Afia lodge kwa sababu ya kuzidisha Viagra

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Polisi katika Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya wanachunguza kifo cha Mwanaume mwenye umri wa miaka 55 ambaye amefia lodge wakati akifanya mapenzi huku chanzo kikidaiwa kuwa ni kuzidisha kiwango cha dawa za kuongeza nguvu za kiume (viagra) ili aweze kumridhisha kingono Msichana wa miaka 25 ambaye alikuwa nae lodge.

Mwanaume huyo ambaye jina lake limefichwa na Polisi anadaiwa kuanguka ghafla akiwa katikati ya tendo na baadaye kufariki akiwa kwenye Lodge hiyo iliyopo eneo la Ndhiwa.

"Mwanaume huyo alichukua chumba kisha dakika chache baadaye akaja Msichana wa miaka 25 wakajumuika nae chumbani wakiendelea kujivinjari ghafla majanga hayo yakatokea na Msichana akatoa taarifa kwa Uongozi wa Lodge hiyo kuwa Mzee amezidiwa".

"Msichana amekiri mbele ya Polisi kwamba alikuwa anafanya mapenzi na Mzee huyo na kwamba anahisi alitumia viagra ili kuongeza nguvu za kiume na huenda ndizo zimemletea matatizo, Msichana huyo anashikiliwa Polisi kwa uchunguzi zaidi".
 
SIjawahi kutumia hivyo vidonge, najiamini kwenye kucheza mechi yangu kama ilivyo, iwe hafifu au vinginevyo tunakwenda tu hivyo hivyo, siongezi minguvu wala nini, kama demu ukichukia uwezo wangu basi pole kwako hehehe.
Sema wanaume kuna mbinu nyingi za kuongeza nguvu na uwezo bila kutumia vidonge......
 
Jamani .... Hivi kama Una njaa hiyo tendo la ndoa/ngono unawezaje?

Wakenya tafuteni msosi mtakufa kwenye kipochi manyoya


Unanjaa halafu una hisia eti? Nonsense
 
Back
Top Bottom