ACT-Tanzania mwiba mkali kwa CHADEMA

ACT-Tanzania mwiba mkali kwa CHADEMA

Mwl. Kaijage

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
216
Reaction score
214
Poleni chadema na Hongereni ACT.
Baada ya chama cha Chadema kushindwa
propaganda ya kumchafua Mzalendo
namba moja Zitto zuberi Kabwe kuwa
anatumiwa na ccm,waliamua kuwatumia
waandishi wa Tanzania Daima pamoja na
wazee mashuhuri ili kumbakisha chadema.
Hofu kubwa ya chadema ni kuhofia endapo
Zitto atajiunga na chama cha Kizalendo cha
ACT,basi itakuwa mwisho wa chadema.
Pamoja na jitihada za kumbakisha chadema
Zitto alitoa Masharti Magumu ambayo
chadema walishindwa kuyatekeleza.
Moja ya sharti la Zitto kubaki chadema ni
wale waliomzushia tuhuma kuwa
anatumiwa kuhujumu chadema basi warudi
kwenye vyombo vya habari na kukanusha
maneno yao(Sharti gumu)
Sharti lingine ni kuwa yupo tayari kubaki
chadema endapo tu wapiganaji wake
watarudishwa kwenye chama,(Prof
Mkumbo,Mwigamba ,na wengine wengi)
Chadema baada ya kushindwa
kumshawishi,wakaja na plan B.
Katika plan hii waliamua kumrubuni
Mwenyekiti wa muda Bw.Kadawi Limbu ili
asikubali kuitisha uchaguzi wa chama na
kisha akiendeshe chama kwa maelekezo
toka makao makuu ya chadema (Ufipa)
Limbu kwa kushawishiwa na pesa kidogo
zilizoletwa na mtu anaeitwa Saidi
Kubenea,akaapa kuwashughulikia wote
wanaodai uchaguzi ndani ya chama
Akamfukuza Katibu Mkuu wa chama na
viongozi wandamizi wa chama bila kufuata
katiba wala taratibu za chama.
Lengo ni kuhakikisha chama
kinasambaratika ili kumkatisha tamaa Zitto
Kabwe ambae muda wowote atatua ACT
kujenga demokrasia kwa vitendo.
Hatimae Plan B nayo imeshindwa,Maana
mission kupewa mtu mwenye shule ya
Form four (Kubenea)kukabiliana na Think
tank za ACT kama Prof Mkumbo,Zitto na
Mwigamba ni sawa na kumtisha kuku ndoo
ya maji.
Kubenea kumshinda Prof Mkumbo ni sawa
na Kabati kuangushwa na Mende.
Nilitegemea tu kuwa plan B nayo
ingeshindwa maana akili ndogo haiwezi
kuishinda akili kubwa.
Kushindwa kwa mipango hiyo dhidi za Zitto
Kabwe ,kumewagharimu mamilioni ya fedha
chadema ,pamoja na hayo yote chadema
wameibuka na plan C.
Hii nikumwaga pesa kwa wahariri wa
vyombo vya habari ili kuhakikisha habari
chanya za Mzalendo Zitto hazitolewi
kwenye vyombo vya habari.
Lakini pamoja jitihada hizo za chadema
kumhujumu Zitto,lakini Zitto anazidi
kuchanja Mbuga.
Ni katikati ya zengwe hilo ,Zitto alihutubia
mkutani Mkubwa huko mkoani Mtwara kwa
kushirikiana na Mchumi wa Dunia Prof
Lipumba.
Lakin kwa upande wa chama cha ACT-
Tanzania imekuwa neema,chama kimepata
coverage ya kutosha katika vyombo vyote
vya habari.
Chama kimejitangaza bila kutumia
gharama,chakufurahisha nikuwa
wamaoitangaza ACT ni chadema.
Huenda kutokana na uelewa mdogo wa
viongozi wao hawajagumdia kama wanazidi
kuifanya ACT kufahamika mbele ya macho
yawanyonge.
Hapa ndipo unapokubali kuwa chama
kikiwa na viongozi makini kazi ya
kurangaza chama huwa rahisi.
Ni ukweli usiopingika kuwa chadema
ilitangazwa na CCM baada ya kuwa
inasemwa kila ccm walipohutubia.
Pia ni ukweli usiopingika kuwa ACT
inatangazwa na chadema
Hongereni ACT kwa kupata covarage
kwenye vyombo vya habari kwa kutumia
gharama za chadema.
Asanteni chadema kwa kuijenga ACT
kupitia magazeti yenu ya Tanzania Daima
na Mawio.
 
Naamini Zitto mwenyewe anachukizwa na siasa hizi za kishamba zinazofanywa na ACT
 
Last edited by a moderator:
Kwi kwi kwi kwi kwi kwi chama hakina hata viongozi, wanafukuzana wenyewe kwa wenyewe halafu eti kiwe tishio kwa CHADEMA! hahahahahahah lol!!!!! Hamuwezi kuwa tishio hata kwa TLP sembuse CHADEMA lol!!!
 
Mwl.umebaki peke yako,wenzako wanajuta.Chama ni maarufu kuliko majina ya wachama unaowataja.Umaarufu wao umeporomoka kiasi kwamba ushawishi wao hauna nguvu tena.Wajiandae kisaikolojia kwa kuangalia fursa zingine kama kilimo,ufugaji au biashara,siasa basi tena
 
Kama na wewe ni mwalimu basi ni halali watoto wetu wamalize masomo wakiwa vilaza.
 
zitto anaipenda cdm ndo maana kawaomba ccm wa.saidie asifukuzwe..
 
Unaongea utumbo tu wakat zito anajitahid kuomba msamaa ili arud chadema na alisema ameimic sn,
Nakuuliza swal mbona kwenye mikutano yenu zito hajawah kuvaa ngua za ACT? Ni gwanda tu, na unajua ACT kiliundwa kupambana na Chadema ila hamta weza nyie kwa nyie mnasalitiana sasa..
 
Kwa kweli kwa sasa heshima ya kuitwa mwalimu imeshushwa sana na watu kama hawa wakina Kaijage. Au huyu ni mwalimu wa Ujinga?
 
Hao wapiganaji wa Zitto ingependeza kama wangepigania wanyonge wanaodhulumiwa na serikali ya CCM lakini wapiganaji wa kupambana na chama kingine cha upinzani mnachelewesha ukombozi ambao imebakia ncha ndogo kuufikia.
ACT tafakari upya ungeza nguvu kufikia ukombozi haraka.
Mh. Zitto na wapiganaji wako kama walivyoitwa vaa uzalendo na usivue magondwa kwani ukombozi umekaribia.
 
Poleni chadema na Hongereni ACT.
Baada ya chama cha Chadema kushindwa
propaganda ya kumchafua Mzalendo
namba moja Zitto zuberi Kabwe kuwa
anatumiwa na ccm,waliamua kuwatumia
waandishi wa Tanzania Daima pamoja na
wazee mashuhuri ili kumbakisha chadema.
Hofu kubwa ya chadema ni kuhofia endapo
Zitto atajiunga na chama cha Kizalendo cha
ACT,basi itakuwa mwisho wa chadema.
Pamoja na jitihada za kumbakisha chadema
Zitto alitoa Masharti Magumu ambayo
chadema walishindwa kuyatekeleza.
Moja ya sharti la Zitto kubaki chadema ni
wale waliomzushia tuhuma kuwa
anatumiwa kuhujumu chadema basi warudi
kwenye vyombo vya habari na kukanusha
maneno yao(Sharti gumu)
Sharti lingine ni kuwa yupo tayari kubaki
chadema endapo tu wapiganaji wake
watarudishwa kwenye chama,(Prof
Mkumbo,Mwigamba ,na wengine wengi)
Chadema baada ya kushindwa
kumshawishi,wakaja na plan B.
Katika plan hii waliamua kumrubuni
Mwenyekiti wa muda Bw.Kadawi Limbu ili
asikubali kuitisha uchaguzi wa chama na
kisha akiendeshe chama kwa maelekezo
toka makao makuu ya chadema (Ufipa)
Limbu kwa kushawishiwa na pesa kidogo
zilizoletwa na mtu anaeitwa Saidi
Kubenea,akaapa kuwashughulikia wote
wanaodai uchaguzi ndani ya chama
Akamfukuza Katibu Mkuu wa chama na
viongozi wandamizi wa chama bila kufuata
katiba wala taratibu za chama.
Lengo ni kuhakikisha chama
kinasambaratika ili kumkatisha tamaa Zitto
Kabwe ambae muda wowote atatua ACT
kujenga demokrasia kwa vitendo.
Hatimae Plan B nayo imeshindwa,Maana
mission kupewa mtu mwenye shule ya
Form four (Kubenea)kukabiliana na Think
tank za ACT kama Prof Mkumbo,Zitto na
Mwigamba ni sawa na kumtisha kuku ndoo
ya maji.
Kubenea kumshinda Prof Mkumbo ni sawa
na Kabati kuangushwa na Mende.
Nilitegemea tu kuwa plan B nayo
ingeshindwa maana akili ndogo haiwezi
kuishinda akili kubwa.
Kushindwa kwa mipango hiyo dhidi za Zitto
Kabwe ,kumewagharimu mamilioni ya fedha
chadema ,pamoja na hayo yote chadema
wameibuka na plan C.
Hii nikumwaga pesa kwa wahariri wa
vyombo vya habari ili kuhakikisha habari
chanya za Mzalendo Zitto hazitolewi
kwenye vyombo vya habari.
Lakini pamoja jitihada hizo za chadema
kumhujumu Zitto,lakini Zitto anazidi
kuchanja Mbuga.
Ni katikati ya zengwe hilo ,Zitto alihutubia
mkutani Mkubwa huko mkoani Mtwara kwa
kushirikiana na Mchumi wa Dunia Prof
Lipumba.
Lakin kwa upande wa chama cha ACT-
Tanzania imekuwa neema,chama kimepata
coverage ya kutosha katika vyombo vyote
vya habari.
Chama kimejitangaza bila kutumia
gharama,chakufurahisha nikuwa
wamaoitangaza ACT ni chadema.
Huenda kutokana na uelewa mdogo wa
viongozi wao hawajagumdia kama wanazidi
kuifanya ACT kufahamika mbele ya macho
yawanyonge.
Hapa ndipo unapokubali kuwa chama
kikiwa na viongozi makini kazi ya
kurangaza chama huwa rahisi.
Ni ukweli usiopingika kuwa chadema
ilitangazwa na CCM baada ya kuwa
inasemwa kila ccm walipohutubia.
Pia ni ukweli usiopingika kuwa ACT
inatangazwa na chadema
Hongereni ACT kwa kupata covarage
kwenye vyombo vya habari kwa kutumia
gharama za chadema.
Asanteni chadema kwa kuijenga ACT
kupitia magazeti yenu ya Tanzania Daima
na Mawio.

unajitahidi kumpamba zitto si aende act kwasasa haitajiki chadema.
 
Mwalimu kichaa huyu, Unadhalilisha taaluma ya Ualimu, wewe ni mfano wa waalimu wanao baka na kulawiti watoto mashuleni, Kila siku kazi kutunga Propaganda za Kike
 
Ingekuwa vizuri kama ungemshauri huyo msaliti mwenzio afute kesi ili ajiunge kwenye hilo genge lenu. Hivi kati yake huyo aliyefungua kesi na cdm,ni nani anayemuhitaji mwingine? Cdm hatumuhitaji na hakuna mtu anayefikiria kumuhitaji,chama limesheheni halihitaji mamluki na wasaliti. Kipimo ni chaguzi za serikali za mitaa, tumekisimamia chama na kushinda maeneo muhimu kwa nguvu za makamanda wa chini mfano ni hapa magu.
 
Wasaliti ni wasaliti tu! Nasisitiza tena ACT siyo chama cha siasa bali ni kikundi cha wasaliti.

Watu kama huyo mwalimu Kaijage anadhani akimtaja sana Zitto kwenye ACT yao ndo itapata wateja. Zitto ni ccm na ndiyo maana hiyo ACT ni tawi la CCM. Hongereni. Endeleeni na kusalitiana na kufukuzana.
 
kaijage siyo mwl. zitto kawatelekeza. kumbuka mgao wa kwanza mlianza biashara ya ndagaa. pesa ilivoisha mkamdanganya zzk kuwa mna mvuto bado akawatumia gari, akawanunulia spika na jenereta. mkaambulia mitaa 2. sasa tunanasubili mgombanie spika. zzk ashindane na mrema au dovutwa na si mbowe na slaa. awa ni level ingine
 
Kama na wewe ni mwalimu basi ni halali watoto wetu wamalize masomo wakiwa vilaza.

Umeonae..! huyu mwailm cjui anawafundisha nini watoto kwan yy mwenyew hajielewi, badala umwage hizo propaganda zako kwa chama cha mafisad unazileta kwenye chama makin kama CHADEMA, jipange upya ila s kwa hoja za kitoto km hizo.
 
Kwi kwi kwi kwi kwi kwi chama hakina hata viongozi, wanafukuzana wenyewe kwa wenyewe halafu eti kiwe tishio kwa CHADEMA! hahahahahahah lol!!!!! Hamuwezi kuwa tishio hata kwa TLP sembuse CHADEMA lol!!!
Sioni tofauti yake na nape.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom