ACT-Tanzania mwiba mkali kwa CHADEMA

ACT-Tanzania mwiba mkali kwa CHADEMA

Nilipost uzi humu kuwa ACT wanaweza kuwa na madhara kwa chadema na UKAWA zaidi kuliko CCM fitna zao zitaongezeka kadiri siku zinavosegea na migogoro yao inavopungua . Unaweza kutambua kinyongo walichonacho wale waliofurumushwa chadema watakuja katika sura nyingi ikiwemo kutumia vyama vingine kama ACT hakukaliki mfano kuna vichama vya Mzirai wakina Dovutwa.Dharau ndio itawaponza mambo yatakuwa ya kustukiza septemba ama august kama mrema alivowastukizia CCM
 
I think mngefanya juhudi kugombana na CCM MNGEKUWA MNAFANYA JAMBO LA MAANA SANA KWA WATANZANIA

KIPINDI HIKI AMBACHO WAPINZANI WANAJARIBU KUZIKA TOFAUTI ZAO NA KUUNGANISHA MAWAZO YAO NA KUWEKA UTAIFA MBELE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU HUU UNAOKUJA MIEZ MICHACHE IJAYO KISHA NYINYI MNAKUJA KUTENGENEZA MIGOGORO NA WAPINZANI WENZENU NI ISHARA YA UCHAWI NA USHIRIKINA

MSIGEUKE CHANUO NYINYI,,,,KAZI ZENU NI MBILI TUH,,KUCHANA NYWELEE NA KUSUKA NYWELEE

MSIWE WAANGAA
 
mr bean.jpg
 
I think mngefanya juhudi kugombana na CCM MNGEKUWA MNAFANYA JAMBO LA MAANA SANA KWA WATANZANIAKIPINDI HIKI AMBACHO WAPINZANI WANAJARIBU KUZIKA TOFAUTI ZAO NA KUUNGANISHA MAWAZO YAO NA KUWEKA UTAIFA MBELE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU HUU UNAOKUJA MIEZ MICHACHE IJAYO KISHA NYINYI MNAKUJA KUTENGENEZA MIGOGORO NA WAPINZANI WENZENU NI ISHARA YA UCHAWI NA USHIRIKINAMSIGEUKE CHANUO NYINYI,,,,KAZI ZENU NI MBILI TUH,,KUCHANA NYWELEE NA KUSUKA NYWELEEMSIWE WAANGAA
hao wanawanga mchana Mukulu! Hadi nikajiuliza hivi hawa act adui yao mkubwa ni Ukawa kuliko ccm! Badala kushirikiana kuua huyu ng'ombe na kugawane nyama wao wanaleta ya mwana kuleta!
 
Namshukuru sana Mungu maana wanangu hawasomi shule za kata , HIVI HUYU NAYE NI MWALIMU ?
 
Yaani kweli watanzania tuna safari ndefu kwenye suala zima la ukombozi wa nchi toka kwa mkoloni mweusi,watu wanajiimarisha kuitokomeza ccm na majambazi yake eti kuna chama kinaanzishwa kwa misingi ya kinafiki kuja kupambana na chadema,jamani?kweli?hii inaonyesha watanzania safari yetu bado ni ndefu sana
 
wakati sisi wengine tukifikiria namna na mbinu za kulikomboa taifa kuna watu wao wanafikiria kutukwamisha tusikomboe hili taifa,kwa kifupi wao ni mamluki..yaani wametumwa kuharibu upinzani,shenzi taipu zenu,bora mkafie mbali uko na uzandiki wenu!
 
