About First Lady In Tanzania

Black BackUp

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
631
1,000
Habari za wakati huu?

Imekua kawaida sana hasa baada ya uchaguzi Mkuu na mpaka kufikia hatua ya kuapishwa kua raisi wa nchi, Wakati akiwa amekabidhiwa nchi punde Mda si mrefu hua wanamfata mkewe popote alipoajiliwa na kumuachisha shughuli aliokua anafanya (ajira yake) pengine kwa kuwaaga wafanyakazi wenzake au lah!

Naomba kufahamu baada ya kuachishwa kazi (ajira) mke wa Raisi (first lady) huwa anapewa kazi gani ya kufanya? na je hua analipwa mshahara Kama raisi anavolipwa? Kama ndio Malipo yake yapoje?

Je, hua ana Ofisi Kama vile makamu/ waziri Mkuu?

Vipi Nssf/ppf yake Kule alipoachishwa kazi anapewa immediately au inaunganishwa Kule anapopelekwa??
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
51,722
2,000
Anaacha kazi ili iwe rahisi kwake kuambatana na rahisi katika ziara pale inapohitajika. Sina uhakika kuhusu malipo.

Ninakumbuka Cherry Blair hakuacha kazi yake kama Jaji wa mahakama kuu mume wake alipokua Waziri Mkuu lakini alipunguza masaa ya kazi.

Aliongengelea pia kuhusu gharama za mavazi na kusema yeye alimudu kujinunulia lakini alipendekeza kuwe na fungu la mavazi ya mke wa PM huko mbele.
 
mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
8,110
2,000
Kama ni mtumishi wa umma anachukua likizo ila mshahara kama kawaida mpaka skistaafu,kama ni house wife kama mama nyerere jibu unalo,kama ni sekta binafsi anaacha kazi,yeye ni msaidizi wa rais anakuwa na mlinzi wake binafsi na wasaidizi,
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,363
2,000
Habari za wakati huu?!!
Imekua kawaida sana hasa baada ya uchaguzi Mkuu na mpaka kufikia hatua ya kuapishwa kua raisi wa nchi, Wakati akiwa amekabidhiwa nchi punde Mda si mrefu hua wanamfata mkewe popote alipoajiliwa na kumuachisha shughuli aliokua anafanya(ajira yake) pengine kwa kuwaaga wafanyakazi wenzake au lah!
Naomba kufahamu baada ya kuachishwa kazi (ajira) mke wa Raisi ( first lady) hua anapewa kazi gani ya kufanya? na je hua analipwa mshahara Kama raisi anavolipwa ?Kama ndio Malipo yake yapoje? Je hua ana Ofisi Kama vile makamu/waziri Mkuu??
Vipi Nssf/ppf yake Kule alipoachishwa kazi anapewa immediately au inaunganishwa Kule anapopelekwa??
Thread imebandikwa saa 7:48 usiku, mi mida hiyo huwa niko dunia nyingine
 
Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
6,457
2,000
Mke wa rais anayo office na fungu kubwa tu kwa kua yeye ni hostess wa wake au waume wa viongozi wanaotembelea nchi.
Kuhusu mafao inategemea njaa yake. Kama ananjaa kubwa anaziomba mapema tu.
Wengi wa wake za Marais huwa wanajiweka bize na charitable organizations Kama Ile ya mama Mkapa EOTF ama Ile ya mke wa Kenyatta. Wa Uganda Ni waziri wa Burundi sijui Kama anajishughulisha na nini zaidi ya tamthilia za Korea.
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,088
2,000
Kama ni mtumishi wa umma anachukua likizo ila mshahara kama kawaida mpaka skistaafu,kama ni house wife kama mama nyerere jibu unalo,kama ni sekta binafsi anaacha kazi,yeye ni msaidizi wa rais anakuwa na mlinzi wake binafsi na wasaidizi,
Mama Nyerere naye ni mwalimu kwa taaluma.
 
Agenda1

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
1,695
2,000
Anaacha kazi ili iwe rahisi kwake kuambatana na rahisi katika ziara pale inapohitajika. Sina uhakika kuhusu malipo.

Ninakumbuka Cherry Blair hakuacha kazi yake kama Jaji wa mahakama kuu mume wake alipokua Waziri Mkuu lakini alipunguza masaa ya kazi.

Aliongengelea pia kuhusu gharama za mavazi na kusema yeye alimudu kujinunulia lakini alipendekeza kuwe na fungu la mavazi ya mke wa PM huko mbele.
Huyo aliasisi ufisadi, ina maana mshahara na marupurupu ya pm hayatoshi kumnunulia mke nguo? jukumu la mme kwa mke ni lipi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom