Afikishwa Mahakamani Kwa Kusambaza Picha za Mwanamke Akizaa

Huyu mama lengo lake lilikuwa kuonyesha athari za mgomo na siyo kumdhalilisha mama aliyekuwa akijifungua. Sasa nashangaa Rais kuamuru akamatwe. Wanahabari wa Tanzania igeni mfano huo wa kuanika mabovu bila kujali. Wadau mnasemaje kuhusu kushtakiwa kwa huyu mhariri? Is there any case to answer?
 
Rais wa Zambia, Rupiah Banda alikasirishwa na picha hizo na wakati akiongea na waandishi wa habari mwezi uliopita aliamuru mtu aliyezisambaza picha hizo akamatwe.

".

Ni ulevi wa madaraka wa huyu Rais!

Shida kuu ya viongozi wa kiafrika ni kwamba wanaongozwa na matukio!
Aligundua kwamba picha hiyo itamharibia image yake usoni pa jamii na hivyo akatumia rungu!

Lakini ujumbe umefika, sio Zambia tu, bali hadi huku Danganyika!
 
huyu kudhitskiwa itakuwa nzuri sana, kwani inategemeana picha hizo alizipiga kwa mwelekeo hani. kama alionyesha uke, ambazo nafikiri zipo hivyo, ndo maana wanaziita picha za ngono, maana yake alionyesha uke wa mama mzazi ambayo ni kitendo cha kinyama, bila kujari justification ya sababu yake- na naamini hakumwomba mama wala hakumwambia madhara yule mama ya picha zake akiwa mtupu kusambazwa miongoni mwa watu-fikiria angekuwa mkeo kaanikwa uchi, na mama yako kaachwa uchi ungefanya nini. huyu aadhibiwe kwa adhabu kali itakayostahili, ikiwezekana naye apigwe picha akiwa uchi, akiwa anakunya tu, halafu zisambazwe. mjinga kabisa huyu.
 
Angeweza kufikisha ujumbe wake kwa namna nyingine bila ya kutumia picha hizo. Hizo picha angeziweka kama exhibit pindi wakubwa wangetaka ushahidi. Moreover, there was no need sending a letter to VP while there are a lot of institutions under him that deals with day 2 day fracases.
But, she has no case to answer.
 
Angeweza kufikisha ujumbe wake kwa namna nyingine bila ya kutumia picha hizo. Hizo picha angeziweka kama exhibit pindi wakubwa wangetaka ushahidi. Moreover, there was no need sending a letter to VP while there are a lot of institutions under him that deals with day 2 day fracases.
But, she has no case to answer.

"A picture is worth a thousand words", wise men assert
 
Waliomdhalilisha zaidi ni wale walioshindwa kumsaidia wakati akihitaji msaada. Maana mpaka muda wa kumpiga picha ukapatikana inaonesha ni jinsi gani huyu mama alipata shida.
 
Kwani kujifungulia nje mahali wazi hadi akapigwa picha si kudhalilika?
Watu wangapi walimuangalia akiwa uchi?
Na wewe fikiri kama ni mkeo angefikia hali ya kuzalia mahali pa wazi namna hiyo ungejiona ni sawa?
Shida ni huduma duni za serikali kwa watu wake.
 
Nilitokea kuwa Zambia kipindi hili linatokea. Kwanza aliyepiga picha ni mume wa huyo mwanamke..ambae alimpeleka mkewe hospitali kwa sababu siku ya uzazi ilikuwa imefikia. Mumewe ndiyo alimpatia huyo mwandishi wa habari wa kike hizo picha..ili zipelekwa zinakostahili.
Na hasira au uchungu wa mume uliopelekea kumpa mwandishi picha hizo, ni kwa sababu, matokeo yake mtoto aliyezaliwa alikufa muda mfupi baada ya mkewe kujifungua.

Sababu kubwa ilikuwa ni mgomo wa wahudumu, ambapo serikali ilikataaa kuwasikiliza...na funny enough RAIS wa nchi akadai wahudumu wote waliogoma wasilipwe mshahara katika siku walizogoma....


Kama kuna kipindi Zambia wanalalamika na Rais aliye madarakani..ni kipindi hichi. Wamegundua wamefanya makosa big time..

Wenzetu Rais na serikali ikichemsha hawachelewi kuchagua upinzani kwenye uchaguzi ujao. Hivi hapa uchaguzi ujao chama cha upinzani kilichomwangusha Kaunda nacho kinatoka..yaani alama zote zinaonekana..

Sisi Tanzania...sijui tunataka tuingie kwenye guiness book of records...kwa utawala wa chama kimoja kwa nusu karne...!!!
 
Huyo mwanadada nampongeza kwa kufanya kile kinachotakiwa kufanywa ili kuiarifu na kuihamasisha jamii kuchachamaa haki zao zinapopondwa na waliwaweka madarakani

Mliaji
 
pia kosa la kumpiga mtu anaezaa picha halitoshi mtu kutiwa hatiani, hallipo ktk sheria za Zambia kama ni picha za ngono.So mama anfuatwa kisiasa kwani kauchokoa ufalme wa Rupiah Banda, ujue mapresident waswahili lao moja tuu, badala ya kupambana na matatizo eti anapambana na mtu alieonyesha jamani hapa kuna problem!! paangaliwe zaidi! yani duh!!
 
Hapa tanzania tunahitaji watu mahiri kama huyo mwandishi hapo juu,watu hufikiri njia rahisi ya kutatua matatizo ni kuyakwepa wakati njia ni kupambana nayo,hapo mzee banda kachemsha
 
Back
Top Bottom