Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,270
Miaka karibia 60 baada ya uhuru 50% ya raia hawana uhakika wa huduma za jamii. Kuna vijiji huko unasafiri siku mbili kabla hujafika kituo chako cha karibu cha polisi. Mtu akifariki kama ni kifo chenye mashaka inabidi maiti ikae siku mbili ndani kabla polisi hajafika.
Elimu, Afya, Maji hali ya huduma ni hivyo hivyo. Huduma za jamii zimekua mtaji wa siasa. Wananchi wanaahidiwa, serikalili inaingia madarakani na baada ya miaka mitano mnaomba mambo yale yale.
Katika harakati za siasa, TANU ilipaswa kuhimiza watu wapate elimu. Wengi wangeelimika wangesukuma maendeleo. Kukosa elimu watu wanafikiri wanapata huduma za jamii kwa hisani ya serikali. Hawafikirii kuwa Hii ni kodi wanayolipa na huduma ni jukumu la serikali si hisani.