Afrika kushabikia ICC ni kama ushamba

Afrika kushabikia ICC ni kama ushamba

Hakuna misingi imara wala matofali imara,ujinga wa wengi na unafki wa hawa wanaoitwa wasomi uchwara ambao kwao matumbo yamewekwa mbele kuliko chochote
Tanzania tutaitetea tu hata yakitungwa majina elfu moja ya dhihaka.

Ndio tuliyonayo haipo nyingine ya bandia.
 
Kama hayo ni makosa na yako ndani ya Rome Statue, wakashitakiwe. Uzuri wa ICC hata wewe unaweza kwenda

sasa wewe ulishawahi ona wap watu wenye akili ccm wakihangaika na mtu ambae hataki kuachia uenyekiti mpaka makamu wake anamkimbia
 
Uzalendo huu ulioletwa bongo unafanana na ule wa Mugabe kipindi kile yuko hai. Sioni tofauti yoyote, ni waase wabongo tuache mawazo haya ya kipuuzi. Kuendelea ni lazima tuwe na demokrasia ya kweli na tushirikiane na ulimwengu zikiwemo nchi zilizoendelea.

Hata kwa mfano iyo China au Urusi zina mahusiano mazuri tuu na Marekani. Sijuwi ni nchi gani ile ilio na maendeleo kwa kujifungia mipaka na kuanza kubandika majina kama mabeberu kwa kila taifa linalotoa makosa katika mfumo wetu wa kidemokrasia.
 
Ndio maana huko nyuma nimeuliza nani atampeleka Trump huko ICC? Maana kasababisha mpasuko mkubwa US.

Kamuua yule general wa Iraq pasipo ushahidi kuwekwa hadharani mpaka leo hii.

Nani atawapeleka Bush na Blair huko ICC wakashtakiwe kwa kumuua Saddam na kushindwa kuonyesha silaha za sumu zipo wapi?.

Magufuli hawezi kuwekwa kwenye kundi la hao niliowataja hapo juu.

Hizo siasa za kina Lissu na wapuuzi wengine ni nyepesi sana kwani wao ni vibaraka waliokubali kutumiwa kwa maslahi ya wanaowatuma.

Mkuu Magufuli ni rais mzalendo sana na sisi tunaojua kusudio lake tutamlinda kimwili na kiroho.
Kwani mmekazana kuongelea Marekani? Why not talk about Africa?

Hapo jirani tu Congo watu wanaumizwa kila siku, watapata wapi haki zao? Nyie mmekazana Bush and Blair.

Unaamini Bashir kushitakiwa ICC kwa genocide ya Darfur ni makosa pia?
 
Uzalendo huu ulioletwa bongo unafanana na ule wa Mugabe kipindi kile yuko hai. Sioni tofauti yoyote, ni waase wabongo tuache mawazo haya ya kipuuzi. Kuendelea ni lazima tuwe na demokrasia ya kweli na tushirikiane na ulimwengu zikiwemo nchi zilizoendelea.

Hata kwa mfano iyo China au Urusi zina mahusiano mazuri tuu na Marekani. Sijuwi ni nchi gani ile ilio na maendeleo kwa kujifungia mipaka na kuanza kubandika majina kama mabeberu kwa kila taifa linalotoa makosa katika mfumo wetu wa kidemokrasia.
Demokrasia ya haki lazima isimamiwe na Wazungu? Nenda ukasome historia ya China na ukamsome Confucius.....
 
NI KAMA USHAMBA TU LEO AFRIKA KUSHABIKIA ICC?

Na Elius Ndabila
0768239284

Msamiati wa ICC umekuwa maarufu sana Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Ninaamini wapo ambao wanalitamka neno ICC wakiwa wanalijua vizuri na wapo ambao wameingia tu kwenye mkenge bila kujua. Leo nitawapitisha kidogo juu ya ICC ili tujue kama ni USHAMBA au ni Ujuvi kuendelea kushabikia hili.

Kwanza ICC(International Criminal Court) ni Mahakama iliyoanzishwa mwaka 2000 huko Rome kwa madhumuni ya kushitaki mauji ya Kimbari, hatia dhidi ya binadamu na hatia za kivita. Ilianzishwa baada ya majadiliano ya takilibani miaka mitatu.

Hii ndiyo ilikuwa tafsiri ya Mahakama hii. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa kuanzisha Mahakama hii ilikuwa ni akili kubwa ya Wazungu hasa waliokuwa na makoloni Afrika mwanzoni kutafuta mbinu mbadala ya kuendelea kuikalia Afrika kusaidiana na ukoloni Mambo leo. Waasisi wa hii Mahakama ni Ujerumanj ambayo ikumbukwe ilipitia kwenye misukosuko ya kiuchumi kwa mda mrefu baada ya bara la Afrika kuwa huru.

