Afrika kushabikia ICC ni kama ushamba

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
NI KAMA USHAMBA TU LEO AFRIKA KUSHABIKIA ICC?

Na Elius Ndabila
0768239284


Msamiati wa ICC umekuwa maarufu sana Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Ninaamini wapo ambao wanalitamka neno ICC wakiwa wanalijua vizuri na wapo ambao wameingia tu kwenye mkenge bila kujua. Leo nitawapitisha kidogo juu ya ICC ili tujue kama ni USHAMBA au ni Ujuvi kuendelea kushabikia hili.

Kwanza ICC(International Criminal Court) ni Mahakama iliyoanzishwa mwaka 2000 huko Rome kwa madhumuni ya kushitaki mauji ya Kimbari, hatia dhidi ya binadamu na hatia za kivita. Ilianzishwa baada ya majadiliano ya takilibani miaka mitatu.

Hii ndiyo ilikuwa tafsiri ya Mahakama hii. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa kuanzisha Mahakama hii ilikuwa ni akili kubwa ya Wazungu hasa waliokuwa na makoloni Afrika mwanzoni kutafuta mbinu mbadala ya kuendelea kuikalia Afrika kusaidiana na ukoloni Mambo leo. Waasisi wa hii Mahakama ni Ujerumanj ambayo ikumbukwe ilipitia kwenye misukosuko ya kiuchumi kwa mda mrefu baada ya bara la Afrika kuwa huru.

Ujerumani kushirikiana na Uingereza ndio walishikia bango kuanzisha kwa Mahakama hii kwa kuwa wao walikuwa na madhumuni makubwa mbali na yale yanayotajwa kwenye Rome Statutes. Wakati wa uanzishwaji nchi 34 za Afrika zilisaini, Ulaya 25 na visiwa vya Caraibean na Amerika 28 nazo zikijiunga.

Wakati mataifa hayo yakijiunga mataifa makubwa ambayo yalishajua kuwa lengo la Ujerumani, Uingereza na wafuasi wao ni kutaka kuendelea na ukoloni wao walikata kujiunga na Mahakama hiyo. Mataifa yaliyokata ni Marekani, China, Urus n.k ndiyo maana pamoja na Marekani kutuma Wanajeshi wake kuua, lakini haijawahi kushitakiwa kwa kuwa si wanachama wa Mahakama hii.

Kumbukumbu zinaonyesha tangu Mahakama hii kuanzishwa yaani miaka 20 sasa ICC imechunguza kesi 26 nyingi zikiwa bado ktk awamu ya majaribio, imetoa waranti 32 za kukamatwa, 15 zikitekelezwa na ina wafungwa 6 ambao wote wanazuiwa. Hukumu ya Kwanza ilikuwa ni mwaka 2014 tangu kuanzishwa. Kesi karibia zote zinatoka Aftika. Kitendo hiki ndicho kinatoa taswira kuwa Mahakama hii ilianzishwa kwa ajili ya bara la AFRIKA ambapo Mahakama hii imekuwa ikitumiwa na Wabaya wa nchi za Afrika kuzishitaki hasa pale wanapoona kiongozi aliyeshinda kwenye uchaguzi hata kidhi mahitaji yao ya kulinyonya bara la AFRIKA.

Ni Mahakama ambayo kwa nchi wanachama inatumika kama chambo cha ukadamizaji hasa unaposhindwa kutii matakwa yao. Ni Mahakama inayotoa vikwazo hasa economic sanction kwa nchi zinazoshindwa kufuata matwa yake.

Ukweli ni kuwa ili Afrika iweze kusonga mbele inahitaji kuwa na nguvu ya pamoja katka kutatua mambo yao. Duniani kote sasa wanaitegemea Afrika kwa rasilimali ya viwanda vyao. Sasa kazi kubwa ambayo sasa mataifa makubwa yanafanya ni kuhakikisha kuwa Afrika Wanafarakana, ni kuhakikisha kuwa wanatengeza makundi ndani ya nchi yatakayoleta misuguano ambayo itawarahisishia wao kupenyeza agenda zao. Mahakama hii imemezwa na bunge la EU.

Mwaka 2018 Rais wa Marekani Mh Donald Trump alitishia kupeleka hoja ya kuifuta Mahakama hii kandamizi. Na kwa kuonyesha u serious wa hilo waziri wa Mambo ya Kigeni Mh Mike Pompeo alitangaza kuwawekea vikwazo viongozi wa Mahakama hiyo wakiongozwa na MwanaMama Fatou Besouda waliokuwa wanajaribu kutishia kuwa wangeeashitaki wanajeshi wa Marekani.

Imefika mahali Waafrika tuamuke. Tuache usingizi wa akina Mangungo. Mahakama hizi hazina upendo na sisi Bali kwenye kutimiza matakwa yao. Ingekuwa ni Mahakama ya haki mungekuwa mnasikia na wao wanashitakiwa, lakini ile ni Mahakama ya Afrika ili kuendelea kutukandamiza. Tunayofursa ya kulijenga bara la AFRIKA kuwa zaidi ya Ulaya kwa kuwa tunazo rasilimali za kutosha kufanya hivyo. Tukiendelea kuwashobokea tutakuwa masikini milele, na watakomaliza kuvuna rasilimali zetu watatua vumbi.

Tafakari.
 
Nani kafungwa au kushtakiwa ICC kwa uonevu?

Ukweli ni kwamba kati ya nchi wanachama, Afrika ndiyo ina watuhumiwa/wahalifu wengi, so it's a no brainer kuona wanaoshughulikiwa zaidi ni Waafrika.

USA, China, Urusi hawakujiunga sio sababu wanaipenda sana Afrika au kushtukua mpango wa ICC bali waliweka maslahi yao wenyewe mbele. Kwanini ujiunge na a 'big brother' who watches over you wakati unaweza kufanya yako kwa uhuru bila kelele za mtu.
 
Mwalimu Nyerere alisema madikteta kwa sasa wamebaki Afrika! Kwa hiyo unaona yaliyofanyika Rwanda Ni sawa? Au ya Sudan? Tukubaliane kwamba watawala Wa Afrika wanaoneana haya, kama ilivyokuwa kwa Mugabe. Mpaka watawaliwe wacharuke ndiyo ujue yanayendelea siyo sawa. Usionyeshe mapenzi kwa watawala wanaolazimisha kutawala kwa nguvu za kijeshi huku wakiumiza raia
 
Kichwa Cha habari na yaliyomo havinasibiani. Nilidhani utaeleza ubutu wa mahakama hii ktk kushughulikia kesi. Kumbe unalalamikia Afrika kuonewa??

Afrika haionewi, bali wavunja haki za binadamu, katiba za nchi na kusababisha vita wapo Afrika zaidi.

Acha waje wawashughulikie ili wanyooke.
 
Watu hawana imani ni mifumo ya utoaji haki katika nchi zao ndio maana wanaona mahakama hiyo kama sehemu wanayiweza kupata haki licha ya mapungufu waliyonayo!
Ningekuona wa maana kama ungewaamsha watawala waweke mifumo imara ambayo itakuwa na mamlaka kamili ya kutoa haki bila kuwa na mipaka!Sasa hapa nchini,Rais hata afanye nini huwezi kumshitaki popote pale hata akitoka madarakani katika mahakama zetu!Kwa hali kama hiyo kwanini watu wasione ICC kama mkombozi kwa yale yanayoshindikana nchini?
Yaani ndugu zetu wauwawe kisa kura halafu tukae tu kimya na huo ndio unakuwa uzalendo!!!!!Haiwezekani!
 
Kwa aina ya watawala tulionao Afrika njia pekee ni ICC na huo sio ushamba Bali viongozi wa Afrika wakiachwa bila kufungwa gavana watafanya Mambo ya ajabu Sana na njia pekee ni the Hague
 
Back
Top Bottom