Baltazari afikishwa hospitali ya Bugando kwa matibabu

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124
Baltazari Thobias ( 18) kutoka kijiji cha mtoni wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza afikishwa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya uvimbe ambao amekua nao kwa muda wa miaka minne sasa.

Akiongea baada ya kumpokea, Daktari Bingwa wa magonjwa ya uso, shingo, taya, kinywa na meno ( Maxillofacial surgeon ) Dkt. Emmanuel Motega amesema “tayari tumempokea Baltazari na tumeeanza kumfanyia vipimo vya awali ikiwemo vipimo vya damu pamoja na
CT - scan, vile vile tumechukua kipimo cha kinyama ( biopsy) kwa ajili ya uchunguzi zaidi, pia kijana huyu ataonwa na jopo la madaktari bingwa kutoka idara tofauti tofauti” amesema Dkt. Motega

Kuletwa kwa kijana huyu Bugando, kunafuatia maelekezo ya serikali kupitia wizara ya afya chini ya Mhe. Ummy Mwalimu baada ya Baltazari kuomba msaada wa matibabu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Rais @samia_suluhu_hassan
 
Back
Top Bottom