Afrika kushabikia ICC ni kama ushamba

Je hiyo inahalalisha hawa wa kwetu nao wafanye ukatili kama huo?

not at all, but kwenda kupeleka malalamiko kwao that's even much awkward, yaani unenda kuripoti kesi yako kwa jambazi kwamba kuna mmwizi kakuibia? what type of madness is this
 
Mkuu mtu mweusi ufahamu wake umedumaa kwa viwango vya kusikitisha.

Ni rahisi kumfanya mtu mjinga kuliko kumwambia amefanywa mjinga.

Wanachokiona hao wanaokupinga ni kubinywa kwa maslahi yao binafsi ya muda mfupi na sio future generations ila wangefikiria hilo wasingekupinga ila kwakuwa africans ni wajinga na ushabiki wa vyama pia kufuata mkumbo ndio sababu hawakuelewi.

Yote ni sababu ya maslahi binafsi wanayotaka wananchi wa kiafrika.
China ingekuwa na wananchi kama wa kiafrika basi pale wasingefika.

No wonder why kwa akili hizi tulifanywa watumwa na baadhi ya waafrika kuuza waafrika wenzao.

Sorry kusema hivi lakini hii inaprove kwamba africans ni wajinga.
Na nilikuwa sahihi na kuendelea kuwa sahihi kwamba mwafrika ni ufahamu wake umedumaa.

Nimeandika kama mwafrika na sio kwa itikadi za kisiasa.
Ni kweli waafrika ni wajinga. Mfano halisi ni wewe. Kama sio mjinga ni mnafiki wa hali yajuu sana. Jaribu kupitia scenario hizi: Tanzania- tangu 2015, Ben Saanane, Alphonse Mawazo, Daudi Mwangosi, Akwilina, Tundu Lissu nawengine, nini kiliwakuta? Wamepata haki? Kenya- baada ya uchaguzi wa 2007 machafuko yaliyofuatia watu wangapi walikufa? wangapi walikua wakimbizi nchini kwao? wangapi walibakwa, walilemazwa, walibaki yatima nk? Sudan- ktk mgogoro wa Dafur watu wangapi wameteswa,wamebakwa, wamepotea, wameuawa, wamekimbia nchi yao nk? Ivory Coast- Baada ya Laurent Gbagbo kushindwa uchaguzi alikubali? Nini kilifata? Ni machafuko, mauaji. Ghambia- Yahaya Jameh alikubali kashindwa uchaguzi, siku moja baadaye, baada ya kushauriwa na wapambe wake akabadilika na kutangaza kufuta ule uchaguzi. Hiyo ndio mifano halisi ya viongozi wa Afrika. Na mifumo ya sheria na katiba ktk Afrika sio rafiki. Mfano: Rais anateua majaji, wakuu wa vyombo vya ulinz na usalama, wakuu wa wilaya namikoa, m/kiti na wajumbe wa tume ya uchaguzi nk. Halafu wakati wa uchaguzi naye ni mgombea. Kwa vyovyote vile hawa watendaji watampendelea boss wao. Hayo yanapotokea na mifumo ya sheria ktk nchi husika haiwezi kuyadhughulikia suluhisho ni ICC.
 
Serikali inafanya kila liwezekanalo kulinda raia wake.

Lakini inaundwa na binadamu wenye udhaifu wa kila aina, lengo la jumla ni jema ingawa upungufu haukwepeki.
Kwa hiyo hiyo serikali iliyoundwa na wadamu inapotokea imekengeuka na kuwadhuru wananchi tutakimbilia wapi kama sio ICC?
 
NI KAMA USHAMBA TU LEO AFRIKA KUSHABIKIA ICC?

Na Elius Ndabila
0768239284


Msamiati wa ICC umekuwa maarufu sana Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Ninaamini wapo ambao wanalitamka neno ICC wakiwa wanalijua vizuri na wapo ambao wameingia tu kwenye mkenge bila kujua. Leo nitawapitisha kidogo juu ya ICC ili tujue kama ni USHAMBA au ni Ujuvi kuendelea kushabikia hili.

Kwanza ICC(International Criminal Court) ni Mahakama iliyoanzishwa mwaka 2000 huko Rome kwa madhumuni ya kushitaki mauji ya Kimbari, hatia dhidi ya binadamu na hatia za kivita. Ilianzishwa baada ya majadiliano ya takilibani miaka mitatu.

Hii ndiyo ilikuwa tafsiri ya Mahakama hii. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa kuanzisha Mahakama hii ilikuwa ni akili kubwa ya Wazungu hasa waliokuwa na makoloni Afrika mwanzoni kutafuta mbinu mbadala ya kuendelea kuikalia Afrika kusaidiana na ukoloni Mambo leo. Waasisi wa hii Mahakama ni Ujerumanj ambayo ikumbukwe ilipitia kwenye misukosuko ya kiuchumi kwa mda mrefu baada ya bara la Afrika kuwa huru.

Ujerumani kushirikiana na Uingereza ndio walishikia bango kuanzisha kwa Mahakama hii kwa kuwa wao walikuwa na madhumuni makubwa mbali na yale yanayotajwa kwenye Rome Statutes. Wakati wa uanzishwaji nchi 34 za Afrika zilisaini, Ulaya 25 na visiwa vya Caraibean na Amerika 28 nazo zikijiunga.

Wakati mataifa hayo yakijiunga mataifa makubwa ambayo yalishajua kuwa lengo la Ujerumani, Uingereza na wafuasi wao ni kutaka kuendelea na ukoloni wao walikata kujiunga na Mahakama hiyo. Mataifa yaliyokata ni Marekani, China, Urus n.k ndiyo maana pamoja na Marekani kutuma Wanajeshi wake kuua, lakini haijawahi kushitakiwa kwa kuwa si wanachama wa Mahakama hii.

Kumbukumbu zinaonyesha tangu Mahakama hii kuanzishwa yaani miaka 20 sasa ICC imechunguza kesi 26 nyingi zikiwa bado ktk awamu ya majaribio, imetoa waranti 32 za kukamatwa, 15 zikitekelezwa na ina wafungwa 6 ambao wote wanazuiwa. Hukumu ya Kwanza ilikuwa ni mwaka 2014 tangu kuanzishwa. Kesi karibia zote zinatoka Aftika. Kitendo hiki ndicho kinatoa taswira kuwa Mahakama hii ilianzishwa kwa ajili ya bara la AFRIKA ambapo Mahakama hii imekuwa ikitumiwa na Wabaya wa nchi za Afrika kuzishitaki hasa pale wanapoona kiongozi aliyeshinda kwenye uchaguzi hata kidhi mahitaji yao ya kulinyonya bara la AFRIKA.

Ni Mahakama ambayo kwa nchi wanachama inatumika kama chambo cha ukadamizaji hasa unaposhindwa kutii matakwa yao. Ni Mahakama inayotoa vikwazo hasa economic sanction kwa nchi zinazoshindwa kufuata matwa yake.

Ukweli ni kuwa ili Afrika iweze kusonga mbele inahitaji kuwa na nguvu ya pamoja katka kutatua mambo yao. Duniani kote sasa wanaitegemea Afrika kwa rasilimali ya viwanda vyao. Sasa kazi kubwa ambayo sasa mataifa makubwa yanafanya ni kuhakikisha kuwa Afrika Wanafarakana, ni kuhakikisha kuwa wanatengeza makundi ndani ya nchi yatakayoleta misuguano ambayo itawarahisishia wao kupenyeza agenda zao. Mahakama hii imemezwa na bunge la EU.

Mwaka 2018 Rais wa Marekani Mh Donald Trump alitishia kupeleka hoja ya kuifuta Mahakama hii kandamizi. Na kwa kuonyesha u serious wa hilo waziri wa Mambo ya Kigeni Mh Mike Pompeo alitangaza kuwawekea vikwazo viongozi wa Mahakama hiyo wakiongozwa na MwanaMama Fatou Besouda waliokuwa wanajaribu kutishia kuwa wangeeashitaki wanajeshi wa Marekani.

Imefika mahali Waafrika tuamuke. Tuache usingizi wa akina Mangungo. Mahakama hizi hazina upendo na sisi Bali kwenye kutimiza matakwa yao. Ingekuwa ni Mahakama ya haki mungekuwa mnasikia na wao wanashitakiwa, lakini ile ni Mahakama ya Afrika ili kuendelea kutukandamiza. Tunayofursa ya kulijenga bara la AFRIKA kuwa zaidi ya Ulaya kwa kuwa tunazo rasilimali za kutosha kufanya hivyo. Tukiendelea kuwashobokea tutakuwa masikini milele, na watakomaliza kuvuna rasilimali zetu watatua vumbi.

Tafakari.
Tungependa tuwe na tume huru na zinazo tenda haki ambazo hazipo
 
Mwenyekiti wa nini mkuu?

Yaani wewe unaona vyama kwenye kila kitu. Sio kila mtu ana chama ndugu... jadili hoja kama huwezi usijaze server.

wewe ni hater wa ccm, mtu anajadili hoja utamjua tu, mfano kuna dogo mmoja anaitwa tindo yuko humu, ni chadema lakini anajadili hoja, mtu kama huyo ndo hata akisema hana chama ndo unaweza kumwamini sasa nyie kamanda uchwara mnataka kusema nn
 
wewe ni hater wa ccm, mtu anajadili hoja utamjua tu, mfano kuna dogo mmoja anaitwa tindo yuko humu, ni chadema lakini anajadili hoja, mtu kama huyo ndo hata akisema hana chama ndo unaweza kumwamini sasa nyie kamanda uchwara mnataka kusema nn
Umeshinda wewe
 
Kwani mmekazana kuongelea Marekani? Why not talk about Africa?

Hapo jirani tu Congo watu wanaumizwa kila siku, watapata wapi haki zao? Nyie mmekazana Bush and Blair.

Unaamini Bashir kushitakiwa ICC kwa genocide ya Darfur ni makosa pia?
Usifananishe Congo na Tanzania. Ni nchi mbili tofauti.

Sisi tunawapokea wakimbizi kutoka afrika inayotuzunguka. Kuna jitihada za kuichafua Tanzania lakini zinafeli na zinaendelea kufeli.

Naiongelea US ili kuonyesha utumwa wetu wa kimawazo, kujiona tuna makosa na kujiona wadogo mbele ya wazungu.
 
Kwa hiyo hiyo serikali iliyoundwa na wadamu inapotokea imekengeuka na kuwadhuru wananchi tutakimbilia wapi kama sio ICC?
ICC hawawezi kusikiliza ujinga hata siku moja.

Wakati kura zinatangazwa na Kaijage walikuwepo wazungu wa huko huko Ulaya ndani ya ukumbi.

Magufuli sio wa kutingishwa kizembe inabidi wanaomjaribu wajipange haswa.
 
Hofu ya ICC hofu ya kunyimwa misaada ndio angalau kidogo uwafanya watawala wa kiafrica wapunguze kuuwa waafrika bila hayo wangetugeuza bucha usiku na mchana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom