Adhabu ya UHAINI ni KIFO pekee?

Adhabu ya UHAINI ni KIFO pekee?

Nimekuwa nikiona mjadala kuhusu adhabu ya uhaini hasa kwa vifungu alivyotuhumiwa navyo Tundu Lissu. Kumekuwa na upande ambao umekuwa ukisema adhabu stahiki si lazima iwe kifo lakini wapo na hasa (Tundu Lissu mwenyewe) kuwa kisheria ni lazima adhabu iwe kifo.

Nimechukua muda wangu kutafuta na kusoma kwa kina kanuni za utoaji hukumu za majaji na mahakimu wa Tanzania yaani "Tanzania Sentencing Guidelines of 2023". Baada ya kusoma hasa ukurasa wa 8, 9 na 10 nimejiridhisha kwamba kwa mujibu wa kifungu alichoshitakiwa nacho Tundu Lissu kama akikutwa na hatia adhabu ya kifo ndiyo adhabu pekee stahiki.

Kanuni hizi zinaeleza kwamba pale ambapo kifungu cha sheria kimetumia kauli "... shall be sentenced to death" basi hapo Jaji hana chaguo zaidi ya kutoa adhabu ya kifo. Sasa ukisoma kifungu alichoshitakiwa nacho Tundu Lissu yaani kifungu cha Penal Code cha 39(2)(d) kimetumia maneno "... shall be sentenced to death" hivyo hukumu ya kifo ni ya lazima.

Aina hii ya uandishi utaiona katika kifungu cha 197 cha Penal Code ambacho pia kinatoa adhabu ya kifo kwa kosa la mauaji ya kukusudia (murder) ambacho nacho kinasema nanukuu:

"197. A person convicted of murder shall be sentenced to death.".

Kama kifungu hiki cha murder kinatafsiriwa kwamba adhabu ya kifo kwa wauaji ni lazima vivyo hivyo kifungu cha 39(2)(d) kinatakiwa kitafsiriwe hivyo hivyo. Adhabu ya uhaini ni kifo na kifo pekee hoja kwamba kunaweza kuwa na hukumu nyingine ni upotoshaji na inashangaza sana kama itatoka kwa watu wanaojitanabaisha kuwa ni wanasheria.

Adhabu unategenea toleo la sheria lililotumika kwenye charge sheet.

Penal code ya 2022 iliyotumika kwenye hati ya Lissu inatumia maneno "shall be liable to death". Hapa jaji anayo hiari ya kutaja adhabu iliyo ndogo kuliko kifo. Case laws nyingi zinasema hivyo. Hata Jaji Ndunguru alisema hivyo mahakamani majuzi.


Lakini penal code toleo la 2023 imeondoa neno "liable" na kusema kila mhaini LAZIMA anyingwe. Hii haimhusu issu.

So, ikiwa Lissu atatiwa hatiani Kesho, jambi ambalo ni most unlikely in the eyes of law, sio lazima tutarajie hukumu ya kifo.
 
Adhabu unategenea toleo la sheria lililotumika kwenye charge sheet.

Penal code ya 2022 iliyotumika kwenye hati ya Lissu inatumia maneno "shall be liable to death". Hapa jaji anayo hiari ya kutaja adhabu iliyo ndogo kuliko kifo. Case laws nyingi zinasema hivyo. Hata Jaji Ndunguru alisema hivyo mahakamani majuzi.


Lakini penal code toleo la 2023 imeondoa neno "liable" na kusema kila mhaini LAZIMA anyingwe. Hii haimhusu issu.

So, ikiwa Lissu atatiwa hatiani Kesho, jambi ambalo ni most unlikely in the eyes of law, sio lazima tutarajie hukumu ya kifo.

..kwanini kesi ya uhaini iliyofunguliwa 2025 itumie penal code ya 2022 wakati tayari tunayo penal code ya 2023?
 
..kwanini kesi ya uhaini iliyofunguliwa 2025 itumie penal code ya 2022 wakati tayari tunayo penal code ya 2023?

Urafiti mdogo umeonyesha kuwa kuna msingi wa kisheria mahali fulani, kama ninavyoeleza hapa chini.

Marekebisho kutoka "shall be liable on conviction to suffer death" kwenda "shall be sentenced to death" yalifanyika tarehe 31 Desemba 2023, sio kupitia mabadiliko ya sheria bungeni.

Lissu alishatkiwa 10 April 2025 kwa kosa alilotenda tarehe 03 April 2025.

Lakini hati ya mashtaka inataja sheria toleo la 2022.

Kwa nini?
Hata hivyo, kiufundi na kisheria, mabadiliko haya hayakuletwa na sheria mpya iliyotungwa bungeni mwaka 2023, bali ni matokeo ya mambo mawili makuu:

1. Uoanishaji wa Kisaria (Alignment): Tangu zamani, Kifungu cha 197 cha Kanuni ya Adhabu (kinachohusu kosa la Mauaji) kimekuwa kikitumia maneno ya lazima: "shall be sentenced to death". Wakati wa mapitio ya vitabu vya sheria mwishoni mwa mwaka 2023, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilifanya uoanishaji wa lugha (textual alignment) ili makosa yote mawili yanayobeba adhabu ya kifo nchini Tanzania (Mauaji na Uhaini) yatumie lugha inayofanana na yenye msisitizo uleule.

2. Kazi ya Kamati ya Mapitio ya Sheria: Kazi ya matoleo yaliyorejelewa (Revised Editions - R.E.) ni kusafisha lugha na kuondoa mikanganyiko ya maneno. Katika toleo la R.E. 2022, neno "liable" lilionekana kuleta mkanganyiko wa kiwewe kama adhabu hiyo ni ya hiari au ya lazima, jambo ambalo lilinyofolewa rasmi tarehe 31 Desemba 2023 ili kufunga mjadala na kuifanya adhabu hiyo kuwa ya lazima kabisa (mandatory).

Hivyo, Mabadiliko haya ya tarehe 31 Desemba 2023 ndio maana hayapaswi kusimamia kesi ya Tundu Lissu, kwa kuwa hayakutokana na sheria mpya ya 2023.

Wanasheria wataongezea....
 
Hakuna mtu aliwahi kuhukumiwa kifo kisha akanyongwa hapa Tanzania.
1994: Kisage Kamfitiye, Hamadi Kamfitiye, Elias Mwaluko, Juma Athman, Lazaro Lukilangaro, Iddi Koch Sasha, Colonel Dominic Nshimanyi, and Zazi Matayo. Inasemekana hawa ndio walikuwa wa mwisho kunyongwa. Waliofuata waliogopa kuidhinisha kutokana na sababu za kiimani, wanaamini ni jukumu la Mungu wa Mbinguni.
 
Back
Top Bottom