Adhabu ya Kunyonga Hadi Kufa imepitwa na wakati?

Nadhani hii inakuwa na manufaa sana kwako sababu kama mtu alimuua ndugu yako kwa mateso au hawa wanaotoa kiungo cha binadamu (au hata rape) inaweza kuacha kovu la maisha kwa mtu ambalo ni mateso kuliko hata kifo..., nadhani watu kama hawa kupewa instant kifo inakuwa ni kama wameget off lightly

Wacha wa get off lightly, mimi sitaki kumuona wala kujua kuwa yupo. Na yeye aende zake aondoke duniani, ni hilo tu


Kifungo cha maisha apewe kwa kunisikiliza mimi niliofiwa, baada ya kwua tayari kulipa fidia kubwa sana.
 
"Why do we Kill People who Kill People to Show that Killing People is Wrong ?"​

Je ni sawa kuwa na Hukumu ya Kifo?
Baada ya yule Chizi wa Norway kuua kadamnasi ya watu (ukizingatia Norway life Sentence ni limited kwa miaka 21 tu) Je ni muhimu kuwa na hukumu ya kifo? Ni nini hasa faida ya hukumu ya kifo?

Je hukumu ya kifo inafanya watu waogope kutenda maovu kwahiyo ni njia nzuri au ni kuonyesha hata sisi hatuna tofauti na waliofanya hayo maovu?

I can argue kwamba huenda hukumu ya kifo ni adhabu rahisi sababu badala ya kumfanya mtu ku-suffer kwa kosa lake, tunampumzisha...Je sio vema kumfunga mtu maisha na kumfanyisha kazi ngumu kwa maisha yake yaliyobaki na kila alichonacho au atakachokitengeneza kiende kwa wale aliowatenda....

What do you think?.....
Binadam ni myama kama wanyama wengine. Tofauti yetu kubwa na wanyama ni kuwa tuna kitu cha ziada (Utu) yaani kutambua mazuri na mabaya, ambacho wenzetu hawana.

Hukumu ya kifo itamhusu yule aliyeuwa kwa makusudi na (si katika wale waliouwa kwa kujikinga wasiuwawe na majambazi), kwa kuwa utu wake umemtoka. Binadam akifikia hatua hii anakuwa amepoteza sifa ya kuwa 'mtu' kwa hivyo hastahili tena kuishi na 'watu' iwe kifungoni au uraiani. Anastahili kuuliwa, sio kama ndio adhabu kwa maana asikie uchungu wa kufa au kuwaliwaza wale ndugu wa aliyeuliwa bila hatia.

Hapana sio kwa sababu hizo, bali ni kwa kuwa hana sifa ya 'utu' kawa myama tu, anaweza akasababisha madhara makubwa zaidi.
 
Hii issue ni ngumu sana, mara nyingine huwa nakaa nafikiria naona kama adhabu ya kifo sio nzuri, kwa sababu mhusika anaponyongwa kimsingi waliodhurika na matendo yake hawapati chochote na yeye pengine anaweza asipate nafasi ya kujifunza na kujuta kwamba nilichokifanya hakikuwa sawa, lakini mara nyingine unafikiri unaona kuna watu akili zao ni mboovu na adhabu yao ni hiyo hamna kitu kingine, mfano majambazi wanaovamia na kuua labda familia nzima watu kama hao unadhani utawafanyaje?
ni thahiri kua binadamu wa kawaida atafikiri km ww mi niongoze jambo moja biblia inasema ukiuwa kwa upanga nawe utauwawa kwa upanga hiyvo kuua kwa kusudia,kwa nia ovu(malice aforethought) ni sawa mtu kupewa athabu ya kifo cha msingi maadili ya sheria yazingatiwe ili kuwe na justice.
 
Adhabu ya kunyongwa sio haki kabisa.
Hao wafungwa wangewezwa kutumikishwa kazi mbali mbali hadi mauti yatakapowakuta.
 
Unamaanisha kwamba mtu akajisingizia mwenyewe kwamba ameuwa ili kumuokoa mtu mwingine? Kama kuna kesi kama hizo, ambazo ni nadra sana, kwa maslahi ya umma mimi sioni tatizo. Maana, hata kwenye vita kuna wapambe ambao wanaweza kujitokeza kukinga vifua vyao ili risasi isimpate kamanda au kiongozi wao wanaomlinda. Huwezi kusema askari wa upande mwingine wasubiri kwanza hadi huyu aliejitokeza aondoke.

My excuses for not formulating my thoughts the way i should have. Nilichomaanisha ni mtu asiye na hatia kujifanya yeye ndiye mtenda kosa ili mtenda kosa halisi asikamatwe. Katika bandiko lako limoja ulisema tunaweza kuwa na uhakika wa asilimia 100 kama mtu akiungama kwamba yeye ndiye aliyetenda kosa. Basi nilijibu kwamba hata hapo hatuwezi kuwa na hakika maana mtu anaweza kudai ni mtenda kosa akidanganya.

Uwezekano mdogo kama huo upo pia hata katika makosa mengine yasiyohitaji adhabu ya kifo. Kwamba, mtu anaweza kufungwa maisha kwa kosa ambalo hakulifanya. Tukufuata maoni yako inabidi hata adhabu ya kifungo cha maisha au kifungo chochote isitolewe maana hamna uwezekano wa kuthibitisha mashitaka asilimia mia moja.

Maoni yako inaonekana kuwa kwamba ni bora adhabu ya kifo iendelee kuwepo ijapokuwa kuna uwezekano uhai wa watu wasio na hatia watatolewa lengo hilo litimizwe. Inamaanisha wenye bahati mbaya ya kuuawa ingawa si wahalifu watalazimishwa kutoa uhai wao ili mradi tu waliopenda waathirika wa mauaji waweze kuwalipiza kisasi wauaji kupitia adhabu ya kifo.
Should I conclude kwamba kisasi kina thamani kubwa kuliko uhai wa mtu asiye na hatia kwako?
Kwa sababu kumhukumu mtu adhabu ya kifo ni taratibu ghali sana na bado hatujui kwa hakika kama uwepo wa adhabu ya kifo inapunguza kiwango cha uhalifu, kisasi ndicho sababu thabiti pekee inayobakia kuhalilisha ile adhabu.

Ni kweli kwamba kufuatana na mantiki yangu tunapaswa kujiuliza kama kutolewa kwa adhabu ya kifungo (au adhabu yo yote) ni sawa au la. To be honest, ni suala ambalo bado natafakari juu lake.
Lakini tofauti ni kwamba, tunapozungumzia adhabu ya kifo, swali linaloibuka ni: "Je, ipi ina thamani kubwa kuliko nyingine: kisasi au uhai wa mtu asiye na hatia?". Ilhali tukizungumzia adhabu ya kifungo, kinachojadiliwa ni "ipi ni muhimu zaidi: freedom au security?". Uhuru na usalama wote wawili ni maadili yanayothaminiwa sana na watu, ndio maana kuchagua moja juu ya nyingine ni vigumu sana kuliko kuchagua baina ya kisasi na uhai (ambao nina karibu uhakika watu waliowengi watauchagua ukiwauliza. Binafsi nawaunga mkono watu hao).
 
what i can arque is , haijapitwa na wakati ila tu kwa namna inavyo tendeka kwasasa is better to deleted into our law books. no meaning of killings while you dont want to be killed..... good punishment is that, killer gets sufferance of his act in jail for life.
 
hakuna faida ya adhabu ya kifo ila hukumu ya kumnyonga mtu inatakiwa kusainiwa na rais lakin hawafanyi hivyo kutokana na haki za binadamu na utu pia ni bora wafungwe maisha na kazi ngumu
 
Yes, he could go out and kill someone else! and Yes, the pain and memories could not be measured. I speak only with humanity, which has not been tested. But let be no law which ends human life, but let be laws which limits enjoyment to social life. In such the loved one should heal and maybe came to term with their loss - the fate of the killer should be imprisonment on their mercy and custodion of state.
 
Kwangu mimi naungana na Marehemu Jaji Mwalusanya Kwenye kesi ya Daudi Pete V. Republic, aliyeamua kuwa adhabu ya kifo ni ya kikatili (barbaric) and it infringes haki ya kuishi, ingawa mauaji yanakuwa yametokea inatakiwa iangaliwe njia mbadala maana two wrongs cannot make it to be right, kuna kesi zimetokea hasa ulaya na Marekani ambapo watu walihukumiwa kifo, wakanyongwa baada ya muda kupita ikaonekana hawakuhusika.
 
Mimi nafikiri imepitwa na wakati. Hizi sheria tulizokopa kutoka kwa Wakoloni wetu kwa sasa zimekosa mashiko. Mimi naamini kifungo cha maisha without possibility of parole na kazi ngumu ni adhabu kubwa na inatosha kumfanya mtu kujutia kosa lake na hata kwa wale waliopoteza ndugu yao watarizika. Amini nawaambia hakuna kitu kinauma kama kukosa uhuru.
 
Kwa nchi zingine hyo inasaida kupunguza crime rate. kama hukumu ya kifo hamna basi walala hoi wote watafanya makosa ili wahukumiwe wapte kila kitu bure. ukiangali jail zingine kama za marekani yaani maisha mfungwa anayoishi ni mazuri kuliko mtu anayefnya biasha ra nyanya kariakoo. so the only way they can control people not to commit crime is to make the fear the punishment. believe me watu huogopa kifo sana no one want to die unless you are insane and you cant distinguish between living and death. so nadhani adhabu ya kifoo ni sahihi sana especially kwa watu walio na roho za kinyama. we don't need people who act like animals.

ukisoma cases za nchi tofauti tofauti utakuta kwamba watu wana behave ajabu kweli mwingine anaamua tu kuwa curious na kuanza kuuwa watu bila sababu simply because they want to be famous or something like that crazy. watu kama wale wanao wauwa albino i dont see the reason why they deserve to live. wewe kama mtu anaamua kumkata mwanadamu mwingine what do you expect. huyo anatakiwa aaondolewe na yeye mara moja isitoshe inapunguza population magerezani au sio.
 
Uwepo wa hukumu ya kifo, achilia mbali utekelezwaji wake au la, ni tishio tosha la kuwaogopesha wengine kutenda kosa la mauaji. Tukisema hukumu ya kifo ifutwe kabisa ktk sheria nauhakika mauaji yataongezeka. Mtu atamuua mwenzie akiweka akichwani kwamba adhabu yake ni kutokua na uhuru wa kuzurura mitaani TU.

Ataendelea kuonana na ndugu na jamaa kwasbb watakua wakimtembelea jela. Kifo kinatisha sana jamani kuliko adhabu yeyote ile. Naona adhabu ya kifo iwepo, itawaogopesha sana wenye fikra za mauaji kwasbb mbali na maumivu yake pia atafikiria kuwa hatopata kuwaona ndugu na jamaa zake milele.
 
wananzengo naandika research yangu ya kumaliza degree yangu ya sheria ya chuo kikuu cha dar es salaam kuhusu mambo ya unconstitutionality of death penalty and the current penal laws, mwenye materilas anisaidie,wenu kimamii
 
hapana,japo mungu hatki,ila mbona china hakuna hujuma?hakuna rushwa za wazwaz kama hapa?
mtu ukijua kuwa nikla rushwa kifo changu,nani angeiba hela za ep,au mikataba mibovu?uswatete
 
kuna baadhi ya sheria zinadai ukihukumu kifo ile inafanya jamii km katishio vile watu wataogopa.bt ki human right na ki humanitarian law sio ishu kbs,kiuhalisia nadhan c dawa ya kutibu tatzo.
 
Ukiniulia mtoto wangu au baba yangu basi na wewe hustahili tena kuishi!

Kama unataka kuishi basi anza kulipia oksijeni na bei nitaamua mwenyewe.
 
Imepitwa na wakati iwapo nchi tayari imekwisha kustaarabika kwa maana ya kila raia kufuata sheria na taratibu kama impasavyo. Kwa nchi zenye matatizo mengi na makubwa kiuwajibikaji haistahili kuondolewa. Lakini hofu kubwa pia ni namna ya matumizi yake kwa sababu kama itakuwa imejikita katika mikono ya kidhalimu na kifedhuli basi itatolewa kidhalimu na kifedhuli ili kudumisha udhalimu na ufedhuli. Kwa hilo haina budi kupitwa na wakati.
 
Hukumu ya kifo sio adhabu kimantiki,lakini ni njia ya kuondoa binadam ambao hawatakiwi katika jamii ya watu wastaarabu. watu wanao ua wenzao,wabakaji na watesaji wa watoto,jamii iliyostarabika haiwahitaji,kuwafunga maisha ni kuwaadhibu hata wale waliotendewa unyama huo kwa kuwatoza kodi ya kuwatunza wahalifu wao.

Lakini akiuawa ukurasa wa tukio na mtenda hufungwa na wala kodi ya watu wema haitatumika kuhudumia wahalifu. ningeshauri makosa yanayohusu kuondoa uhai wa mwingine kwa dhamira hukumu yake iwe ni kifo tu kwa mtenda,lakini makosa ya kisiasa na yale ambayo hayahusiani na kukatisha uhai kwa mwingine kwa kudhamiria yasiwemo kwenye kustahili hukumu ya kifo kwa mtenda.

WAUAJI HAWASTAHILI KUWEPO NA KUHUDUMIWA NA JAMII,WAUAWE KWA NJIA YOYOTE. kunyongwa,kupigwa risasi, kupewa sumu,kwa umeme n.k
 
Back
Top Bottom