Mara ya kwanza kumjua mtu aliyejiua kwa sababu ya Mapenzi

willpower

JF-Expert Member
Dec 3, 2019
404
2,271
Hii tukio nimelikumbuka baada ya kutumiwa picha yangu ya zamani na mmoja wa watu tuliokuwa tukiishi mtaa mmoja.

Nakumbuka nikiwa kidato cha tatu; asubuhi moja ya Februari 14, majira ya saa nne asubuhi, kilio kilisikika kutoka katika nyumba moja.
Ilikuwa sauti ya kilio kikubwa kutoka kwa mama mmoja; nikiwa ndio kwanza natafakari ni kilio cha nini; mama yangu aliingia kwa kasi na kusema ''mtoto wa mama T amejinyonga''

Mama T alikuwa na watoto wawili, huyo T ambaye alikuwa kijana wa chuo mwaka wa kwanza na dada yake ambaye tulikuwa naye kidato kimoja.
Kama ilivyo kawaida nikiwa nimejawa na wasiwasi na simamzi nikaona ngoja na mimi nikashuhudie japo kwa mbali.
Wakati nafika mbele ya nyumba ya mama T ndio nakuta Defender ya Polisi (miaka ile zilikuwa zote Land Rover za Rangi nyeupe) ilikuwa imefika na polisi kadhaa walishafika ndani ya nyumba.

Huku kukiwa na vilio; polisi wakiwa na mjumbe wakatoka wakiwa wamebeba mwili wa kijana T ambaye kwa sisi wanafunzi wa sekondari tulimuona kama mfano na roll model wetu kwenye njanja ya elimu.

Swali likawa kwa nini amejinyonga? Hii ni miaka ambayo watu wengi hapa Dar walikuwa wakijiua kwa kumeza Vidonge vingi vya Chloroquine (Klolokwini).

Tukiwa bado tunatafakari mjumbe akawa ameongozana na polisi mmoja wapo huku akiwa ameshika karatasi; kuelekea ndani ilimokuwamo familia ya T; ikaja kujulikana baadaye kuwa T alijiua kwa sababu ya mapenzi; msichana aliyekuwa naye kwenye mahusiano alimwambia kuwa waachane maana yeye amepata mtu mwingine.
Hivyo jamii ikajua kuwa T amejiua kwa sababu ya mapenzi, aliachwa na akaona hawezi kuishi bila huyo dada.

Kwa wakati ule; nikiwa na miaka 16 nilishindwa hata kuelewa maamuzi ya T, leo bado nashindwa kujua kwa nini T alichukua maamuzi yale. Ukweli ni kwamba T hakuwa mtu wa mwisho kujiua kwa sababu ya mapenzi; nimeendelea kusikia visa vingine vingi vya watu kujitoa uhai na madhira mengine ya mapenzi.

Mama T bado yupo hai, na yumkini dada aliyeachana na T naye yupo hai; nilipata nafasi ya kuonana na mama T miaka kadhaa iliyopita, bado kifo cha mtoto wake kinaendelea kumuumiza; nakumbuka nikiwa namsalimia pamoja na mke na watoto wangu , mama T alisema ''unajua kaka yako T sasa hivi angekuwa na watoto wakubwa sana''. Hii ilinihuzunisha sana.

Wadogo zangu hakuna justification ya kujitoa uhai; mpenzi wako uliyejitoa uhai kwa ajili yake atasahu na maisha yake yateendelea; ila familia yako haitasahau; utawaacha katika majonzi na huzuni mpaka siku wanakufa.

Kaka T aliamua alichaoamua; sipo hapa kumhukumu lakini alituachia funzo; sio kwamba tuache kupenda ila kupenda na mapenzi sio sababu ya kujitoa uhai.

Nakukumbuka baba yangu alikuwa anatuambia mimi na kaka yangu; mapenzi ni sehemu ya maisha lakini sio maisha yote.

Usifanye sehemu ya maisha kuwa ndio maisha yote. Hii ilitusaidia sana mimi na kaka yangu maana tuliona hatari ya kufanya mapenzi kuwa ndio maisha.

Walisema watu wa magharibi; Nothing Last Forever...Hakuna kinachodumu milele.

Niwatakie siku njema.
 
Kuna watu wana roho za ajabu sana. Siwezi kuacha vizuri vya dunia hii kwa sababu ya mbususu mm. Mambususu yamejaa kila kona, halafu nife kwa sababu ya kimbususu cha mtu. AAHAAPANAA
 
Mimi mara ya kwanza kuona mtu amejiua kisa mapenzi ni 2014,TUMAINI MKMR UNVRSTY...
Tuliamka asubuhi tukamkuta mwamba amejining'iniza kwenye parking ya magari halafu mikono ipo mfukoni...

walipomtoa mikono ndio ikaonekana barua aliyoandika na akamtaja mpaka demu wake,roho iliniuma sana..
tulisafirisha maiti mpaka kwao songea tulipofika baba akamtandika viboko mwanae(marehemu),ilisikitisha sana..

halafu home kwao maisha magumu sana halafu jamaa badala ya kusoma ili akapunguze ujinga home yeye akajiua...
yani nilitoa machozi aisee doh.
 
Daaah aisee roho ya mauti ni Mbaya Sana yaani kutokupendwa na mtu mmoja ndyo kumfanye mtu ajiue inasikitisha Sana alafu huyo Dem sasahivi kashasahau anakula raha tu.

Watu msipende msipopendwa .Ukiona hupendwi explore more and more women . Wanawake ni wengi hawafanani hawawezi kukataa wote.
 
Kufanya vitu vya uwekezaji kwenye mapenzi kumeua watu wengi sana na sio sababu kuachwa sababu za kujiua huwa ni vitu alivyomfanyia yule mpenzi aliemuacha na anaona kuvipata tena ni ngumu kwenye maisha yake
 
Nimechukua huu msemo wa Baba for further reference;
Nakukumbuka baba yangu alikuwa anatuambia mimi na kaka yangu; mapenzi ni sehemu ya maisha lakini sio maisha yote.

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Mtu kujiua ni roho, ambazo zina history kwenye hizo familia. Ukichunguza utagundua Kuna wengine nyuma yake walijiua hivyo hivyo. Vijana wanatakiwa kumuweka Mungu mbele kwanza Ili wawe na hofu pia Mungu ataziondoa hizo roho watakuwa huru. Binafsi nilikuwa na roho ya ukatili na hasira kubwa nilivyokuwa Kijana. Mtu akinikonikorosha nafunga Mtaa mzima Kwa Kurusha mawe. Namshuku Mungu kanitengeneza baada ya kugundua hizo hasira zilikuwa roho za Kifamilia.
 
Mimi mara ya kwanza kuona mtu amejiua kisa mapenzi ni 2014,TUMAINI MKMR UNVRSTY...
Tuliamka asubuhi tukamkuta mwamba amejining'iniza kwenye parking ya magari halafu mikono ipo mfukoni...

walipomtoa mikono ndio ikaonekana barua aliyoandika na akamtaja mpaka demu wake,roho iliniuma sana..
tulisafirisha maiti mpaka kwao songea tulipofika baba akamtandika viboko mwanae(marehemu),ilisikitisha sana..

halafu home kwao maisha magumu sana halafu jamaa badala ya kusoma ili akapunguze ujinga home yeye akajiua...
yani nilitoa machozi aisee doh.
🥲
 
H

Huyo mzee alivyomtandika alifanya Jambo jema Sana.
 
Back
Top Bottom