Katika tabia zote mimi huwa nachukizwa na tabia za uongo, huyu mleta mada ni mzushi, alichokisema Rage ni kwamba hakujuwa kama shati lake lilifunuka, na yeye kila siku akitoka nyumbani kwake bastola yake huwa ni lazima iwe kiunoni. Ila kuna kitu nimegunduwa yale mahojiano waliyarekodi hayakuwa live, kuna kauli Rage alikuwa ameanza kuongea hawa wapumbavu Kibonde&company wamekata yale mahojiano maana yangeibuwa mjadala mkubwa zaidi. Lakini wenye akili tumeshajuwa alitaka kuongea nini. Ilikuwa ni kauli ya kudefence zaidi kitendo chake lakini ni kauli yenye madhara makubwa sana kwa chama chake, maana ccm inahubiri Tanzania tuna amani huku viongozi wake wanapanda na silaha majukwaani.