Afrika kushabikia ICC ni kama ushamba

Afrika kushabikia ICC ni kama ushamba

Waswahili wanasema "Aliyekula ndizi hawezi kukumbuka, aliyezoa maganda hawezi kusahau"

Ni rahisi kusema ICC imekuja kuleta ukoloni hapa Africa, ila siku moja ukiwa victim wa serikali/wanasiasa wa Afrika ndio utaelewa kwanini kuna umuhimu wa hivi vyombo.

Binafsi nilikuwa na mtazamo kama wako, ila nilikuja kufahamiana na mtu ambaye alikuwa victim wa Al Bashir huko Darfur. Siku alipoamua kufunguka kuhusu mambo aliyopitia na yaliyomfanya akimbie kwao, nilibadilisha kabisa mtazamo. Kuna mambo hata kusimuliwa yanatisha. Siku wao wanakimbia na gari wakafika sehemu kuna checkpoint ya Janjaweed, walitolewa wote [baba mama na watoto 5]. Walichinjwa wazazi na kaka zake, akabaki yeye na mdogo wake wa kike; ndio wakaambiwa ondokeni kwa miguu... kuna mambo yanatisha.
 
Kuuwawa kumeanza kuwepo kabla mama yako hajazaliwa.

Wameuwawa watu enzi za Yesu kwa kukatwa vichwa wewe unashangaa watu kuuwawa leo.

Umeshasahau kuwa kibiti na Mkuranga watu waliuwawa! Au vifo vyao havina umuhimu?

Wanauwawa watu Msumbiji kila siku bila ya hatia au wao sio muhimu?.
Umewahi kuwa victim wa serikali/wanasiasa?
 
Hii idea ya kila kitu kukimbilia ukoloni ikoje hii ? Naona imekolea sana siku za karibuni, kiukweli nchi changa kama za Africa zinahitaji hio mahakama. Unadhani mauaji kama yale ya Rwanda nani ataweza kusimamia, atoke ndani ya Rwanda ?
 
Mleta mada ni mpumbavu kiwango cha phd.Wakat Tz tunaridhia kujiunga na hizi mahakama tulilazimishwa.Km kuna mambo yanayostahili sisi kuchunguzwa acha tuchunguzwe na hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wahusika.
NAONA UNATUMIA MASABURI KUFIKIRI.Kumbafu.
 
NI KAMA USHAMBA TU LEO AFRIKA KUSHABIKIA ICC?

Na Elius Ndabila
0768239284

Msamiati wa ICC umekuwa maarufu sana Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Ninaamini wapo ambao wanalitamka neno ICC wakiwa wanalijua vizuri na wapo ambao wameingia tu kwenye mkenge bila kujua. Leo nitawapitisha kidogo juu ya ICC ili tujue kama ni USHAMBA au ni Ujuvi kuendelea kushabikia hili.

Kwanza ICC(International Criminal Court) ni Mahakama iliyoanzishwa mwaka 2000 huko Rome kwa madhumuni ya kushitaki mauji ya Kimbari, hatia dhidi ya binadamu na hatia za kivita. Ilianzishwa baada ya majadiliano ya takilibani miaka mitatu.

Hii ndiyo ilikuwa tafsiri ya Mahakama hii. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa kuanzisha Mahakama hii ilikuwa ni akili kubwa ya Wazungu hasa waliokuwa na makoloni Afrika mwanzoni kutafuta mbinu mbadala ya kuendelea kuikalia Afrika kusaidiana na ukoloni Mambo leo. Waasisi wa hii Mahakama ni Ujerumanj ambayo ikumbukwe ilipitia kwenye misukosuko ya kiuchumi kwa mda mrefu baada ya bara la Afrika kuwa huru.

Ujerumani kushirikiana na Uingereza ndio walishikia bango kuanzisha kwa Mahakama hii kwa kuwa wao walikuwa na madhumuni makubwa mbali na yale yanayotajwa kwenye Rome Statutes. Wakati wa uanzishwaji nchi 34 za Afrika zilisaini, Ulaya 25 na visiwa vya Caraibean na Amerika 28 nazo zikijiunga.

Wakati mataifa hayo yakijiunga mataifa makubwa ambayo yalishajua kuwa lengo la Ujerumani, Uingereza na wafuasi wao ni kutaka kuendelea na ukoloni wao walikata kujiunga na Mahakama hiyo. Mataifa yaliyokata ni Marekani, China, Urus n.k ndiyo maana pamoja na Marekani kutuma Wanajeshi wake kuua, lakini haijawahi kushitakiwa kwa kuwa si wanachama wa Mahakama hii.

Kumbukumbu zinaonyesha tangu Mahakama hii kuanzishwa yaani miaka 20 sasa ICC imechunguza kesi 26 nyingi zikiwa bado ktk awamu ya majaribio, imetoa waranti 32 za kukamatwa, 15 zikitekelezwa na ina wafungwa 6 ambao wote wanazuiwa. Hukumu ya Kwanza ilikuwa ni mwaka 2014 tangu kuanzishwa. Kesi karibia zote zinatoka Aftika. Kitendo hiki ndicho kinatoa taswira kuwa Mahakama hii ilianzishwa kwa ajili ya bara la AFRIKA ambapo Mahakama hii imekuwa ikitumiwa na Wabaya wa nchi za Afrika kuzishitaki hasa pale wanapoona kiongozi aliyeshinda kwenye uchaguzi hata kidhi mahitaji yao ya kulinyonya bara la AFRIKA.

Ni Mahakama ambayo kwa nchi wanachama inatumika kama chambo cha ukadamizaji hasa unaposhindwa kutii matakwa yao. Ni Mahakama inayotoa vikwazo hasa economic sanction kwa nchi zinazoshindwa kufuata matwa yake.

Ukweli ni kuwa ili Afrika iweze kusonga mbele inahitaji kuwa na nguvu ya pamoja katka kutatua mambo yao. Duniani kote sasa wanaitegemea Afrika kwa rasilimali ya viwanda vyao. Sasa kazi kubwa ambayo sasa mataifa makubwa yanafanya ni kuhakikisha kuwa Afrika Wanafarakana, ni kuhakikisha kuwa wanatengeza makundi ndani ya nchi yatakayoleta misuguano ambayo itawarahisishia wao kupenyeza agenda zao. Mahakama hii imemezwa na bunge la EU.

Mwaka 2018 Rais wa Marekani Mh Donald Trump alitishia kupeleka hoja ya kuifuta Mahakama hii kandamizi. Na kwa kuonyesha u serious wa hilo waziri wa Mambo ya Kigeni Mh Mike Pompeo alitangaza kuwawekea vikwazo viongozi wa Mahakama hiyo wakiongozwa na MwanaMama Fatou Besouda waliokuwa wanajaribu kutishia kuwa wangeeashitaki wanajeshi wa Marekani.

Imefika mahali Waafrika tuamuke. Tuache usingizi wa akina Mangungo. Mahakama hizi hazina upendo na sisi Bali kwenye kutimiza matakwa yao. Ingekuwa ni Mahakama ya haki mungekuwa mnasikia na wao wanashitakiwa, lakini ile ni Mahakama ya Afrika ili kuendelea kutukandamiza. Tunayofursa ya kulijenga bara la AFRIKA kuwa zaidi ya Ulaya kwa kuwa tunazo rasilimali za kutosha kufanya hivyo. Tukiendelea kuwashobokea tutakuwa masikini milele, na watakomaliza kuvuna rasilimali zetu watatua vumbi.

Tafakari.
Umeongea upuuzi, kama icc wamethubutu kutaka kushitaki hao wanajeshi wa marekani kwanin unasema eti icc ipo kwa afrika tu?
 
Nafuata sheria kadri ya uwezo wangu wote, kadri niwezavyo.
Vizuri.... wewe unadhani kila anayeumizwa na wanasiasa hakufuata sheria?

Unadhani wananchi wa Congo Mashariki wooote ni wahalifu?
Unadhani wananchi wa Darfur wooote ni wahalifu?
Au Wakenya walioathirika na vurugu za baada ya uchaguzi 2007 walikuwa hawafuati sheria?

ICC kazi yake ndio hiyo, kuwapatia haki watu ambao serikali zao hazina uwezo au nia ya kuwapa haki. Tusiangalie sana kuhusu Marekani na Ulaya, tuwaze kuhusu sisi, leo hii ikitokea Serikali imeanza kudhuru raia wake, wewe unadhani utaenda wapi kupata haki?
 
Serikali inafanya kila liwezekanalo kulinda raia wake.

Lakini inaundwa na binadamu wenye udhaifu wa kila aina, lengo la jumla ni jema ingawa upungufu haukwepeki.
 
unapozungumzia haki za binadam, ni pamoja na wale waliofukuzwa bungeni kipindi cha corona pia, na wale wanaotishiwa maisha wakitaka kua wenyekiti, haki za binadam sio kuuliwa tu
 
Mbona wamarekani wameua sana tu hapo Uarabuni tena wakina mama na watoto lakini hawajashitakiwa? Nisaidie mkuu ili nielewe!

Relax king, hwa machalii tutawashuhulikia vizuri wnaaopiga kelele pale ufipa! Wao wakishapata uteuzi wao basi uchaguzi ulikua huru na haki sasa safari hii tutawaweka fimbo vizuri
 
Serikali inafanya kila liwezekanalo kulinda raia wake.

Lakini inaundwa na binadamu wenye udhaifu wa kila aina, lengo la jumla ni jema ingawa upungufu haukwepeki.
Ndugu unaongea kama vile unaishi kwenye kisiwa. Unalolisema ni wakati zinatimiza wajibu wake, ICC ipo kwa ajili ya serikali au viongozi wanaokwenda kinyume.

Nimekupa mfano wa Darfur, labda nikuulize watu waliopata madhara huko haki wakapate wapi?
 
unapozungumzia haki za binadam, ni pamoja na wale waliofukuzwa bungeni kipindi cha corona pia, na wale wanaotishiwa maisha wakitaka kua wenyekiti, haki za binadam sio kuuliwa tu
Kama hayo ni makosa na yako ndani ya Rome Statue, wakashitakiwe. Uzuri wa ICC hata wewe unaweza kwenda
 
Ndugu unaongea kama vile unaishi kwenye kisiwa. Unalolisema ni wakati zinatimiza wajibu wake, ICC ipo kwa ajili ya serikali au viongozi wanaokwenda kinyume.

Nimekupa mfano wa Darfur, labda nikuulize watu waliopata madhara huko haki wakapate wapi?
Ndio maana huko nyuma nimeuliza nani atampeleka Trump huko ICC? Maana kasababisha mpasuko mkubwa US.

Kamuua yule general wa Iraq pasipo ushahidi kuwekwa hadharani mpaka leo hii.

Nani atawapeleka Bush na Blair huko ICC wakashtakiwe kwa kumuua Saddam na kushindwa kuonyesha silaha za sumu zipo wapi?.

Magufuli hawezi kuwekwa kwenye kundi la hao niliowataja hapo juu.

Hizo siasa za kina Lissu na wapuuzi wengine ni nyepesi sana kwani wao ni vibaraka waliokubali kutumiwa kwa maslahi ya wanaowatuma.

Mkuu Magufuli ni rais mzalendo sana na sisi tunaojua kusudio lake tutamlinda kimwili na kiroho.
 
Wazalendo uchwara co?wa kusifu na.kuabudu
Mkuu mleta mada, humu jukwaani kuna Mawakala wa Wazungu wao kazi yao ni kuwatisha Watanzania.

Ni marafiki wa yule kaka wa MIGA, wameshindwa kabisa kuelewa kuwa awamu hii ni ya kizalendo na isiyokuwa na uoga wa kuyatetea maslahi mapana ya nchi.
 
Hakuna misingi imara wala matofali imara,ujinga wa wengi na unafki wa hawa wanaoitwa wasomi uchwara ambao kwao matumbo yamewekwa mbele kuliko chochote
Kenya kulikuwa na vita ya dhahiri ya kiukabila na walikufa watu zaidi ya elfu moja.

Lini Tanzania imetokea vita ya uchaguzi mpaka wakafa watu elfu moja, hatuna siasa za kiukabila wala za kimajimbo kama Ethiopia ya sasa.

Wapo mawakala wa wazungu wanajaribu kuivuruga hii nchi lakini hawataweza kwani ina misingi imara sana.
 
Back
Top Bottom