Afikishwa Mahakamani Kwa Kusambaza Picha za Mwanamke Akizaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afikishwa Mahakamani Kwa Kusambaza Picha za Mwanamke Akizaa

Discussion in 'International Forum' started by Bikra, Aug 6, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Chansa Kabwela, mmoja wa wahariri wanawake maarufu wa nchini Zambia, alimpiga picha mwanamama aliyekuwa akijifungua mbele ya hospitali bila ya msaada wowote ili kuwaonyesha watu jinsi huduma za afya zilivyozorota nchini humo.

  Baada ya kupiga picha hizo, Chansa aliwatumia picha hizo wanasiasa na wanaharakati wa kupigania haki za wanawake ndipo alipokamatwa na kupandishwa kizimbani akituhumiwa kusambaza picha za ngono.

  Akitoa ushahidi mahakamani, Kenneth Ngosa, sekretari binafsi wa makamu wa rais wa Zambia, George Kunda, alisema kuwa Chansa alimtumia barua akilalamikia mgomo wa madaktari uliosababisha mwanamke ajifungue mbele ya hospitali bila msaada.

  "Katika barua hiyo, kulikuwa na picha tatu za mwanamke akizaa. Nilisita kumpa makamu wa rais picha hizo kwakuwa yeye ni bosi wangu lakini kwakuwa alinisisitiza nimpe, nilimkabidhi makamu wa rais barua ikiwa na picha hizo" alisema Ngosa.

  "Makamu wa rais alishtushwa na picha hizo na kusema kuwa hajawahi kuona picha kama hizo maishani mwake" Ngosa aliiambia mahakama.

  Chansa ambaye ni mhariri wa gazeti la Independent Post, alikamatwa mwezi uliopita baada ya kuzituma picha hizo ofisi ya makamu wa rais na kwa viongozi wa vikundi vya kutetea haki za wanawake .

  Rais wa Zambia, Rupiah Banda alikasirishwa na picha hizo na wakati akiongea na waandishi wa habari mwezi uliopita aliamuru mtu aliyezisambaza picha hizo akamatwe.

  Wanachama wa chama cha upinzani cha Patriotic Front waliujaza ukumbi wa mahakama wakati wa kesi hiyo wakati watu wanaomuunga mkono Chansa walikuwa wakiandamana nje ya mahakama wakiwa na mabango yanayosema "Chansa umeonyesha kuwa wewe ni shujaa" na mabango mengine yanayosema "Rupiah acha kutuangusha".
   
 2. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyu mama lengo lake lilikuwa kuonyesha athari za mgomo na siyo kumdhalilisha mama aliyekuwa akijifungua. Sasa nashangaa Rais kuamuru akamatwe. Wanahabari wa Tanzania igeni mfano huo wa kuanika mabovu bila kujali. Wadau mnasemaje kuhusu kushtakiwa kwa huyu mhariri? Is there any case to answer?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ni ulevi wa madaraka wa huyu Rais!

  Shida kuu ya viongozi wa kiafrika ni kwamba wanaongozwa na matukio!
  Aligundua kwamba picha hiyo itamharibia image yake usoni pa jamii na hivyo akatumia rungu!

  Lakini ujumbe umefika, sio Zambia tu, bali hadi huku Danganyika!
   
 4. L

  Lukundo Member

  #4
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu kudhitskiwa itakuwa nzuri sana, kwani inategemeana picha hizo alizipiga kwa mwelekeo hani. kama alionyesha uke, ambazo nafikiri zipo hivyo, ndo maana wanaziita picha za ngono, maana yake alionyesha uke wa mama mzazi ambayo ni kitendo cha kinyama, bila kujari justification ya sababu yake- na naamini hakumwomba mama wala hakumwambia madhara yule mama ya picha zake akiwa mtupu kusambazwa miongoni mwa watu-fikiria angekuwa mkeo kaanikwa uchi, na mama yako kaachwa uchi ungefanya nini. huyu aadhibiwe kwa adhabu kali itakayostahili, ikiwezekana naye apigwe picha akiwa uchi, akiwa anakunya tu, halafu zisambazwe. mjinga kabisa huyu.
   
