SOFTWARE Adiuta Biz Assistant - Programu ya Usimamizi wa Biashara zako

Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,291
2,000
Habari njema kwa wafanyabiashara mliokuwa mnapata changamoto juu ya namna bora ya kusimamia biashara zenu.
Adiuta Business Assistant ni Mfumo unaokusaidia kusimamia fedha za biashara yako kwa kukuwezesha kujua mapato, matumizi, mali na madeni ya biashara yako.

Iwe ni biashara ndogo ya kuuza vifaa, duka la dawa, au iwe kampuni ndogo, ya kati au kubwa, Adiuta inakuwezesha kupata picha halisi ya biashara yako na kukuwezesha kufanya maamuzi bora. Baadhi ya faida za kutumia Adiuta Business Assistant ni:
 1. Kupata picha ya Mapato, Matumizi na Madeni kwa kipindi chochote cha biashara yako. Hii inakuwezesha kujua wapi pa kupunguza matumizi na wapi pa kuongeza nguvu kwenye mapato na madeni unayodai na kudaiwa.
 2. Kwa biashara zinazojihusisha na uuzaji wa bidhaa, Adiuta inakupa ripoti ya kuonesha mauzo yako kwa bidhaa. Hapa inakupa picha ya bidhaa zinazotoka sana na zinazochelewa ili kukusaidia kuamua kwenye kuagiza mzigo wako.
 3. Rekodi miamala yako yote ya Benki kwa urahisi, na pata ripoti za mapato na matumizi kwa kila akaunti yako: Iwe ni MPesa, TigoPesa, AIRTEL Money, n.k na upate ripoti ya fedha iliyoingia na kutoka kwa kila akaunti
 4. Tumia kwenye Simu yako ya Kiganjani. Ukiwa na Adiuta unaweza kufanya mambo yote Muhimu kwenye simu yako ya mkononi.
 5. Kwa Makampuni unaweza kufanya mambo ya kihasibu kwa kutumia Adiuta, vitu kama Charting Accounts, Invoicing, Bills, Assets Register and Depreciation, na Manual Journals. Pia unapata standard reports kama Balance Sheet, Income Statement na nyingine nyingi.
Kwa Makampuni baadhi ya mambo Adiuta Business Assistant inakusaidia
 1. Kuweza kuwatumia Invoices wateja wako, ukiwa kwenye kompyuta ama simu. Hii inakusaidia kufanya kazi kwa uharaka na kuongeza ufanisi
 2. Kuandika Bills za kila matumizi hivyo kuweza kujua Matumizi yako na yanatumika zaidi wapi. Hii inakusaidia kujua matumizi ya kupunguza ili kuongeza faida.
 3. Kurekodi Miamala kwenye akaunti za kibenki (Benki, MPESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY et al) na kufanya reconcilliation ya statement ya benki dhidi ya System. Adiuta ina auto match algorithm inayokusaidia kutambua miamala toka kwenye Bank Statement hivyo kukurahisishia kazi ya kufanya "reconcilliations"
 4. Kujua madeni unayodai na unayodaiwa, yale ambayo yapo ndani ya muda na yale ambayo yamepita muda wake wa kulipwa
 5. Kuweza kuwa na rekodi ya mali zako, thamani zake na muda wa mwisho wa matumizi (Asset register and depreciation)
 6. Kupata report za kihasibu ambapo zitarahisisha kujua faida, hasara, mali, madeni na kurahishisha ukaguzi wa ndani na nje
Kwa nini utumie Adiuta Business Assistant? Hizi ni baadhi ya sababu za msingi
 • Kuepuka kuibiwa kwa kuwa Adiuta inafuatilia bidhaa tangu inapoagizwa (Purchase order) Inapopokelewa na inapouzwa.
 • Kujua Mahesabu ya biashara yako kwa ripoti zetu nyingi hivyo kufanya maamuzi ukiwa na taarifa.
 • Kuepuka kupoteza vitu kwa kuharibika (Expired Items). Adiuta ina namna inayokusaidia kuuza vitu kwa namna ambayo utauza kwanza vinavyokaribia kuisha muda wake kabla ya vile vinavyo haribika kipindi kirefu kijacho.
 • Kuendesha kampuni kisasa na kwa ubora. Huwezi kuongoza biashara karne ya 21 bila taarifa za kifedha za biashara yako.
 • Kuendesha biashara popote ulipo duniani. Ukiwa na Adiuta unaweza kufanya kazi popote ulipo. Upo ofisini? Unaweza kutumia Kompyuta yako. Uko kwenye gari, daladala, hotelini au mahali pengine na huna kompyuta? Unaweza kutumia simu yako. Adiuta itakuwezesha kufanya kazi popote pale!

Je Ninaipataje?
Ni rahisi sana. Wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo
Piga: 0673651520 au 0767893474
WhatsApp Tuchati: 0767893474
Instagram: adiuta_biz

Ninatumia programu nyingine, Ninawezaje kuhama?
Kama unatumia Programu nyingine na ungetaka kuhamia Adiuta, tutakusaidia namna bora ya kuhamia na kila inapowezekana, tutakusaidia kuhamisha data zako. Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.

Karibuni sana tuwahudumie kwa viwango na ubora uliotukuka. Mafanikio yako ni ya msingi sana!
 
Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,291
2,000
Unaweza kuwasiliana nasi kwa njia ya WhatsApp, Email au kwa ktupigia simu. Pia unaweza kutufuata Instagram kwa jina adiuta_biz.
Unaweza kuitumia kuendesha kampuni, Duka au Biashara ya aina yoyote ambayo inatoa huduma au inauza bidhaa.
Fungua akaunti yako uijaribu wenyewe. Bure kwa siku 30

Karibuni sana!
 
Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,488
2,000
Kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri na hatua mliyofikia.Functionalities nimeona ziko za kutosha na bado naona kama product iko room ya kuimprove hasa kwa kuwa ni local content basi ni fursa kwenu developers na kwa market kuikuza.Maswali yangu ni Je mko na self hosted option? Je iko katika lugha ya kiswahili na kiingereza?Je ni mdular product yaani mtu anaweza kuicoustomize kwa kuzingatia aina ya biashara/hudma yake?Je selling point ni idadi ya users au n functionality au ni vyote?Maana nammini kabisa kwamba hii kama business suite ni vyema mtu akapewa access ya all business functioanality na kisha selling point ikawa ni idadi ya users,self hosted au hosted,training and support,etc.

Maoni yangu ni kama mtu ambaye niko sokoni kama muuzaji wa aina mbalimbali za product na nimekuwa nikipata shida kupush local product sokoni kwa sababu ya hizo limitation hapo juu.

Vile vile kukiwa na module ya kuwezesha payment integration itasaidia sana kuhakikisha kwamba hata mobile payment,epayment zinakuwa supported.

Vile vile mnaweza kuongea na TRA kuwe na uwezekano wa integration ya Virtual efd ili mtu akinunua mfumo wenu asilazimike kuwa na EFD bali risit zake ziwe verified na TRA.Najua option hizi zote zinawezekana technologically na zina gharama ni ninaamini mnaweza kuziweka katika plan ya future edition.

As a courtesy nitawasilisha product yenu kwa baadhi ya potential clients na nitawapa mrejesho.

Otherwise nawatakia kila la heri.

Keep up the good work!!!

NB.Nitakutafuta PM tujadili namna tutafanya kazi pamoja.
 
Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,291
2,000
Kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri na hatua mliyofikia.Functionalities nimeona ziko za kutosha na bado naona kama product iko room ya kuimprove hasa kwa kuwa ni local content basi ni fursa kwenu developers na kwa market kuikuza.
Ahsante kwa complement. Ulichosema ni sahihi kabisa.

Maswali yangu ni Je mko na self hosted option?
Hapana. Ni Software as a Service. Kwa sasa hatufanyi self hosting na hakuna mpango huu in any foreseeable future

Je iko katika lugha ya kiswahili na kiingereza?
Kwa sasa Android App ina lugha zote mbili, kiswahili na Kiingereza. Kwa upande wa Web kuna Kiingereza na kiswahili bado kianendelea kufanyiwa kazi. Siku sio nyingi option ya kiswahili kwa ukamilifu wake itakuwa inapatikana.

Je ni mdular product yaani mtu anaweza kuicoustomize kwa kuzingatia aina ya biashara/hudma yake?Je selling point ni idadi ya users au n functionality au ni vyote?Maana nammini kabisa kwamba hii kama business suite ni vyema mtu akapewa access ya all business functioanality na kisha selling point ikawa ni idadi ya users,self hosted au hosted,training and support,etc.
Iko based na plan ambayo mteja atachagua. Kila Plan ina features zake as well as limit ya watumiaji. Tunaamini kabisa tumefanya segmentation ambayo itawasaidia Watumiaji kuchagua wanachokitaka. Kwa anayetaka full features kuna plan ya Pro.
Taarifa zote zipo kwenye website yetu iliyopo kwenye kipeperushi. Bahati mbaya JF kona hii hawaruhusu kuweka link!

