lord atkin
JF-Expert Member
- Sep 30, 2018
- 260
- 929
Nimekuwa nikiona mjadala kuhusu adhabu ya uhaini hasa kwa vifungu alivyotuhumiwa navyo Tundu Lissu. Kumekuwa na upande ambao umekuwa ukisema adhabu stahiki si lazima iwe kifo lakini wapo na hasa (Tundu Lissu mwenyewe) kuwa kisheria ni lazima adhabu iwe kifo.
Nimechukua muda wangu kutafuta na kusoma kwa kina kanuni za utoaji hukumu za majaji na mahakimu wa Tanzania yaani "Tanzania Sentencing Guidelines of 2023". Baada ya kusoma hasa ukurasa wa 8, 9 na 10 nimejiridhisha kwamba kwa mujibu wa kifungu alichoshitakiwa nacho Tundu Lissu kama akikutwa na hatia adhabu ya kifo ndiyo adhabu pekee stahiki.
Kanuni hizi zinaeleza kwamba pale ambapo kifungu cha sheria kimetumia kauli "... shall be sentenced to death" basi hapo Jaji hana chaguo zaidi ya kutoa adhabu ya kifo. Sasa ukisoma kifungu alichoshitakiwa nacho Tundu Lissu yaani kifungu cha Penal Code cha 39(2)(d) kimetumia maneno "... shall be sentenced to death" hivyo hukumu ya kifo ni ya lazima.
Aina hii ya uandishi utaiona katika kifungu cha 197 cha Penal Code ambacho pia kinatoa adhabu ya kifo kwa kosa la mauaji ya kukusudia (murder) ambacho nacho kinasema nanukuu:
"197. A person convicted of murder shall be sentenced to death.".
Kama kifungu hiki cha murder kinatafsiriwa kwamba adhabu ya kifo kwa wauaji ni lazima vivyo hivyo kifungu cha 39(2)(d) kinatakiwa kitafsiriwe hivyo hivyo. Adhabu ya uhaini ni kifo na kifo pekee hoja kwamba kunaweza kuwa na hukumu nyingine ni upotoshaji na inashangaza sana kama itatoka kwa watu wanaojitanabaisha kuwa ni wanasheria.