Kama kama ana vi elements vya ufisadi, na anapenda sana pesa za kifisadi, na anaota kuwa tajiri kupitia ufisadi basi aende halmashauri! Kama ni hizi halmashauri ndogo, baada ya miaka 3-5 anakuwa Mkuu wa Idara! Hapo ni mwendo wa 10% zinazotokana na miradi ya ujenzi! Kwa mwaka halmashauri ikifanya kazi za thamani ya 200M, hapo ana angalau 20M kwa mwaka! Kama halmashauri ni kubwa na miradi ni mingi, kukiwa na kazi za thamani ya 500M, 50M anazifisidi! Sie ambao kazi zetu zinaingiliana sana na halmashauri tunajua yanayoendelea kule! Avumae baharini ni papa lakini kule Halmashauri kuna wapigaji hata huko kwenye mawizara wanasubiri!!
Najua unajua ila nakujuza zaidi, nasikia Kamanda Mbowe nae alipewa chake na Dully wakati hapo kabla tuliambiwa Kamanda ni tajiri, hana njaa manake anamiliki hadi mtaa huko Dubei! Wala sijui nishike lipi na niache lipi! Au unataka nikukumbushe wale Makamanda waliokuwa wananunuliwa kama Machangudoa enzi za Mwamba JPM? Ni kwamba umesahau hata yule Padri ambae nae alikuwa kimya kabisa baada ya kulambishwa asali? Akaandika hadi kitabu cha kuiponda CHADEMA? Kakatiwa mrija wa asali eti nae hivi sasa anajifanya tena kuwa mpambanaji na Wajinga wanamuamini!! Hiyo ndo Bongo! Ukipinda kibyongo wenzako Wanabongoa! Hapa natafuta kazi serikalini manake hii kazi yangu ya kusafirisafiri kwenye barabara za vumbi imeshanichosha! Nikienda huko serikalini, labda niwekwe mbali na jungu lenye vinono vinginevyo ni mwendo wa kuiba tu! Nchi usimwamini hata mmoja manake yote ni majizi tu!