Maoni yangu ni kama mtu ambaye niko sokoni kama muuzaji wa aina mbalimbali za product na nimekuwa nikipata shida kupush local product sokoni kwa sababu ya hizo limitation hapo juu.
Tumejaribu kufikiria kila namna, reasonable ya ku cover base kubwa zaidi. Tunaamini wengi wataweza kuchagua sehemu wanayoitaka.
Kama kuna mteja ambaye anadhani mahitaji yake hayako covered na hizi Plana anaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizo hapo kwenye kipeperushi. Tunaweza endelea naye na kumsikiliza tokea hapo!

Vile vile kukiwa na module ya kuwezesha payment integration itasaidia sana kuhakikisha kwamba hata mobile payment,epayment zinakuwa supported.
Sijaelewa una maana gani maana hii ni pana kidogo. Kama unamaanisha kuweza kulipa moja kwa moja kwenye simu yako ukiwa kama mteja wetu, hizi options ziko underway. Tutakuwa tunatoa update hapa na kwenye Insta account yetu adiuta_biz

Vile vile mnaweza kuongea na TRA kuwe na uwezekano wa integration ya Virtual efd ili mtu akinunua mfumo wenu asilazimike kuwa na EFD bali risit zake ziwe verified na TRA.Najua option hizi zote zinawezekana technologically na zina gharama ni ninaamini mnaweza kuziweka katika plan ya future edition.
Kuna mengi yanaendelea chini ya kapeti, ila itoshe kusema tu mapinduzi makubwa ya uendeshaji wa biashara yameanza na mambo mazuri mengi yanakuja!

As a courtesy nitawasilisha product yenu kwa baadhi ya potential clients na nitawapa mrejesho.
Ahsante sana kwa zawadi hii.
Kwa niaba ya Kampuni, tunashukuru!

Otherwise nawatakia kila la heri.

Keep up the good work!!!

NB.Nitakutafuta PM tujadili namna tutafanya kazi pamoja.
Karibu sana!
 
Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,488
2,000
Ahsante kwa complement. Ulichosema ni sahihi kabisa.

Hapana. Ni Software as a Service. Kwa sasa hatufanyi self hosting na hakuna mpango huu in any foreseeable future

Kwa sasa Android App ina lugha zote mbili, kiswahili na Kiingereza. Kwa upande wa Web kuna Kiingereza na kiswahili bado kianendelea kufanyiwa kazi. Siku sio nyingi option ya kiswahili kwa ukamilifu wake itakuwa inapatikana.

Iko based na plan ambayo mteja atachagua. Kila Plan ina features zake as well as limit ya watumiaji. Tunaamini kabisa tumefanya segmentation ambayo itawasaidia Watumiaji kuchagua wanachokitaka. Kwa anayetaka full features kuna plan ya Pro.
Taarifa zote zipo kwenye website yetu iliyopo kwenye kipeperushi. Bahati mbaya JF kona hii hawaruhusu kuweka link!Tumejaribu kufikiria kila namna, reasonable ya ku cover base kubwa zaidi. Tunaamini wengi wataweza kuchagua sehemu wanayoitaka.
Kama kuna mteja ambaye anadhani mahitaji yake hayako covered na hizi Plana anaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizo hapo kwenye kipeperushi. Tunaweza endelea naye na kumsikiliza tokea hapo!

Sijaelewa una maana gani maana hii ni pana kidogo. Kama unamaanisha kuweza kulipa moja kwa moja kwenye simu yako ukiwa kama mteja wetu, hizi options ziko underway. Tutakuwa tunatoa update hapa na kwenye Insta account yetu adiuta_biz

Kuna mengi yanaendelea chini ya kapeti, ila itoshe kusema tu mapinduzi makubwa ya uendeshaji wa biashara yameanza na mambo mazuri mengi yanakuja!

Ahsante sana kwa zawadi hii.
Kwa niaba ya Kampuni, tunashukuru!

Karibu sana!
Responding style yako kama mwalimu.NImekuelewa.Lets keep in touch.
 
Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,291
2,000
Pale unapolipia plan yoyote, staff wetu atakupitisha kwenye system nzima akikufundisha namna ya kuitumia kwa matokeo bora zaidi.

Unahitaji computer ikiwa na Zoom au Skype na akaunti yako ya Adiuta. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba hizi:
Piga: +255673651520 or +255767893474
WhatsApp: +255767893474
 
Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,291
2,000
Je Biashara yako inakulazimisha uwe unatembea mara kwa mara? Au kuna wakati unataka kufanya baadhi ya kazi muhimu mahali ulipo?
Tumekusikia! Ukiwa na Adiuta Mobile App, utaweza kufanya kazi Muhimu kama kutengeneza, kuidhinisha na kutuma Ankara kwa mteja wako, au kutengeneza, na kuidhinisha Bili zako.

Pamoja na haya unaweza kurekodi miamala ya Benki, Mauzo ya bidhaa na mengine mengi: Yote kwenye kiganja chako.
Jisajili leo bure na uujaribu mfumo wetu, kwa siku 30!

Ni wakati wa kuhamishia biashara Dijitalini kwa usimamizi na makuzi bora!

WhatsApp Image 2021-08-03 at 11.48.53.jpeg
 
Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,291
2,000
Una Duka la Dawa, Vinywaji, Vyakula, au aina nyingine za biashara zinazofanana na hizi? Tunakuletea Adiuta Business Assistant, msaidizi wako katika biashara. Adiuta inakusaidia kujua mauzo yako, bidhaa zilizobakia, bidhaa zinazoelekea kufikia mwisho wa matumizi yake, na mengine mengi.

Wakati wa mauzo Adiuta itakuelekeza bidhaa za kuuza, ili bidhaa za zinazokaribia kufikia mwisho wa matumizi ziuzwe kwanza, na kukuepusha na hasara ya bidhaa kutupwa kwa kufikia mwisho wa matumizi. Pamoja na mengine mengi, Adiuta inakusaidia kuendesha biashara yako kisasa.

Kwa maelezo zaidi, mafunzo na maswali usisite kuwasiliana nasi: Piga simu: 255673651520 au tuandikie WhatsApp 255767893474 Pia tunapatikana Instagramu kwa handle ya adiuta_biz karibu tukuhamishie biashara yako kwenda Dijitalini!

IMG-20210805-WA0003.jpg
 
Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,291
2,000
Una Supermarket na ungependa kupata suluhisho la kuisimamia ukiwa mbali? Basi usiache kuwasiliana nasi. Pia unaweza kujiandikisha bure na kuijaribu program hii bure kwa siku 30 kuona kama inakufaa ama la.

Inaungwanishwa na printer kwa ajili ya risiti na unaweza kutumia barcode scanner kurahisisha uingizaji wa bidhaa wakati wa kuuza.

IMG-20210812-WA0040.jpg
 
Cybergates

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
469
1,000
ja
Screenshot from 2021-08-17 09-02-53.png

Nitaleta mrejesho baadae. nimejaribu kuitumia kama siku mbili ivi. baada ya kuitumia nikajaribu kumfundisha na bimkubwa nitaleta maoni baadae. Mda Huu ngoja kwanza tujengea ili taifa
 
Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,291
2,000
Hongera sana Cybergates nitafurahi kuona review yako ya mazuri na mapungufu. Tuko tayari kuyafanyia kazi mapungufu. Kuna nyongeza ya mambo machache:
1. Tupo kwenye utaratibu wa kuandaa documentation. Kila mara tunaongeza maelezo ya namna ya kutumia Adiuta. Unaweza kupitia Documenation link pale adiuta.com
2. Kama bidhaa unazotumia kwenye Inventory zina Barcode then unaweza kutumia barcode reader. Hakikisha kila product in UPC field umejaza barcode number/code. Then wakati wa kuuza unascan tu bidhaa, Adiuta itaiongeza automatically bila ku type

Ukiwa na changamoto yoyote, unaweza kuripoti kwa contact zetu, au moha kwa moja kwenye mfumo kwenye Get help menu kwa step hizi

1. Click profile name utapata

Screen Shot 2021-08-17 at 10.30.46.png

2. Click Get help & Support

Screen Shot 2021-08-17 at 10.30.59.png

3. Bonyeza Open Ticket na kisha jaza tatizo na tuta respond

Screen Shot 2021-08-17 at 10.31.10.png

Ahsante kwa kuijaribu Adiuta na kuwa mjumbe wetu. Kwa niaba ya HHTCL tunashukuru sana!
 
Cybergates

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
469
1,000
Hii System nimeitumia kwa mda, niliitumia package ya free trial. Kuna baadhi ya mambo nime appreciate sana pia kuna changamoto nilikutananazo

Kwanza nilipenda kwenye kufungua account email ya registration ilikuja faster sana. Pia option ya kuadd user pia nimeikubali sana. Error za js kwenye form zipo vizuri

Pia fee ya subscription sio kubwa sana kwangu naona ipo sawa tu

Sema sasa mara ya kwanza najisalili ilikua shuhuli nilivyo click link ya ku activate email ilinipeleka kwenye error page. hapa nili kwama kama dk 9 ivi mpaka nakuju kifika page ya register bussines nilikua nime click link zote na ku login upya.

Tatizo lingine likaja kwenye kujaza taarifa za setup opening bussines. Dha mkuu zile input ni nyingi sana bro. Nilikua nawaza hapa labda ugejaribu ku ka-categories labda input za finacial statiment, balance sheet, expenses etc na input nyingine ziwe option tu, pia ungeogezea mtu aweza ku add manually taarifa zake. Labda account ya discount allowed awe anaweza kufanya wenyewe bila kutegemea default zilizopo. Pia nilizaja taarifa zangu hapo form ikawa ina leta tu error ikabidi ni skip sijajua shida ni nini.

Pia kwenye option ya ku add user ungetupatia option ya ku add avatar ya huyo user alafu pia mm kama admin niweze ku set limitations za huyo user labda aweze ku access only category ya sales au expenses pia aki login huyo user aone tu option za kwenye category alizo pewa access.

Pia kwenye product ungetupa uwezo wa ku set hata picha moja ya iyo bidhaa. Pia ku add bidhaa moja moja inachosha sana mkuu ungejaribu kutupa uwezo wa ku add in bulk kwa kutumia hata excell ingesaidia sana na pia ing'e save mda.

Kwenye swala la payment mkuu nilijaribu ku add taarifa za malipi zonagoma. Niambia payment amount lazima iwe sawa na package duration. Nilijaribu kwa both usd na tzs. Alafu sijajua reference pale na jaza nini transaction date au transaction ID.

Ku ujumla system ipo vizuri pia documentation ipo sawa
 
Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,291
2,000
Hii System nimeitumia kwa mda, niliitumia package ya free trial. Kuna baadhi ya mambo nime appreciate sana pia kuna changamoto nilikutananazo

Kwanza nilipenda kwenye kufungua account email ya registration ilikuja faster sana. Pia option ya kuadd user pia nimeikubali sana. Error za js kwenye form zipo vizuri
Ahsante kwa head up boss!
Pia fee ya subscription sio kubwa sana kwangu naona ipo sawa tu
Tumefurahi pia kuwa tumeweka structure inayofanania thamani tunayoitoa.

Sema sasa mara ya kwanza najisalili ilikua shuhuli nilivyo click link ya ku activate email ilinipeleka kwenye error page. hapa nili kwama kama dk 9 ivi mpaka nakuju kifika page ya register bussines nilikua nime click link zote na ku login upya.
Hili pia tuliliona wakati wa routine maintenance. Liko fixed as of now. Kama kuna mtu atakayetengeneza akaunti akakutana na hii shida nitafurahi kupata mrejesho.

Tatizo lingine likaja kwenye kujaza taarifa za setup opening bussines. Dha mkuu zile input ni nyingi sana bro. Nilikua nawaza hapa labda ugejaribu ku ka-categories labda input za finacial statiment, balance sheet, expenses etc na input nyingine ziwe option tu,
Hii ni sehemu pia ambayo tulikuwa tunawaza namna bora ya kuiweka. Kuhamisha biashara kwenye system mpya ni changamoto sana hasa kama mtumiaji sio mhasibu na hana accounting background. Maoni yako haya ni mazuri na ya thamani, tutayafanyia kazi kikamilifu.

pia ungeogezea mtu aweza ku add manually taarifa zake. Labda account ya discount allowed awe anaweza kufanya wenyewe bila kutegemea default zilizopo.
Unaweza ku setup Chart of account kwa namna unavyopenda mwenyewe. Ukiacha System accounts ambazo huwezi ku edit, zingine zote unaweza ku edit na hata kufuta kama haina data au kui archive kama ina data na hutaki kuitumia tena.

Kwenye Menu kuu nenda Accounting --> Chart of Acounting na hapo unaweza ku set accounts zako upendavyo. Naomba uiangalie hii halafu kama kuna kitu hautakiona utaniambia tuone namna ya kuweka.

Pia nilizaja taarifa zangu hapo form ikawa ina leta tu error ikabidi ni skip sijajua shida ni nini.
Nitapitia tena nione kuna shida gani. Ahsante kwa taarifa!

Pia kwenye option ya ku add user ungetupatia option ya ku add avatar ya huyo user alafu pia mm kama admin niweze ku set limitations za huyo user labda aweze ku access only category ya sales au expenses pia aki login huyo user aone tu option za kwenye category alizo pewa access.
Hii inawezekana ila huwa inakuwa inamchanganya mtumiaji ambaye sio mtaalam. Kama utanisaidia exactly unataka ku limit vitu gani, tunaweza kuangalia namna ya kuweka advanced settings zikiwa na manageable options maana as of now kuna permissions nyingi, zaidi ya 50. itakuwa very confusing kuziruhusu zote ziwe configurable. Kwa hiyo tungetamani kuachia zile tu relevant. Na ndio maana mahitaji yako exactly hapa yatasaidia sana kwenye hili.

Pia kwenye product ungetupa uwezo wa ku set hata picha moja ya iyo bidhaa. Pia ku add bidhaa moja moja inachosha sana mkuu ungejaribu kutupa uwezo wa ku add in bulk kwa kutumia hata excell ingesaidia sana na pia ing'e save mda.
Kwenye picha inawezekana, ila unaweza kueleza rationale? Mnatumia eCommerce somewhere? Ninatamani kuelewa kwa nini mnahitaji picha japo sio ajabu kwenye inventory.

Bulk Import iko njiani possibly next week itakuwa tayari. Tupo tunafanya utaratibu wa kuwahamisha watumiaji wa SupaDuka (Sina hakika kama bado developer wa hii software wanaitengeneza) na thru the process tunatengeneza Bulk Import feature. So usiwe na shaka, inakuja.

Kuna specific software ambayo ulikuwa unaitumia? Kama unaweza ku share Excel format uliyo nayo ili katika design iwe considered pia nitashukuru!

Kwenye swala la payment mkuu nilijaribu ku add taarifa za malipi zonagoma. Niambia payment amount lazima iwe sawa na package duration. Nilijaribu kwa both usd na tzs. Alafu sijajua reference pale na jaza nini transaction date au transaction ID.
Pole kwa kupata taabu boss. Tunaomba radhi kwa usumbufu.
Integration zinaendelea za malipo na kadri muda unavyokwenda tutakuwa na automated integration na Billing interface itakuwa improved na itakuwa na information chache sana.

Kwa Tigo unaweza kulipia automatically kuanzia sasa, just kwenye Payment Chagua Tigo Pesa kama inavyoonesha chini hapo

Screen Shot 2021-08-19 at 12.25.45.png

1. Payment Date:
Ni Siku ambayo umelipia

2. Method:
Ni njia ya malipo ulioiyoitumia kulipia. Ukichagua hapa itakupa taarifa za namna ya kulipia. Kwa zile ambazo auto-integration haijakamilika zitakupa manual way ya kulipia zikiwemo process na namba za malipo.

3. Amount:
Ni kiwango unacholipia. Hiki lazima kifanano na Plan. Mfano, picha hapo juu inaonesha Plan ni Pro ambayo ni 94,000TZS na ni kwa mwezi. Kwa hiyo kama nimechagua mwezi mmoja nitaweka kwenye amount 94k. Nikichagua miezi miwili ninapaswa kuandika 188k, na kuendelea. Naona inaleta confusion, kwa hiyo field ya Amount tutaitoa, mtu achague miezi tu halafu iwe auto calculated. Ahsante kwa ku report hii issue. Tuta review pia Billing Interface!

4. Reference:
Hii inatumika kwa sasa kwa jili ya kusaidia manua verification. Mfano ukilipa kwa MPESA kwa sasa inabidi kulipia kawaida kwa USSD/MPESA app. baada ya malipo kukamilika inakurudishia reference namba. Ile ndio reference utaiweka hapa kusaidia msimamizi wetu wa akaunti kuhakiki malipo na mlipaji. Ila kadri tunavyofanya automation hii field itaondoka moja kwa moja.

