Aende wapi kati ya TARURA kwa Mkataba ama HALMASHAURI ila Perment!

Aende wapi kati ya TARURA kwa Mkataba ama HALMASHAURI ila Perment!

Aende wapi kati ya TARURA kwa Mkataba ama HALMASHAURI ila Permanent!


  • Total voters
    10
Halmashauri wapo kwa ajili ya umbea na wivu, kutwa wanasemana😄, ukiwahi kazini utawasikia wakongwe wanakunanga tu, ukiwa na juhudi ya kazi napo ni mipasho ya kukukatisha tamaa yaani. Bora aende MAKKA tu😀
Halmashauri kiukweli kuna uswahili mwingi na usiombe uwakute wale wazee hlmashuri wanaiona kama mali yao ....ndio maana ikaitwa local gvt
 
Nenda kwenye permanent ukiacha utakuja kujijutia mbele, ingia kwenye system then mengine yatajiseti
 
HALMASHAURI Kuna mishahara ya milioni, tupeni hiyo michongo
 
WanaJF! Kwema? Moja kwa moja niende kwenye Mada.

Mdogo wangu kapata kazi ya Uhandisi ya Mkataba TARURA ila pia kapata Kazi Permenent HALMASHAURI.

TARURA atapata kama 2M na marupurpu mengine kwa anabyodai Wakati Halmashauri ni 1M pia kwa ufatiliaji wake Halmashauri marupuru ni kwa manati.

Yuko njia panda, check number anaitaka ila pia anaogopa kujiingiza Halmashauri asije kupotea kule na ugumu wa Maisha pia.

Mkataba una faida ya kimaslahi kwa sasa ila anaogopa consequences zake kama kusitishiwa, kutopanda daraja na pia kuwa na zero chances ya kuwa kiongozi unless mkataba ufanywe permenent.

Na Je asiporipoti kuna consequences zipi za ki utumishi? Ataruhusiwa kuendelea kuomba na kupangwa wakati ujao?

Watalaam leteni mawazo yenu.
Aende tarura
 
Aende TARURA. Halmashauri kazi zipo tu, akizitaka atazikuta baadaye.

Lakini pia TARURA ni semi autonomy ila iko chini ya Halmashauri hizo hizo.
Hawezi pangiwa tena kazi huyo.

PSRS wakikupangia kazi usiporipoti sahau tena placement kutoka kwao ya kazi ya ngazi hiyo ya elimu.
 
Hii nilisikia sehemu fulani
Screenshot_20250514_212424_Chrome.jpg
 
Mshauri aende chap akaripoti Halmashauri. Kwa engineers Halmashauri ni kuzuri sana na isitoshe anakuwa na uhakika wa kuendelea na usajili kwa ngazi za bodi ya engineers.
Tarura ajira za muda hazina uhakika na hasa mwaka huu wa uchaguzi.
Baada ya miaka 3 akiwa kwenye ajira ya kudumu anaweza kuhamia taasisi nyingine au kuazimwa kwa muda huko huko TARURA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom