Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Habari za asubuhi ndugu abiria,mimi ni kapteni Bob mazishi.Karibuni katika ndege yetu ya abracadabra airways.Safari yetu ni kuelekea Mwanza,lakini hatuna uhakika wa kufika mwanza,tunaweza kutua sehemu yoyote kaskazini mwa nchi na kama ukiwa na bahati labda tutatua kijijini kwenu.Viwango vyetu vya usalama ni vya mashaka kiasi ambacho hata magaidi wanaogopa kusafiri na sisi.Zaidi ya 50% ya abiria waliosafiri kwa kampuni yetu.walifika makwao salama salmini.Kwa wale abiria wapagani,kwa kusafiri kwa ndege yetu ndo utajua mungu yupo au la.Tunakushauri ujifunge mkanda uliopo kwenye siti yako,kama siti yako haina mkanda,tumia mkanda wako kujishikiza kwenye siti yako.Katika ndege yetu haturuhusu kuvuta sigara hivyo ukiona moshi ujue injini pekee ya ndege yetu imepata hitilafu.Kwa wale abiria watakaokereka na mngurumo wa injini ya ndege yetu,tutaizima injini ili kuondoa kero ya kelele.Safari njema kwenu nyote!