Poleni chadema na Hongereni ACT.
Baada ya chama cha Chadema kushindwa
propaganda ya kumchafua Mzalendo
namba moja Zitto zuberi Kabwe kuwa
anatumiwa na ccm,waliamua kuwatumia
waandishi wa Tanzania Daima pamoja na
wazee mashuhuri ili kumbakisha chadema.
Hofu kubwa ya chadema ni kuhofia endapo
Zitto atajiunga na chama cha Kizalendo cha
ACT,basi itakuwa mwisho wa chadema.
Pamoja na jitihada za kumbakisha chadema
Zitto alitoa Masharti Magumu ambayo
chadema walishindwa kuyatekeleza.
Moja ya sharti la Zitto kubaki chadema ni
wale waliomzushia tuhuma kuwa
anatumiwa kuhujumu chadema basi warudi
kwenye vyombo vya habari na kukanusha
maneno yao(Sharti gumu)
Sharti lingine ni kuwa yupo tayari kubaki
chadema endapo tu wapiganaji wake
watarudishwa kwenye chama,(Prof
Mkumbo,Mwigamba ,na wengine wengi)
Chadema baada ya kushindwa
kumshawishi,wakaja na plan B.
Katika plan hii waliamua kumrubuni
Mwenyekiti wa muda Bw.Kadawi Limbu ili
asikubali kuitisha uchaguzi wa chama na
kisha akiendeshe chama kwa maelekezo
toka makao makuu ya chadema (Ufipa)
Limbu kwa kushawishiwa na pesa kidogo
zilizoletwa na mtu anaeitwa Saidi
Kubenea,akaapa kuwashughulikia wote
wanaodai uchaguzi ndani ya chama
Akamfukuza Katibu Mkuu wa chama na
viongozi wandamizi wa chama bila kufuata
katiba wala taratibu za chama.
Lengo ni kuhakikisha chama
kinasambaratika ili kumkatisha tamaa Zitto
Kabwe ambae muda wowote atatua ACT
kujenga demokrasia kwa vitendo.
Hatimae Plan B nayo imeshindwa,Maana
mission kupewa mtu mwenye shule ya
Form four (Kubenea)kukabiliana na Think
tank za ACT kama Prof Mkumbo,Zitto na
Mwigamba ni sawa na kumtisha kuku ndoo
ya maji.
Kubenea kumshinda Prof Mkumbo ni sawa
na Kabati kuangushwa na Mende.
Nilitegemea tu kuwa plan B nayo
ingeshindwa maana akili ndogo haiwezi
kuishinda akili kubwa.
Kushindwa kwa mipango hiyo dhidi za Zitto
Kabwe ,kumewagharimu mamilioni ya fedha
chadema ,pamoja na hayo yote chadema
wameibuka na plan C.
Hii nikumwaga pesa kwa wahariri wa
vyombo vya habari ili kuhakikisha habari
chanya za Mzalendo Zitto hazitolewi
kwenye vyombo vya habari.
Lakini pamoja jitihada hizo za chadema
kumhujumu Zitto,lakini Zitto anazidi
kuchanja Mbuga.
Ni katikati ya zengwe hilo ,Zitto alihutubia
mkutani Mkubwa huko mkoani Mtwara kwa
kushirikiana na Mchumi wa Dunia Prof
Lipumba.
Lakin kwa upande wa chama cha ACT-
Tanzania imekuwa neema,chama kimepata
coverage ya kutosha katika vyombo vyote
vya habari.
Chama kimejitangaza bila kutumia
gharama,chakufurahisha nikuwa
wamaoitangaza ACT ni chadema.
Huenda kutokana na uelewa mdogo wa
viongozi wao hawajagumdia kama wanazidi
kuifanya ACT kufahamika mbele ya macho
yawanyonge.
Hapa ndipo unapokubali kuwa chama
kikiwa na viongozi makini kazi ya
kurangaza chama huwa rahisi.
Ni ukweli usiopingika kuwa chadema
ilitangazwa na CCM baada ya kuwa
inasemwa kila ccm walipohutubia.
Pia ni ukweli usiopingika kuwa ACT
inatangazwa na chadema
Hongereni ACT kwa kupata covarage
kwenye vyombo vya habari kwa kutumia
gharama za chadema.
Asanteni chadema kwa kuijenga ACT
kupitia magazeti yenu ya Tanzania Daima
na Mawio.

Hii ACT unayoizungumzia ni ipi, hii hii au kuna nyingine. ACT ninayoijua mimi iko kwenye migogoro, kinachoendelea sasa hivi ni minyukano. Wengine wanasema ACT inataka kumshitaki Zitto kwa sababu ameshindwa kutimiza ahadi ya kujiunga kwenye chama hicho. Leo ACT hii imekuwa tishio kwa CHADEMA ki vipi. Tishio la CHADEMA ni CCM siyo ACT.
 
ccm ktk mbinu ya
~ divide & rule ~
ktk mfumo wa vyama vingi.

sawa na vita vya panzi furaha kwa kunguru.
 
Hongera sana Mwl Kaijage kwa Makala nzuri,tulikumis sana Jamiiforums maana wewe ni kiboko ya hawa watumwa wa Mtei.
Ukiona mtu anapemda kumtaja mtu ujue anamkosesha raha hivyo usilegeze uzi,wasasambue mpaka wasambaratike.

mimi sasa nipo ACT -TANZANIA

sasa mbona unampongeza na kumkejeli tena?
umesema ukimuona MTU anamsema Sana mwenzake ujue anamnyima usingizi.
which means that Chadema wanawanyima Act usingizi, kila siku act wao ni chadema chadema tu.yaani wao mbaya wao ni chadema wala sio ccm nccr au cuf.
poleni Sana Ccm pamoja na litoto lenu ACT,chadema ni mpango Wa mungu hanuiwezi kirahisi nahisi hivyo.
 
hawa ndio wanao muharibia zitto, kwa uelewa wako mdogo unazani unampamba zitto kumbe unamuharibia
 
Act hawezipambana na chadema aibu unamfumania mkeo unapewa kifinyo unaenda kumuita dadako akusaidie unategemea nini kitatokea kama SI kuolewa wote na wewe mw.kaijage soon tutatangaza wedding yako babako kashindwa we kukuwajana unajitia kuwika kwenye mitandao
chadema hakiongozi nchi ajabu mnapambana na chadema kwa akili ya kawaida mnaonekana mmetumwa na laana yenu ya kutaka kuwacheleweshea watanzania haki Yao mtasambaratika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom