Adhabu za wanajeshi

Adhabu za wanajeshi

Mimi sikubaligi upumbavu, huyo mwanajeshi mshamba na njaa Kali angekuja kwangu aone, ningevomjibu dry sitishiwi bunduki Mimi, Wala sitishiwi kifo hata siku moja

Angeenda ailete hata Kambi nzima, siogopagi kufa Mimi, liwalo na liwe na ndo wangejua kweli hii Dunia kuna watu watata, sio Dunia, Tanzania kuna watu watata. Mimi ndio MWAMBA.
Safi sana.
Hamna shida.
Ipo siku utaumia tu.
 
Kiranga sorry, wewe ulikuwa na jina au ulitumia tu jina la huyo mwenzako wa kwa Baba Ben?
Romeo and Juliet Act II, Scene II, William Shakespeare

Juliet:

O Romeo, Romeo! wherefore art thou Romeo?
Deny thy father and refuse thy name;
Or, if thou wilt not, be but sworn my love,
And I'll no longer be a Capulet.

Romeo:

[Aside] Shall I hear more, or shall I speak at this?

Juliet:

'Tis but thy name that is my enemy;
Thou art thyself, though not a Montague.
What's Montague? It is nor hand, nor foot,
Nor arm, nor face, nor any other part
Belonging to a man. O, be some other name!
What's in a name? That which we call a rose
By any other name would smell as sweet;

So Romeo would, were he not Romeo call'd,
Retain that dear perfection which he owes
Without that title. Romeo, doff thy name,
And for that name which is no part of thee
Take all myself.

Romeo:

I take thee at thy word:
Call me but love, and I'll be new baptized;
Henceforth I never will be Romeo.
 
Wanajeshi wengi huwa hawajui sheria atakunyanyasa akikutana na wewe ambae umelelewa kwenye misingi ya uoga uoga ila ukikomaa nae mwisho huwa wanaomba radhi na hata fidia unalipwa maana anajua kazi yake inaenda kuharibika

Kuna askri mmoja wa jwtz private ndugu yake aligongwa na pikipiki baada ya kugongwa na pikipik kesi ilienda hadi mahakamani kesi ikaisha kwa maamuzi ya mahakama lakini aliegongwa akawa bado anaendelea na matatibabu.

Jamaa huyo private wa jwtz akiwa likizo alichoamua kukifanya akiwa yupo likizo akaenda kumkamata yule jamaa aliemgonga ndugu yake na baada ya kumkamata akaenda kumfungia kwao hilo Ni kosa la kwanza alifanya kinyume na sheria(utekaji)

Kosa la pili akiwa anamuhoji akampiga yule jamaa akishinikiza kuwa jamaa amuhudumie mgonjwa wao hilo ni kosa la pili (shambulio la kudhuru mwili) kilichotokea hapo ni kuwa ndugu wa yule ndugu yao ambae amefanyiwa hivyo walikua wanajua haki zao wakakusanya ushahidi wote na mashahidi wakawepo ndugu yao alivyoaachiwa tu akiwa na majeraha wakaenda kuchukua pf 3 polisi ikaenda kuthibishwa na daktari kuwa jamaa kweli kashambuliwa na kapata madhara (hapa tayari shahidi wa 3 ambae ni daktari kapatikana)

Baada ya kutoka hospitali Sasa wakaenda kufungua kesi ya shambulio polisi kwakua ushahidi wote upo polisi ikabidi waende kumkatamta katika kumuhoji kumbe kweli alikua ni Askari wa jwtz, kilichotokea hapo taarifa ikatumwa kikosini kwake, utaratibu ulivyo ni kuwa Askari yeyote hapelekwi mahakama za kawaida kwa makosa ya jinai hadi kwanza apitie mahakama za kijeshi na afukuzwe kwanza kazi ndo apelekwe akiwa kama raia wa kawaida

Hali ilipofikia hapo na ndugu wa yule mwanajeshi wakaona kibarua cha mtoto wao kinaenda kuharibika ikabidi wajishushe wakaenda kuomba msamaha kwa yule alieshambuliwa wakabembeleza sana ili aifute hiyo kesi mwisho jamaa alikubali akapokea fidia lakini muda huo yule private wa jeshi kashakaa lockup ya polisi siku 6 maana utaratibu ilikua kikosini kwake ndo waje wamchukue lakin hawakuja kwa siku zote 6

Baadae kesi ilifutwa lakin Kama jamaa wangekomaa nae alikua anaenda kufukuzwa kazi kwasababu ameiingilia hadi mahakama kwa kesi ambayo ilishatolewa maamuzi,lakin pia alifanya makosa ya jinai kuteka na kushambulia

Sasa watu wanatakiwa wajue haki zao na siyo kutishwa tishwa wanakua Kama kondoo mwisho wa siku tunakua na taifa la wajinga

Asante Kwa kutuelewesha lakini watz wengi ni waoga
 
Siku moja Wajeda wa Mwenge miaka ya nyuma kidogo walijichanganya kwa kijana mmoja mtu wa mazoezi sana, Alikuwa bado denti lakini mtu wa Mazoezi sana, alikuwa akicheza karate. Dogo anawahi shule, kupiga paper, wakamzingua kwa kumuita ili aende walipokuwa wamekaa, dogo akawaambia anawahi hawezi kwenda. Dogo alipotembea mita kadhaa mbele, Jamaa hawakuridhika, mmoja akamuungia ili amsimamishe amchimbe biti. Jamaa akataka kutumia ubabe, Dogo akaona isiwe tabu, akasimama kiume akazipanga na jamaa, mkono ukapigwa pale. Mjeda ulimi huu. Wakaja wajeda wengine ili kusaidiana na Jamaa, Dogo bado akajisimamia, Mkono ukapigwa pale, Dogo kagoma kuwa kondoo. Mpaka raia wakaanza kusogea. Wakaona isiwe tabu wampeleke ndani kwa mkubwa, dogo akakubali kwenda. Kufika kule Mkubwa akawaona wale Wajeda wendawazimu. Wamefanya Ujinga. Dogo akawachimba biti wale jamaa kuwa hawajamalizana, na yeyote atakayekutana naye kitaa ama zake ama za mjeda, Ugomvi bado haujaisha!. Ilibidi wajeda wake watume watu wa kureconcile na Dogo maana naye ni mtoto wa mitaa ile. Na wajeda sometimes huingia mitaani.

Nguvu ya Wajeda ipo katika Kamandi, na ndani ya formation za kikosi. Kama Ukijipanga vizuri, na unajiamini na ukikataa intimidation za kisaikolojia unaweza kusimama naye man to man na ukamnyoosha vizuri ili aende akaite wenzie.

Mob psychology inawasumbua baadhi ya Wajeda.
 
Tulipokuwa jkt kuna ile siku wanaita msafara wa polini. Sasa kuna raia alikuwa anaendesha pikipiki ina mzigo pembeni yetu. Jamaa wakamchomolea funguo wakamwambia awafuate na kuiacha pikipiki hawaezi. Ikabidi mwamba asukume.
 
vijana wa JKT nao wakajioba Masoja?
 
Kwenye pitapita zangu nikaingia kwenye eneo la Jeshi kukata majani ya kulisha ng'ombe. Mbele yangu kulikuwa na maembe dodo yanatamanisha sana. Sasa mimi sikujua kama ni eneo la jeshi.

Nikaenda chini ya embe dodo nikaanza kuyapopoa maembe.

Muda kidogo naona pale nilipoacha mkokoteni wa kubebea majani kuna mtu amekaa na magwanda, huku anazuga anaongea na simu.

Oya, siisahau ile siku.
Tupe mkasa mzima jombaa😂
 
Hawa Jamaa usiombe uingie kwenye 18 zao, utajuta kuwafahamu.

Siku moja Tulikuwa kwenye foleni ya kuelekea mjini, kuna jamaa wa Lori akaziba geti la kuingilia pale kambi ya Abdallah Twalipo uhasibu. MP akamfuata kistaarabu kabisa "mambo vipi Kaka?" Jamaa akaitikia "Safi kabisa afande". Afande akamuuliza hapa uliposimama si unajua Kama ni getini? Mwamba kwa kujiamini kabisa akaitikia ndiyo afande ila tatizo foleni haitembei, Sina jinsi, samahani sana.

Kama kawaida ya wanajeshi kujifanya wastaarabu kwenye matukio ya aina hii. Afande akamwambia sasa ndugu kwa kuwa foleni haiendi shuka tu hapa upumzike tupige stori, foleni ikitembea utaendelea na safari yako. Dereva wa Lori kwa mbwembwe akafungua mlango ashuke eti apumzike na wanajeshi. Hapo ndiyo 'ntiti' ulipoanza!!

MP akamwambia "kaka sijasema ushuke mlangoni, shukia dirishani" lilikuwa ni tukio la kuchekesha Sana kwa sisi wapita njia ila kwa lililomtokea lilikuwa ni tukio mbaya na la kufedhehesha.

Picha linaanza,gari anayoendesha jamaa ni Scania R 420,Chuma mpya kabisa ya Transit alafu imepanda hewani Kama farasi, imebeba mafuta inaelekea nje. Gari ikisimama dereva unamwona yule kuleee ghorofani. Sasa vuta picha dereva ameambiwa ashuke kupitia dirisha badala ya mlangoni. Sisi wengine wa pembeni Tulicheka Sana maana jamaa kwanza ni bonge alafu ili ashuke kwa kutumia dirisha inabidi ajikusanye awe Kama fungu la nyanya Kisha ndiyo atoe miguu nje. Ilimchukua karibia dakika 15 kushuka. Wakati huo MP alikuwa siriazi hacheki wala haongei. Yeye anamsubiri jamaa tu ashuke wapige stori. Dereva akadondoka chini Kama mzigo wa viazi mbatata vya Mbeya..Tiii!!

Suruali yote imechanika kwenye maungio ya miguu. Aliposhuka huku kijasho kinamtoka mjeda akaanza kupiga nae stori Kama hakuna kilichotokea "naona chuma imeshakunywa wese inasepa?" Dereva kinyonge akajibu yeah inaelekea Ndola, Zambia. Wakapiga stori Mara foleni ikafunguka magari yakaanza kutembea. Afande akamwambia dereva Sasa unaweza kwenda tu maana gari zinatembea. Dereva akatoa shukrani Kisha akaelekea kwenye gari yake asepe.

Cha ajabu wakati dereva anafungua mlango Mjeda akamwambia mzee baba si tulikubaliana tunapitia dirishani? Ahahahhaha kazi ya kupanda dirishani ikaanza tena. Nina uhakika Yule dereva alimtukana mjeda matusi yote ya hapa duniani ila kimoyomoyo.. Ile siku yule dereva hataisahau kamwe maishani.

Unakumbuka kisa chochote Cha wanajeshi na adhabu zao kwa raia pindi raia akijichanganya kwenye anga zao?
Duh! 😂😂
 
Ila wajeda Kama kweli mbinguni kupo Basi wengi wao watabaki kupasikia tu.

Hawa jamaa Ni makatili Sana.
 
Afande akileta upuuzi huo unamgomea tu, maana ni kinyume cha maadili ya kazi za jeshi. Hawezi kukufanya lolote. Hawezi kukuua na kama Akikudhuru unamfikisha kwa wakubwa wake tu , uone kama kibarua chake hakijaota nyasi.

Tatizo watu hawajui haki zao na wanaogopa magwanda. Lakini nidhamu za kijeshi zinakataza kabisa askari kuonea raia.
Unafika kwa wakubwa zake ukiwa ushaumia, inasaidia nini sasa??
 
Mimi sikubaligi upumbavu, huyo mwanajeshi mshamba na njaa Kali angekuja kwangu aone, ningevomjibu dry sitishiwi bunduki Mimi, Wala sitishiwi kifo hata siku moja

Angeenda ailete hata Kambi nzima, siogopagi kufa Mimi, liwalo na liwe na ndo wangejua kweli hii Dunia kuna watu watata, sio Dunia, Tanzania kuna watu watata. Mimi ndio MWAMBA.
Ulishawahi kufa mara ngapi??
 
Unafika kwa wakubwa zake ukiwa ushaumia, inasaidia nini sasa??
Kwanza ukifika kuna wakukusikiliza mwache ajipe moyo, ukiona unasikilizwa ujue hyo ni critical issue kweli kweli la sivyo ukifika ataitwa "afande maro mbona kijana amechafuka embu mpereke akaoge" hapo ujue unaenda kuoga vumbi ukitoka huko hurudi tna
 
Back
Top Bottom