Adhabu ya Bakora Yaahirishwa Hadi Baada ya Mfungo wa Ramadhan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adhabu ya Bakora Yaahirishwa Hadi Baada ya Mfungo wa Ramadhan

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Aug 26, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kartika Sari Dewi Shukarno Monday, August 24, 2009 5:29 PM
  Adhabu ya kuchapwa bakora sita iliyokuwa ikimkabili mrembo wa vivazi wa Malaysia ambaye alikamatwa akinywa pombe hadharani imeahirishwa hadi baada ya kuisha kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan. Maafisa wa Malaysia walisema kwamba adhabu ya bakora sita iliyokuwa ikimkabili mrembo wa vivazi wa Malaysia, Kartika Sari Dewi Shukarno imeahirishwa hadi baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan.

  Awali Kartika ambaye ni muislamu alitakiwa kuingizwa jela leo jumatatu na kuchapwa bakora sita ndani ya wiki wiki kama adhabu ya kosa lake la kunywa pombe hadharani.

  Hata hivyo, Mohamad Sahfri Abdul Aziz, mwakilishi wa serikali katika masuala ya dini alisema kwamba adhabu hiyo itatelekezwa baada ya kuisha kwa mwezi mtukufu wa ramadhan. Mwezi wa ramadhan ulioanza jumamosi unaisha katikati ya mwezi ujao wa tisa.

  Mwakilishi huyo alisema kwamba uamuzi wa kuahirisha adhabu hiyo umechukuliwa baada ya mashauri yaliyotolewa na ofisi ya mwanasheria wa serikali.

  Kartika, 32, alipatikana na hatia ya kunywa pombe hadharani katika klabu ya starehe iliyopo kwenye hoteli moja iliyopo mashariki mwa mji wa Pahang mwaka jana.

  Malaysia ina mifumo miwili ya sheria. Mfumo mmoja ni wa kawaida na mfumo mwingine unafuata sheria za kiislamu kwaajili ya waislamu wanaokiuka misingi ya kiislamu.

  Raia wa Malaysia wenye asili ya China na India ambao wengi wao si waislamu wao wako huru kunywa pombe muda wowote bila kubughudhiwa.

  Hali ni tofauti kwa raia wa Malaysia ambao ni waislamu kwani matendo yao yoyote yanayokiuka misingi ya kiislamu huamriwa na mahakama za sharia za kiislamu.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  upuuuuuuzi tu.nchi zingine bana!
   
Loading...