Afariki baada ya kukabwa na nyama akiwa msibani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afariki baada ya kukabwa na nyama akiwa msibani

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by fabinyo, Feb 2, 2012.

 1. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Thursday, 02 February 2012 07:47

  Joseph Lyimo,Babati
  MKAZI kijiji cha Gehandu,Wilayani ya Mbulu Mkoani Manyara, Gainame Mori (61) amefariki dunia baada ya kukabwa na finyango ya nyama wakati akila chakula kwenye mazishi ya jirani yaliyofanyika kata ya Magara wilayani Babati.
  Hali hiyo ilisababisha watu waliofika msibani hapo kushikwa na mshtuko akiwemo Mamo Magi (30) kupoteza fahamu na kusababisha baadhi ya waombolezaji kukimbia mbali na eneo hilo kwa kuogopa kufanywa mashahidi.

  Tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni katika kijiji cha Mayoka A wilayani Babati ambapo mzee huyo alifariki dunia papo hapo kwa kile kinachodaiwa kukosa hewa baada ya kunyongwa na finyango ya nyama wakati akila pilau.
  Wakizungumza na Mwananchi baada ya kutokea kwa tukio hilo, baadhi ya mashuhuda walidai kuwa mzee huyo alifika kwenye msiba huo kwenye kijiji cha Mayoka A, kata ya Magara akiwa mzima wa afya.

  Walisema mzee huyo akiwa ni miongoni mwa watu waliokuwa kwenye shughuli hiyo na akawa anapata chakula katika sinia pamoja na wazee wenzake huku wakisubiri taratibu za mazishi hayo.

  “Ghafla wakati anaendelea kula chakula mzee huyo akawa anatoa macho na machozi na watu waliokuwa jirani yake wakadhani mzee Mori anamsikitikia na kumlilia marehemu huyo,” alisema mmoja kati ya shuhuda wa tukio hilo.

  Walisema baadhi ya watu walitambua mzee huyo amekwamwa na nyama wakawa wanampiga ngumi mgongoni lakini nyama hiyo haikutoka ndipo mmoja kati yao akaitoa kwa kuingiza mkono wake kwenye kinywa cha mzee huyo.

  Hata hivyo,walisema mzee huyo alifariki dunia papo hapo kwa kile kinachodaiwa kukosa hewa baada ya kunyongwa na nyama hiyo,ndipo wakatoa taarifa kwenye ofisi ya kijiji hicho pamoja na polisi.

  Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya wilaya ya Mbulu kwa uchunguzi zaidi na Magi amelazwa kituo cha afya cha Magara ambapo hali yake inasemekana inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.
  -------------------------------------------------*************************-----------------------------------------------------------
  Wakati nasoma nilikuwa na huzuni sana lakini nilipofika hapo kwenye red,nikacheka sana halafu nikarejea tena kwenye huzuni!mkono wa mtu au?poleni sana wana Mbulu
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Watakuwa walimfinyia punje huyo.
  Shughuli za wenyewe ni nowmer mazee...
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Mhm!! Mungu amlaze mahali pema peponi. Amen
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,504
  Likes Received: 19,920
  Trophy Points: 280
  so sad...wata watasema ni uchawi ..for me i see ni accident tu ya kawaida
   
 5. G

  Gervas deogratius Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Da! Da!...its so bad R.I.P..
   
 6. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  yah,so sad wadau!
   
 7. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Habari nyepes nyepesi!i
   
 8. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,538
  Likes Received: 12,802
  Trophy Points: 280
  Rip mzee!
   
 9. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Bwana ametoa na Bwana ametwaa....
   
Loading...