Mchungaji Nurdin Abdallah jela miaka 30 kwa kumbaka mwanaye

Dexta

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
1,756
4,144
Mchungaji Nurdin Abdallah ambae ni muinjilisti wa vitabu amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka kwa nyakati tofauti binti yake mwenye umri wa miaka 6.

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi mwandamizi Erick Kimaro wa mahakama ya wilaya ya Magu amesema mahakama hiyo imejiridhisha pasipo kuwa na shaka kwamba mshtakiwa huyo ametenda kosa hilo.

Ushahidi huo umethibitishwa kupitia mashahidi ambao ni mtoto aliyekuwa anabakwa pamoja na Ushahidi wa daktari aliyeithibitishia mahakama hiyo kuwa ni kweli sehemu za siri za binti huyo zilikuwa zinaonesha ameingiliwa.
Screenshot_20230421-201121_Facebook.jpg

Zaidi, soma: Mchungaji Nurdin Abdallah afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mwanaye wa miaka 6
 
Mchungaji Nurdin Abdallah ambae ni muinjilisti wa vitabu amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka kwa nyakati tofauti binti yake mwenye umri wa miaka 6.

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi mwandamizi Erick Kimaro wa mahakama ya wilaya ya Magu amesema mahakama hiyo imejiridhisha pasipo kuwa na shaka kwamba mshtakiwa huyo ametenda kosa hilo.

Ushahidi huo umethibitishwa kupitia mashahidi ambao ni mtoto aliyekuwa anabakwa pamoja na Ushahidi wa daktari aliyeithibitishia mahakama hiyo kuwa ni kweli sehemu za siri za binti huyo zilikuwa zinaonesha ameingiliwa.
View attachment 2595415
Nurdin Abdallah anakuwaje mchungaji?
 
Lazima itakuwa ni maagizo toka kwa mganga ili apate mvuto wa kuwa na waumini wengi apate sadaka.

Upuuzi kama huu ndio unafanya hata wahubiri wa kweli wa dini waonekane makanjanja.
 
Ila wanaume!!
Si mnasemaga zipo mpaka za buku3, sasa huyo mjomba Abdallah ilikuwaje?

Mnatutisha wakuu, tutaogopa kuwaacha nyumbani na watoto.

Zipo sema mpka ujue chimbo

Halafu huyu bwana ni mchungaji yawezekana ni maagano ya kishetan ayo
 
Back
Top Bottom