Ujerumani kushirikiana na Uingereza ndio walishikia bango kuanzisha kwa Mahakama hii kwa kuwa wao walikuwa na madhumuni makubwa mbali na yale yanayotajwa kwenye Rome Statutes. Wakati wa uanzishwaji nchi 34 za Afrika zilisaini, Ulaya 25 na visiwa vya Caraibean na Amerika 28 nazo zikijiunga.

Wakati mataifa hayo yakijiunga mataifa makubwa ambayo yalishajua kuwa lengo la Ujerumani, Uingereza na wafuasi wao ni kutaka kuendelea na ukoloni wao walikata kujiunga na Mahakama hiyo. Mataifa yaliyokata ni Marekani, China, Urus n.k ndiyo maana pamoja na Marekani kutuma Wanajeshi wake kuua, lakini haijawahi kushitakiwa kwa kuwa si wanachama wa Mahakama hii.

Kumbukumbu zinaonyesha tangu Mahakama hii kuanzishwa yaani miaka 20 sasa ICC imechunguza kesi 26 nyingi zikiwa bado ktk awamu ya majaribio, imetoa waranti 32 za kukamatwa, 15 zikitekelezwa na ina wafungwa 6 ambao wote wanazuiwa. Hukumu ya Kwanza ilikuwa ni mwaka 2014 tangu kuanzishwa. Kesi karibia zote zinatoka Aftika. Kitendo hiki ndicho kinatoa taswira kuwa Mahakama hii ilianzishwa kwa ajili ya bara la AFRIKA ambapo Mahakama hii imekuwa ikitumiwa na Wabaya wa nchi za Afrika kuzishitaki hasa pale wanapoona kiongozi aliyeshinda kwenye uchaguzi hata kidhi mahitaji yao ya kulinyonya bara la AFRIKA.

Ni Mahakama ambayo kwa nchi wanachama inatumika kama chambo cha ukadamizaji hasa unaposhindwa kutii matakwa yao. Ni Mahakama inayotoa vikwazo hasa economic sanction kwa nchi zinazoshindwa kufuata matwa yake.

Ukweli ni kuwa ili Afrika iweze kusonga mbele inahitaji kuwa na nguvu ya pamoja katka kutatua mambo yao. Duniani kote sasa wanaitegemea Afrika kwa rasilimali ya viwanda vyao. Sasa kazi kubwa ambayo sasa mataifa makubwa yanafanya ni kuhakikisha kuwa Afrika Wanafarakana, ni kuhakikisha kuwa wanatengeza makundi ndani ya nchi yatakayoleta misuguano ambayo itawarahisishia wao kupenyeza agenda zao. Mahakama hii imemezwa na bunge la EU.

Mwaka 2018 Rais wa Marekani Mh Donald Trump alitishia kupeleka hoja ya kuifuta Mahakama hii kandamizi. Na kwa kuonyesha u serious wa hilo waziri wa Mambo ya Kigeni Mh Mike Pompeo alitangaza kuwawekea vikwazo viongozi wa Mahakama hiyo wakiongozwa na MwanaMama Fatou Besouda waliokuwa wanajaribu kutishia kuwa wangeeashitaki wanajeshi wa Marekani.

Imefika mahali Waafrika tuamuke. Tuache usingizi wa akina Mangungo. Mahakama hizi hazina upendo na sisi Bali kwenye kutimiza matakwa yao. Ingekuwa ni Mahakama ya haki mungekuwa mnasikia na wao wanashitakiwa, lakini ile ni Mahakama ya Afrika ili kuendelea kutukandamiza. Tunayofursa ya kulijenga bara la AFRIKA kuwa zaidi ya Ulaya kwa kuwa tunazo rasilimali za kutosha kufanya hivyo. Tukiendelea kuwashobokea tutakuwa masikini milele, na watakomaliza kuvuna rasilimali zetu watatua vumbi.

Tafakari.
Wewe mwenyewe hapo ulipo mshamba wa vitu jitu zima ovyo kabisa.
 
Kwani mmekazana kuongelea Marekani? Why not talk about Africa?

Hapo jirani tu Congo watu wanaumizwa kila siku, watapata wapi haki zao? Nyie mmekazana Bush and Blair.

