Adhabu za wanajeshi

Itakuwa enzi za mwalimu hizo au nao polisi waliokuwa kwenye kituo hicho walikuwa wapumbavu
 
Sasa hivi sifa ni pesa sio upot, aje na upot wake aje na mwenye pesa zake hata Dem, alaf tuwafungulie mbwa wakali tuone ni nani atakaeng'atwa

yani hapo lazma pot ang'atwe na upot Wake maana hana pesa.
Wewe ukifunguliwa mbwa mkali wale mbwa vichaa Germany shefad una uhakika utapona ?
 
Itakuwa enzi za mwalimu hizo au nao polisi waliokuwa kwenye kituo hicho walikuwa wapumbavu
Enzi hizi unakuaje wanafungulia kesi Mahakamani au sio au wanaongeza na kasimu ?
 
Tanzania hadi ufungue kesi hio labda uende ukafungue kesi kwa kasimu bila hivyo unakusumbua tu, Mahakama inafanya kazi na Jeshi la Polisi usijifanye haujui, ushanielewa lakini au nikwambie tu ulichokiandika kipo kwenye CPA na kwenye Penal Code Ila wakikubanisha lazima wakuchangamshe damu kidogo ili uwe adabu siku nyingine usirudie kufanya ujinga, sawa na mama yako akwambie usichezee kiwembe hicho ukachezea kikakukata akiona umejikata anakuosha kwanza mabanzi ya sura km manne hivi au matano alafu ndio anakupa huduma ya kwanza ili siku nyingine usirudie kufanya ujinga wewe mtoto Mpumbavu, mwanajeshi ampi adhabu za kuchosha raia mtiifu, tembelea shule zilizo karibu na kambi za Jeshi asubuhi mtu km wewe wale watoto unaweza ukasema wanaonewa tena unaweza ukaingilia kati uwaambie jamàa waache kuwapigisha kwata wasiendelee kuburuzwa kwa kuwapigisha gwaride la kufanya kazi za usafi wa shule asubuhi asubuhi na baridi
 
Akhil za mtanzania
 
02.Tukio la pili ni siku ya kwanza kwenda pale shuleni! Ilikuwa form five!
Aisee kwanza nilienda shule saa mbili ahsubui, nikamkuta MP anaitwa MSENGI. Akaniweka bakora nne, huwezi amini day one.
Hii kawaida.
Day 1 nilienda na sketi nimeshona kwa fundi Maiko, sikuvaa zile zao na viatu vyao sijavaa.
Kumaliga akanidaka.. akanipeleka kwa Matrons, anawaambia huyu hajavaa nguo zetu.
Kufika kwa Matrons nikiwa Dar hali ya hewa inanitakatisha flani hivi, kauso kanakuwa 👌Yule Matrons akaniangalia kwa wenge sijui akanambia nimejiremba 😂😂
Uwii niliambiwa kanawe uso urudi unatiririka maji.
Na bado nikachapwa kwanini sijavaa sketi zao na viatu vyao.
 
Kabla sijakuunga mkono kuhusu kutoogopa kifo kwako, tuambie ulishakufa mara ngapi ili tujue uhalisia wa kauli yako
 
Kuna jamaa alitaka kuovertake msafara wa wajeda barabara ya Iringa~Dar, kabla hajamaliza kuyapita magari yao mbele gari ikatokea ikabidi abane katikati ya wajeda. Aloo walimwambia nae Kawa part ya msafara wao Hadi DSM wakati jamaa alikua anaishia Moro.
 
Hawakuzingui km hujazingua, pita Lugalo nenda kwenye zile bustani za pembeni vua sketi yako mwaga kojo alafu jamaa wakuone hakikisha wamekuona
Napitaga zangu tu pembeni huku, ila Sasa Hadi avue nguo hadharani huyo si mgonjwa wa akili
 

 
Mie mwenyewe sikubali mtu anizalilishe kisa eti ni mjeda na Kuna wajeda wengine huzalilisha Hadi watu umri wa kuwazaa kabisa eti kisa mjeda. Jamani Mimi sifanyi adhabu yoyote tuone ka wataniua
 
Siyo wanajeshi matured tu mkuu, bali na waliosoma yaani wenye elimu zao, utayakuta mambo haya kwa watoto wa masikini wenye elimu za fom foo tena za kuunga unga
 
Si unataka kujua km wanajeshi wanabutua au wanafanyaje, hawakupi adhabu km huna kosa au hujawakosea hususani unapokua mazingira ya eneo la Jeshi
Hekima ni hii, hakuna haja ya kujifanya mjuaji ukikosa. Tii na uwe mpole tu.
 
Kiranga sorry, wewe ulikuwa na jina au ulitumia tu jina la huyo mwenzako wa kwa Baba Ben?
 
Huo unakuwa mshamba mkuu. Hawawezi man to man
Man to man kuna watu wapo vizuri kuliko hawa wanajeshi,
Kisa kingine kuna mshikaji anaendesha bajaj hapa maeneo ya Mwenge,basi kuna siku anavuka tu barabara bila bajaji kuna gari ya wanajeshi walikuwa wawili wakampelekea mshikaji anaevuka kwa miguu zima zima,sasa yule mshikaji kuona anataka kugongwa na lile gari si akamind na wale wajeda wakamind mjeda mmoja akashuka kumfuata mshikaji,anataka kumkamata mshikaji bahati mbaya ikamtoka ngumi bhana ikampata yule mjeda usoni,bahati nzuri kabla ugomvi haujaendelea watu tukajaa tukawaamua wasipigane,yule mshikaji akapata upenyo akakimbia kumbe wale wanajeshi wakauliza wakaambiwa kuwa yule mshikaji anapaki bajaj pale Mwenge,kesho yake wakaja watatu wakamkuta mshikaji wakamchukua mpaka kwenye uwanja wa vinyago pale Mwenge huwa wanacheza mpira,wakaanza kumuogesha matope mshikaji bhana,kumbe pale kuna mkubwa wao akawauliza inaama huyu mtu aliepigana na mwanajeshi ndio huyu?embu muachane aondoke zake mnalidhalilisha jeshi tu,maana huyo mshikaji ukimuona ni mwembamba kichizi.mshikaji karudi kijiweni kalowa tope mwili mzima.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Haya hufanywa na askari wadogo tu
 
Afandeeee K
Arando

Kuna siku ilikuwa ni mida ya kutoka sasa, ni jioni saa 11 nikakatiza pale Smart Area nikapaona peupe pee nikajua hakuna watu, nikaanza kutembea kiboss.
Kumbe bwana kuna watu nyomi wameshikwa wapo nyuma ya ofisi kwa kosa la kutembea na sio kukimbia. Ile kukatiza tu nakuta naitwa "Wee kuja hapa" ile kwenda tu nakuta watu nyomi wanapihishwa push up.
Aisee nilikoma.
2017 hiyo
 
Bangi haijawahi mwacha mtu salama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…