 5. J

  Jafar JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Angeweza kufikisha ujumbe wake kwa namna nyingine bila ya kutumia picha hizo. Hizo picha angeziweka kama exhibit pindi wakubwa wangetaka ushahidi. Moreover, there was no need sending a letter to VP while there are a lot of institutions under him that deals with day 2 day fracases.
  But, she has no case to answer.
   
 6. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Corruption, corruption, corruption.
   
 7. P

  Prince Member

  #7
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "A picture is worth a thousand words", wise men assert
   
 8. S

  Sumji R I P

  #8
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waliomdhalilisha zaidi ni wale walioshindwa kumsaidia wakati akihitaji msaada. Maana mpaka muda wa kumpiga picha ukapatikana inaonesha ni jinsi gani huyu mama alipata shida.
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kwani kujifungulia nje mahali wazi hadi akapigwa picha si kudhalilika?
  Watu wangapi walimuangalia akiwa uchi?
  Na wewe fikiri kama ni mkeo angefikia hali ya kuzalia mahali pa wazi namna hiyo ungejiona ni sawa?
  Shida ni huduma duni za serikali kwa watu wake.
   
 10. M

  MissKitim Member

  #10
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilitokea kuwa Zambia kipindi hili linatokea. Kwanza aliyepiga picha ni mume wa huyo mwanamke..ambae alimpeleka mkewe hospitali kwa sababu siku ya uzazi ilikuwa imefikia. Mumewe ndiyo alimpatia huyo mwandishi wa habari wa kike hizo picha..ili zipelekwa zinakostahili.
  Na hasira au uchungu wa mume uliopelekea kumpa mwandishi picha hizo, ni kwa sababu, matokeo yake mtoto aliyezaliwa alikufa muda mfupi baada ya mkewe kujifungua.

  Sababu kubwa ilikuwa ni mgomo wa wahudumu, ambapo serikali ilikataaa kuwasikiliza...na funny enough RAIS wa nchi akadai wahudumu wote waliogoma wasilipwe mshahara katika siku walizogoma....


  Kama kuna kipindi Zambia wanalalamika na Rais aliye madarakani..ni kipindi hichi. Wamegundua wamefanya makosa big time..

  Wenzetu Rais na serikali ikichemsha hawachelewi kuchagua upinzani kwenye uchaguzi ujao. Hivi hapa uchaguzi ujao chama cha upinzani kilichomwangusha Kaunda nacho kinatoka..yaani alama zote zinaonekana..

  Sisi Tanzania...sijui tunataka tuingie kwenye guiness book of records...kwa utawala wa chama kimoja kwa nusu karne...!!!
   
 11. M

  Mliaji New Member

  #11
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo mwanadada nampongeza kwa kufanya kile kinachotakiwa kufanywa ili kuiarifu na kuihamasisha jamii kuchachamaa haki zao zinapopondwa na waliwaweka madarakani

  Mliaji
   
 12. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  pia kosa la kumpiga mtu anaezaa picha halitoshi mtu kutiwa hatiani, hallipo ktk sheria za Zambia kama ni picha za ngono.So mama anfuatwa kisiasa kwani kauchokoa ufalme wa Rupiah Banda, ujue mapresident waswahili lao moja tuu, badala ya kupambana na matatizo eti anapambana na mtu alieonyesha jamani hapa kuna problem!! paangaliwe zaidi! yani duh!!
   
 13. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Picha wapi sasa?
   
 14. R

  Ronaldinho Member

  #14
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa tanzania tunahitaji watu mahiri kama huyo mwandishi hapo juu,watu hufikiri njia rahisi ya kutatua matatizo ni kuyakwepa wakati njia ni kupambana nayo,hapo mzee banda kachemsha
   
Loading...