Unaamini Bashir kushitakiwa ICC kwa genocide ya Darfur ni makosa pia?
Congo wanauana kwa kuwa kuna Madini. Maeneo mengi yenye rasilimali Wazungu wanatabia ya kutengeneza minyukano ili wapate mfereji wa kuiba rasilimali. Kwa nini hujiulizi mbona nchi ambazo hazina malighafi hakuna vita? In vast impoverished area they can't create a conflict bse there's nothing to gain
 
Kesi karibia zote zinatoka Aftika. Kitendo hiki ndicho kinatoa taswira kuwa Mahakama hii ilianzishwa kwa ajili ya bara la AFRIKA ambapo Mahakama hii imekuwa ikitumiwa na Wabaya wa nchi za Afrika kuzishitaki hasa pale wanapoona kiongozi aliyeshinda kwenye uchaguzi hata kidhi mahitaji yao ya kulinyonya bara la AFRIKA.
Afrika ni bara la giza. Waafrika bado hatujastaarabika. Wengi wa viongozi wa Afrika wakishapata madaraka ubinadamu unawatoka. Wanakua kama fisi, nguruwe. simba, panya and the like dhidi ya raia wao. Kiongoxi anageuka kua Mungu-mtu. Hataki tena kuondoka pindi anakataliwa kwny sanduku la kura. Ndio maana utaona kila aina ya uovu kwny chaguzi za Afrika- wapinza kunyanyaswa, kupigwa, kuuawa, kuibiwa kura nk. Rejea chaguzi za Tanzania, Uganda, Rwanda, Ivory Coast, Kenya, Drc nk. Ukiukwaji wa haki za binadamu ni mkubwa sana barani Afrika. uwepo wa mahama ya ICC ni muhimu sana kwa bara hili kuliko eneo lingine lolote la dunia hii, ili iwe zuio (deterrent) kwa hawa madikteta ambao wako tayar kuona damu isiyo na hatia inamwagika kwaajili ya maslahi yao binafsi. Ni Afrika tuu kiongozi anaweza kukukaa madarkan miaka hata 40, sio kwa mapenzi ya raia bali kwa kutumia majeshi na kila aina vitisho nadhuluma. Btw, hivi ni kweli mh. wetu alitamka: 'Nikuteue mimi, nikulipe vizuri, nikupe nyumba na gari; halafu umtangaze mpinzani ameshinda. Nitakushanga sana'?
 
Kesi karibia zote zinatoka Aftika. Kitendo hiki ndicho kinatoa taswira kuwa Mahakama hii ilianzishwa kwa ajili ya bara la AFRIKA ambapo Mahakama hii imekuwa ikitumiwa na Wabaya wa nchi za Afrika kuzishitaki hasa pale wanapoona kiongozi aliyeshinda kwenye uchaguzi hata kidhi mahitaji yao ya kulinyonya bara la AFRIKA.
Ushenzi na unyang'au mfanye wenyewe halafu mnaanza kumtafuta mchawi nani?

Africa ni bara la giza.
 
Congo wanauana kwa kuwa kuna Madini. Maeneo mengi yenye rasilimali Wazungu wanatabia ya kutengeneza minyukano ili wapate mfereji wa kuiba rasilimali. Kwa nini hujiulizi mbona nchi ambazo hazina malighafi hakuna vita? In vast impoverished area they can't create a conflict bse there's nothing to gain
Naona unaenda nje ya mada.... tuongee kuhusu ICC

Vipi mauaji ya Kenya baada ya uchaguzi? Ilikuwa madini pia? Wazungu ndio walitengeneza Post Election Violence ya Kenya?
 
Mmeteua majaji wote wapo ccm sasa unataka twende wapi. hiyo ndo dawa yenu, na bado
 
Congo wanauana kwa kuwa kuna Madini. Maeneo mengi yenye rasilimali Wazungu wanatabia ya kutengeneza minyukano ili wapate mfereji wa kuiba rasilimali. Kwa nini hujiulizi mbona nchi ambazo hazina malighafi hakuna vita? In vast impoverished area they can't create a conflict bse there's nothing to gain
Suala la rasilimali linageuzwa kichaka cha madikteta kujificha wakisingizia kulinda rasilimali. Kuna nchi za afrika hazina rasilimali nyingi kivile lakini zina chafuko, vita- Somalia, Msumbiji, CAR, Ethiopia, Mali. Na kuna nchi zenye rasilimali nyingi lakini zina utulivu- SA, Ghana, Angola, nk. Nchi hizi zina demokrasia. Sii kweli keep la mgogoro unasababishwa na wazungu, mingine inatengenezwa na viongozi wa Afrika ili watumie mkono wa chuma kubakia madarakani.
 
Back
Top Bottom