sasa CCM wamechanganyikiwa na mwenyekiti wao kasawajika mtazame hata body language mambo hayako sawa..
 
Ahsante Sana mkuu kwa kujaribu kuleta hili, kiukweli tunapaswa kuamka, tupo katika usingizi mzito mno, giza zito, tupo katika dhoruba kubwa mnoo, tupo katika shimo refu, lakini tunaambiwa kuwa tukitoka katika hayo ni hatarii kwetu, nasi tunaamini , Sina mashaka na taifa langu maana tumeshaamua kusonga mbele, naamini tutafika tuu.
 
Ni kiongozi gani wa kiafrica aliyeshtakiwa kwenye Mahakama hii kwa mashtaka ya kusingiziwa???

Miafrica inaona raha kuua waafrica wenzao halaf wakishtakiwa mnasema figisu???

Waache kuua, waache kuiba kura...waache ukatili..pumbavu zao la sivyo acha yashtakiwe tu.
 
Wewe unashabikia yaliyokuwa yanafanywa na Bahir,Habre,Kenyatta na wengineo ktk nchi zao?Unanufaika na nini watu kuuliwa na kuteswa kisa hawakubaliani na jinsi tawala za nchi zao wanavyowatendea raia?
 
Kwanza kusema kwamba hii mahakama ni kwa ajili ya Afrika sio kweli kwani kuna watu wamewahi kuburuzwa kwenye hiyo mahakama ambao hawakuwa waafrika kama akina Slobodan Milosevic na Radvan Karadzic wote wa Serbia.

Afrika ni bara inayoongoza duniani kuwa na watawala wa kiimla na kwa bahati mbaya mwisho wa siku hata Tanzania nasi sasa tuna mtawala wa kiimla.

Kwa hali hii hakuna namna yoyote inaweza ikafanyika hawa madikteta watendewe haki kwani kwenye nchi zao kuna hata watu huthubutu kuwaabudu kama Mungu.

Wanaongoza serikali katili zinazoteka watu, kuwatesa na hata kuwaua pasipo hofu ya kufanywa chochote huku vyombo vyote vya kiutawala vikiwa chini yao. Kwa njia hii ICC ndio njia muafaka.
 
Mleta mada ameleta upuuzi wa ajabu. Ameandika mashairi yasiyokuwa na uthibitisho hata mmoja. Upyyzi mkubwa!

Hivi Wakenya waliposhtakiwa kutokana na mauaji yaliyotokana na mauaji wakati wa vita, wazungu walikuwa wanataka kuchukua rasilimali gani toka Kenya?

Tuna wengi wanaojua kusoma na kuandika lakini hawajatokwa na ujinga na uwendawazimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wizi huu ambao NEC inaruhusu karatasi za Kura kugawiwa mitaani Kama sio nyaraka za serikali,nivema wote waende ICC tumechoka kunyanyashwa na polisi kuitetea ccm
Alafu wagombea wa Upinzani wa Ubunge na Udiwani wanakamatwa na kufunguliwa makosa ya ujambazi na uhujumu Uchumi ili wakose dhamana eti wasigombee kwa sababu CCM wapite bila kupingwa.

Kwa tulipofikia acha tu wapelekwe ICC, mtu mweusi bila kudhibitiwa anakuwa na roho mbaya sana!
 
Mkuu mleta mada, humu jukwaani kuna Mawakala wa Wazungu wao kazi yao ni kuwatisha Watanzania.

Ni marafiki wa yule kaka wa MIGA, wameshindwa kabisa kuelewa kuwa awamu hii ni ya kizalendo na isiyokuwa na uoga wa kuyatetea maslahi mapana ya nchi.
 
Mleta mada ameleta upuuzi wa ajabu. Ameandika mashairi yasiyokuwa na uthibitisho hata mmoja. Upyyzi mkubwa!

Hivi Wakenya waliposhtakiwa kutokana na mauaji yaliyotokana na mauaji wakati wa vita, wazungu walikuwa wanataka kuchukua rasilimali gani toka Kenya?

Tuna wengi wanaojua kusoma na kuandika lakini hawajatokwa na ujinga na uwendawazimu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kenya kulikuwa na vita ya dhahiri ya kiukabila na walikufa watu zaidi ya elfu moja.

Lini Tanzania imetokea vita ya uchaguzi mpaka wakafa watu elfu moja, hatuna siasa za kiukabila wala za kimajimbo kama Ethiopia ya sasa.

Wapo mawakala wa wazungu wanajaribu kuivuruga hii nchi lakini hawataweza kwani ina misingi imara sana.
 
Ndabila, wandali ni wabinafsi sana. wewe Baba ako CCM, mama ako CCM, huwezi ona umuhimu wa ICC kwa wa Afrika.
 
Kenya kulikuwa na vita ya dhahiri ya kiukabila na walikufa watu zaidi ya elfu moja.

Lini Tanzania imetokea vita ya uchaguzi mpaka wakafa watu elfu moja, hatuna siasa za kiukabila wala za kimajimbo kama Ethiopia ya sasa.

Wapo mawakala wa wazungu wanajaribu kuivuruga hii nchi lakini hawataweza kwani ina misingi imara sana.
Angeuawa mama yako au mtoto wako ndiyo ungejua kuwa uhai hata wa mtu mmoja una thamani ya namna gani. Kwa sababu ndani yako kuna roho ya shetani inayokuongoza, na kwa vile waliouawa kinyama bila hatia na serikali ya kishetani siyo ndugu zako, huoni thamani ya uhai wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NI KAMA USHAMBA TU LEO AFRIKA KUSHABIKIA ICC?

Na Elius Ndabila
0768239284


Msamiati wa ICC umekuwa maarufu sana Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Ninaamini wapo ambao wanalitamka neno ICC wakiwa wanalijua vizuri na wapo ambao wameingia tu kwenye mkenge bila kujua. Leo nitawapitisha kidogo juu ya ICC ili tujue kama ni USHAMBA au ni Ujuvi kuendelea kushabikia hili.

Kwanza ICC(International Criminal Court) ni Mahakama iliyoanzishwa mwaka 2000 huko Rome kwa madhumuni ya kushitaki mauji ya Kimbari, hatia dhidi ya binadamu na hatia za kivita. Ilianzishwa baada ya majadiliano ya takilibani miaka mitatu.

Hii ndiyo ilikuwa tafsiri ya Mahakama hii. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa kuanzisha Mahakama hii ilikuwa ni akili kubwa ya Wazungu hasa waliokuwa na makoloni Afrika mwanzoni kutafuta mbinu mbadala ya kuendelea kuikalia Afrika kusaidiana na ukoloni Mambo leo. Waasisi wa hii Mahakama ni Ujerumanj ambayo ikumbukwe ilipitia kwenye misukosuko ya kiuchumi kwa mda mrefu baada ya bara la Afrika kuwa huru.

Ujerumani kushirikiana na Uingereza ndio walishikia bango kuanzisha kwa Mahakama hii kwa kuwa wao walikuwa na madhumuni makubwa mbali na yale yanayotajwa kwenye Rome Statutes. Wakati wa uanzishwaji nchi 34 za Afrika zilisaini, Ulaya 25 na visiwa vya Caraibean na Amerika 28 nazo zikijiunga.

Wakati mataifa hayo yakijiunga mataifa makubwa ambayo yalishajua kuwa lengo la Ujerumani, Uingereza na wafuasi wao ni kutaka kuendelea na ukoloni wao walikata kujiunga na Mahakama hiyo. Mataifa yaliyokata ni Marekani, China, Urus n.k ndiyo maana pamoja na Marekani kutuma Wanajeshi wake kuua, lakini haijawahi kushitakiwa kwa kuwa si wanachama wa Mahakama hii.

Kumbukumbu zinaonyesha tangu Mahakama hii kuanzishwa yaani miaka 20 sasa ICC imechunguza kesi 26 nyingi zikiwa bado ktk awamu ya majaribio, imetoa waranti 32 za kukamatwa, 15 zikitekelezwa na ina wafungwa 6 ambao wote wanazuiwa. Hukumu ya Kwanza ilikuwa ni mwaka 2014 tangu kuanzishwa. Kesi karibia zote zinatoka Aftika. Kitendo hiki ndicho kinatoa taswira kuwa Mahakama hii ilianzishwa kwa ajili ya bara la AFRIKA ambapo Mahakama hii imekuwa ikitumiwa na Wabaya wa nchi za Afrika kuzishitaki hasa pale wanapoona kiongozi aliyeshinda kwenye uchaguzi hata kidhi mahitaji yao ya kulinyonya bara la AFRIKA.

Ni Mahakama ambayo kwa nchi wanachama inatumika kama chambo cha ukadamizaji hasa unaposhindwa kutii matakwa yao. Ni Mahakama inayotoa vikwazo hasa economic sanction kwa nchi zinazoshindwa kufuata matwa yake.

Ukweli ni kuwa ili Afrika iweze kusonga mbele inahitaji kuwa na nguvu ya pamoja katka kutatua mambo yao. Duniani kote sasa wanaitegemea Afrika kwa rasilimali ya viwanda vyao. Sasa kazi kubwa ambayo sasa mataifa makubwa yanafanya ni kuhakikisha kuwa Afrika Wanafarakana, ni kuhakikisha kuwa wanatengeza makundi ndani ya nchi yatakayoleta misuguano ambayo itawarahisishia wao kupenyeza agenda zao. Mahakama hii imemezwa na bunge la EU.

Mwaka 2018 Rais wa Marekani Mh Donald Trump alitishia kupeleka hoja ya kuifuta Mahakama hii kandamizi. Na kwa kuonyesha u serious wa hilo waziri wa Mambo ya Kigeni Mh Mike Pompeo alitangaza kuwawekea vikwazo viongozi wa Mahakama hiyo wakiongozwa na MwanaMama Fatou Besouda waliokuwa wanajaribu kutishia kuwa wangeeashitaki wanajeshi wa Marekani.

Imefika mahali Waafrika tuamuke. Tuache usingizi wa akina Mangungo. Mahakama hizi hazina upendo na sisi Bali kwenye kutimiza matakwa yao. Ingekuwa ni Mahakama ya haki mungekuwa mnasikia na wao wanashitakiwa, lakini ile ni Mahakama ya Afrika ili kuendelea kutukandamiza. Tunayofursa ya kulijenga bara la AFRIKA kuwa zaidi ya Ulaya kwa kuwa tunazo rasilimali za kutosha kufanya hivyo. Tukiendelea kuwashobokea tutakuwa masikini milele, na watakomaliza kuvuna rasilimali zetu watatua vumbi.

Tafakari.
Dude refuuu lakini pumba tupu
Ccm kuna sifa ya upumbavu mkubwa haujapataonekana toka dunia iumbwe.

WASHAMBA NI SERIKALI YA CHAMA CCM WALIOSAINI MIKATABA YA KIMATAIFA.
 
Angeuawa mama yako au mtoto wako ndiyo ungejua kuwa uhai hata wa mtu mmoja una thamani ya namna gani. Kwa sababu ndani yako kuna roho ya shetani inayokuongoza, na kwa vile waliouawa kinyama bila hatia na serikali ya kishetani siyo ndugu zako, huoni thamani ya uhai wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuuwawa kumeanza kuwepo kabla mama yako hajazaliwa.

Wameuwawa watu enzi za Yesu kwa kukatwa vichwa wewe unashangaa watu kuuwawa leo.

Umeshasahau kuwa kibiti na Mkuranga watu waliuwawa! Au vifo vyao havina umuhimu?

Wanauwawa watu Msumbiji kila siku bila ya hatia au wao sio muhimu?.
 
Back
Top Bottom