Afariki kwa ajali ya 'ungo' jioni hii

Afariki kwa ajali ya 'ungo' jioni hii

Junapili jamani nimeshasema tunamwaga maombi nchi nzima kwa hio wachawi tulizaneni majumbani mwenu mtakufaa
 
Acha ubishi uchawi upo,......kuna jamaa walipaa na ungo pale mawasiliano ubungo mchana kweupe na watu kushuhudia..ili wawaonyeshe ambao hawaamini......NATAMANI UNGEKUWEPO SIKU HIYO HALAFU UONE.....Hata biblia na misahafu vinasema uchawi upo.
nitumie video yake
 
Hahahaaaaa!!! Akusoma hilo bango ktk iyo nyumba pemben y gari. R.I.P babu mchawi
 
Kama hamna kitu kama hicho, hebu elezea kilichotokea, maana unapobisha bisha kwa hoja, pichani unaona gari ya polisi, kuonyesha kuwa hakufariki katika mazingira ya kawaida. Yote kwa yote huo ungo pia unaonekana hapo pichani, ingingekua huo ungo hausiani na kifo chake polisi wasingeubeba. Tena kwa kuogopa wamemuwekea mwenyewe. Ila uchawi ni umaskini ungo umechoka kiasi hicho kwanini usimwangushe, ungo unaupata kwa buku mbili tu, ameshindwa kununua mpya.
 
Sijui kunafaida gani mtu kakonda kama hivyo alafu unauendekeza uchawi bora kama mtu unakua na hadhi kuliko mateso hayo
 
Unaweza kujuta mzee wa watu 'kalewa' kutokana na 'herbs' alizokunywa/nusa wakati wa kutambika, kisha kupoteza fahamu na kuanguka (trip not fall), wabongo wanadai kadondoka kutoka angani. Kuna aliyemuona?

Kiranga vipi hii?
 
Alikatiza kwenye anga ambayo sio yake, ametunguliwa
 
Uchawi upo wa aina Nyingi duniani, inategemea unatumia uchawi wa gani? Na kwa manufaa ipi?
 
Huyo mze alokosea kitu kimoja hapa....hii ndege yake (ungo) ilipasuka (kutoboka toboka) na kufanya upepo kupita kwenye injini na kuizidi kasi ndipo injini ikabuma. Mbona anaonekana kama mshana jr au Mpare fulani hivi.
 
Wakimsachi wanaweza mkuta n'a kadi ya uanachama wa team l....mumbas

OVA
 
Makanisa Mengi sana huku Kijichi atakua kavutwa tu Huyo,rada yake ilisoma vibaya tangu anaondoka pale Sumbawanga maana ukungu ulikua mwingi sana time ana take off
 
Hii kitu ya ungo ni imagination haiwezekani hata kidogo eti mtu apande kwenye ungo.

1. Serikari ifanye uchunguzi wa kina yawezekana watu wamefanya mauaji halafu waka plot scene ili kufunika uovu wao

2. Kwa kuwa jamii ilishalishwa dhana ya uongo ya watu kusafiri na ungo wamekuwa obsessed na illusion hiyo na hivyo kufunika hata uwezo wao wa kufikiri nje ya box na kubakia wakiamini kile wanachokiona na macho ya kawaida.

3. Ni mara nyingi watu wameshambuliwa na wengine hata kuuawa kwa imani za kijinga kama hizo pale ambapo waganga matapeli wa kienyeji wanapo kula deal na mtu kwa kumpaka mazizi na kumbebesha ungo na kujifanya eti amemtungua kwa nguvu zake ili apate wateja.

Hivyo , mtu huyo achunguzwe ni wawapi, ndugu zake, mara ya mwisho alionekana na nani au aliwasiliana na nani au alikuwa na uadui na nani.
Perfectly said mkuu! Wangefanya postmortem investigation immediately wangegundua aliuwawa ama kwa kunyongwa au kwa njia nyingine! Sijui kwa nini watanzana tumetekwa nyara hivyo na dhana nyepesi na potofu hivyo kwamba hatuwezi ku - reason things out! This is just too low for us to believe cheeply karne hii! Good grief! Pumzika kwa amani wewe uliyeuwawa kwa sababu tusizozijua na sasa WAPUMBAVU wanaaminishwa eti ulipata ajali ya ungo!
 
Back
Top Bottom