5. Currency:
Hii ni sarafu ya kulipia. Kwa sasa tuna support TZS tu. Ila tutakuwa na support ya USD baada ya kumaliza hii hatua ya ndani na kufungua matumizi kwa Internationals. Kwa hiyo kwa sasa tuna disable selection mpaka hapo baadaye. Hapa pia nikushukuru kwa kutoa taarifa.

6. Period:
Hiki ni kipindi ambacho unalipia. Mfano umeamua kulipia kwa miezi sita sita. Hapa utachagua 6 Months. Hakikisha Amount pia inakuwa ni ya miezi sita. Hapa tutaboresha ili kuepusha usumbufu wa mteja kupiga hesabu. Pia nikushukuru kwa kuripoti hili. Tutalifanyia kazi kwa udharura.

Ku ujumla system ipo vizuri pia documentation ipo sawa
Ahsante kwa Compliment. Tunajitahidi kuweka documentation iwe bora zaidi. Ukikutana na mapungufu kwenye documentation usiache kutuachia maoni ili tuboreshe zaidi. Tunatamani kushindana katika anga za kitaifa na kimataifa na ni maoni ya wateja wetu kama wewe watatusaidia kufikia lengo.

Tunakushukuru sana!
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
10,537
2,000
Kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri na hatua mliyofikia.Functionalities nimeona ziko za kutosha na bado naona kama product iko room ya kuimprove hasa kwa kuwa ni local content basi ni fursa kwenu developers na kwa market kuikuza.Maswali yangu ni Je mko na self hosted option? Je iko katika lugha ya kiswahili na kiingereza?Je ni mdular product yaani mtu anaweza kuicoustomize kwa kuzingatia aina ya biashara/hudma yake?Je selling point ni idadi ya users au n functionality au ni vyote?Maana nammini kabisa kwamba hii kama business suite ni vyema mtu akapewa access ya all business functioanality na kisha selling point ikawa ni idadi ya users,self hosted au hosted,training and support,etc.

Maoni yangu ni kama mtu ambaye niko sokoni kama muuzaji wa aina mbalimbali za product na nimekuwa nikipata shida kupush local product sokoni kwa sababu ya hizo limitation hapo juu.

Vile vile kukiwa na module ya kuwezesha payment integration itasaidia sana kuhakikisha kwamba hata mobile payment,epayment zinakuwa supported.

Vile vile mnaweza kuongea na TRA kuwe na uwezekano wa integration ya Virtual efd ili mtu akinunua mfumo wenu asilazimike kuwa na EFD bali risit zake ziwe verified na TRA.Najua option hizi zote zinawezekana technologically na zina gharama ni ninaamini mnaweza kuziweka katika plan ya future edition.

As a courtesy nitawasilisha product yenu kwa baadhi ya potential clients na nitawapa mrejesho.

Otherwise nawatakia kila la heri.

Keep up the good work!!!

NB.Nitakutafuta PM tujadili namna tutafanya kazi pamoja.
Aaaaaaaah we nae.... TRA wamekujaje tena huku?! Yale majizi hayatakiwi kushirikishwa kwenye mambo ya kisasa. Yakija na huku yataharibu kila kitu.

Mamlaka za serikali kazi yao kuu ni kudhoofisha, kufilisi na kuua biashara za watanzania so huwa sionagi point ya kuwahusisha na mambo kama haya wapuuzi wale.
 
Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,291
2,000
Aaaaaaaah we nae.... TRA wamekujaje tena huku?! Yale majizi hayatakiwi kushirikishwa kwenye mambo ya kisasa. Yakija na huku yataharibu kila kitu.
Hapa mdau alikuwa anaongelea kuhusu TRA validated Receipts. Hili ni suala muhimu sana. Kuna watu wana biashara na wanalazimika kuwa na EFD mashine nyingi na kila moja inagharimu fedha. Kwa hiyo ukiunganisha mfumo na VFD maana yake ni kuwa hautakuwa na haja ya kuwa na mashine nne kwa sababu tu una maduka manne yaliyo katika sehemu nne tofauti.

Hata hivyo, ikiwa tutafanikiwa kuunganisha na TRA, itakuwa ni optional addon ambayo mtu anaamua mwenyewe. Hatutamlazimisha mtu kama anaona hahitaji hiyo option.
 
Umefafanua vizuri sana nitakupigia tuyajenge......
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom