Sheikh Ponda: Haya ndiyo madai Muhimu ya Waislam...

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Kumekuwepo na Upotoshaji juu ya Madai ya Waislam Juu ya kipengere Cha dini katika Sensa

Kwanza kabisa Serikali ya CCM ndio wanaoleta Udini Katika Nchi na Kuwagawa Watanzania:

1. Mtu anapo kamatwa anaulizwa dini wakati polisi na serikali hawana dini. Hapa haki haiwezi kutendeka hasa inapo onekana mtoa haki anataka kujua dini
2. Mtuhumiwa anapopelekwa mahakamani anaulizwa dini yake na kulazimishwa kuapa kwa dini kinyume na vitabu vya dini.
3. Wafungwa na mahabusu wanafungwa na kuhifadhiwa kwa dini jambo ambalo ni hatari kwa utaifa.Tumetembelea Magereza mengi tukaona serikali hiyo hiyo imewafunga watu na kuelezea kipengere cha dini ambapo tumebaini kuwa Wafungwa wengi ni Wailamu
4. Wananchi wanalazimishwa kuapa mahakamani mbele ya Makalani wa mahakama na Mahakimu wamekuwa miungu watu
5. Ikulu ya DSM inaapisha watu kwa dini na tumefuatilia na kugua kuwa tangia Ikulu ianze kuapisha watu , Wakristo wengi wameapishwa.
6. Bungeni Wabunge wana apishwa kwa Dini zao na tangia Uhuru Wabunge Wakristo ndio wanao tawala nchi hii huku Waislam wakihujumiwa.
7. Wagombea ubunge na urais Wanalazimishwa kuapa mahakamani kw kipengele cha dini na kumuasi Mungu na ndio maana Laana imelikumba Taifa na machafuko ya migomo.

Hoja ni kwamba kama serikali inaapisha watu kwa dini zao basi Katiba ya nchi itambue uwepo wa Mungu ili iwe sheria Vinginevyo Watu wananyanyaswa na kumuasi Mungu kwa kulazimishwa kuapa!!!

Kama serikali haitaki UDINI katika Sensa basi Waondoe Uchafu huo katika Mihimili yote ya dola kwa maana ya Serikali( Ikulu) , Bunge, na Mahakama!!

Ni jambo la ajabu kuona kuwa CCM inapinga pinga udini ndiyo imekuwa ya kwanza kuchochea udini katika suiasa kwa maslahi ya utawala.

Ilani ya CCM 2005 ina kipegere na UDINI kuwagawa Waislam!!


JUKWAA LA WAISLAMU LA KURATIBU MCHAKATO

WA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA
(JUWAKATA)
MUHIMU WA KWAISLAMU WOTE


1. JUWAKATA
JUWAKATA ni Jukwaa la waislamu la Kuratibu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Tanzania. Chombo hiki kinaundwa na Jumuiya na Taasisi mbalimbali za Kiislamu sizizopungua 40. Chombo hiki kilizinduliwa rasmi katika kongamano kubwa lililohudhuriwa na kada mbalimbali za Masheikh, wanataaluma na viongozi wa Kiislamu lililofanyika Januari 6,2012 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam na kuhusisha vyombo mbalimbali vya habari. Makao makuu ya JUWAKATA ni Dar es Salaam. JUWAKATA lina mawasiliano ya karibu na Waislamu wa Tanzania visiwani kwa uratibu wa pamoja.
Aidha azimio la mkutano mkuu wa Jumuiya na Taasisi za kiislamu, liipa JUWAKATA idhini ya kushirikiana na muislamu au mwananchi yeyote mwenye malengo ya kupatikana katiba yenye missing ya haki na uhuru pasina ubaguzi wa aina yoyote.

2.
MAELEZO YA AWALI
Nchi yetu imo katika mchakato wa mabadiliko ya katiba ya nchi. Wananchi wa Tanzania wanakabiliwa na jukumu moja la kuhakikisha katiba ijayo itakuwa kwa maslahi ya watanzania wote na yenye kuzingatia haki na usawa bila kujali kbila, rangi, dini wala jinsia. Tukio la kuundwa kwa katiba ya nchi ni miongoni mwa matukio makubwa kabisa katika nchi yoyote ile dunia. Ni kwa sababu hii, mivutano, ushindani, kupigana vikumbo, mizengwe na mahala pengine vita vya wenewe kwa wenyewe hutokea. Ni kwa kutambua ukweli huu, sisi waislamu wa Tanzania tayari tumekwisha ipatia ushauri serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Tume ya kurekebisha katiba tahadahari y akuzingatiwa haki na uadilifu katika mchakato wote wa mabadiliko ya katiba ili katiba iwe ka faida ya wote wa mabadilliko ya katiba ili katiba iwe kwa faida ya wote na iwe msingi wa kudumisha amani iliyopo.


3.
KATIBA YA NCHI NI NINI
Katiba ya nchi ni makubaliano ya wananchi kuhusu haki na wajibu mbalimbali kati ya dola na raia na jinsi ya mgawanyo wa madaraka na rasilimali za taifa, mfumo wa utoaji haki na ulinzi na usalama wan chi.
Kutokana na ainisho hili la ujumla, makubaliano haya ya katiba yanaweza kuwekwa katika maandiko au yasiwekwe. Hata hivyo nchi nyingi duniani zinaongozwa kwa katiba iliyoandikwa. Mara nyingi tumepata kasikia kwamba ‘katiba ndiyo sheria mama ya nchi’. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, sheria na kanuni mbalimbali zinazoongoza nchi chimbuko lake ni katiba. Katiba hujumuisha mambo makubwa ya kisheria ambayo huandikwa kwa mukhtasari. Kwa mfano kipengele kimoja kinachozuia ubaguzi, kinaweza kukusanya mambo lukuki yanayohusu ubaguzi wa rangi, jinsia, dini, ukabila umri, hadhi katika jamii nk. Kwa muktadha huo Bunge la nchi ndicho chombo kinachoundwa na katiba kwa unadhumuni ya kutunga sheria, kanuni mbalimbali ili kufafanua jinsi ya kutekeleza vipengele vya katiba huska. Sheria na kanuni ambazo hutungwa na bunge, ikiwa zitapingana na katiba ya nchi, sheria hizo huhesabika kuw ani batili (yaani ill and void).

4.
Katiba zimegawanyika katika mfungu makubwa mawili.

o
Katia za kisekula na
o
Katiba ya Kiislamu.

Katiba za kisekula zimebeba taswira kubwa mbili:


(a) Katiba za kidikteta na
(b)
Katiba za kidemokarasia.

Katiba za kidikteta
ni zile ambazo wananchi hawana kauli juu mambo ya uendeshaji wan chi yao wala hawaruhusiwi kuchagua wawakilishi wao bali mamlaka na madaraka yote ya nci yako mikononi mwa mtu au tabaka la watu wachache. Katiba za kidemokrasia ni ile ambayo wananchi wanashirikishwa katika kuamua nchi yao iendeshwe namna gani na wanashiriki katika kuiendesha nchi kwa kuchagua wawakilishi wao. Katiba ya Kiislamu – Hii hutokana na Qur’n na snnah za Mtume (SWALALLAH ALAYHI WASALLAH) na Ijumaa ya wanazuoni. Wananchi hulazimika kutii na kutekeleza mipango na ibada nyingine kwa kadiri ya uwezo walio nao. Watawala wa Kiislamu huongoza na kutoa hukumu kwa kila jambo kwa kuzingatia mwongozo wa Allah (Subhaanahu Wataala) na Sunnah za Mtume (SWALALLAH ALAYHI WASLLAM).

5.
MUUNDO NA VIPEGELE VYA KATIBA YA TANZANIA
Muundo wa dola ya Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya sasa ni wa ushirikishwaji wa wananchi katika uendeshaji wan chi kupitia wawakilishi ( wabunge, wajumbe wa baraza la wawakilishi na madiwani).
Katiba ya Tanzania ina sehemu kuu kumi (10) na ibara (152) kuhusu mambo mbalimbali. Katika sehemu zake kumi (10) na ibara (vifungu) 152 katiba ina sehemu zinazoeleza misingi ya katiba, muundo wa dola, mipaka ya nchi, vyama vya siasa, sera ya nchi, haki za raia na wajibu wao, majukumu ya Serikali, bunge, Mahakama nk. Kwa ujumla kutokana na muundo huu wa katiba ya Tanzania, katiba iliyopo sasa inahesabika kuwa ni miongoni mwa ‘katiba za kidemokrasia’.

6. HATUA ZA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA
o
Kupitishwa kwa Sheria yamabadiliko ya Katiba Hatua hii ilifikiwa mnamo mwezi wa Novemba, 2011 pale muswada wa Sheria Na. 8 ya mabadiliko ya katiba 2011 ulipopitishwa na Bunge. Kisha yalifuata marekebisho ambayo yalifanyika Januari, 2012. Sheria hii ya mabadiliko ya katiba, ndiyo inayomumika kuongoza mchakato huu.

o Kuundwa Tume ya Katiba
Tume ya kukusanya na kuratibu maoni ndicho chombo chenye dhima ya kushughulikia sehemu kubwa ya mchakato wa katiba mpya. Chombo hiki chenye wajumbe 30, Mwenyekiti na Makamu wake, kimeundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kushirikiana na rais wa Zanzibar April 6, 2012. Hatua hii imetanguliwa na ile ya bunge la Jamhuri ya Muungano kupitisha sheria ya mabadiliko ya katiba The Constitutional review Act iliyopitishwa Novemba 18, 2011.
Tume ya Katiba itakuwa na sekretarieti yake ambayo ndiyo itakuwa mtekelezaji wa shughuli mbalimbali za tume kiufundi Ukusanyaji maoni kutoka kwa Wananchi Tume itaendesha, mikutano (mabaraza) ya hadhara ya ndani na nje, na hata kupokea maoni kwa njia ya maandishi kwa nchi nzima. Hii ndio kazi ya msingi ya tume mara baada ya kuundwa na kuapishwa wajumbe wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano.Baada ya kazi ya kukusanya maoni tume itaandaa rasimu ya katiba mpya itakayotokana na maoni iliyoyakusanya.

o
Rasimu yaKatiba mpya
Baada ya kukusanya maoni na kuandaa rasimu ya katiba mpya iliyotokana na maoni yaliyotolewa, rasimu ya katiba mpya itachapishwa katika vyombo vya habari ili kutoa fursa kwa wananchi kuthibitisha maoni yao. Baada ya hatua hiyo rasimu ya katiba mpyaitakabidhiwa kwa Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar.

Rasimu ya katiba mpya kujadiliwa na Bunge maalum la katiba.Bunge hili litaundwa na wajumbe wafuatao.
i. Wabunge wote wa muungano
ii. Wajumbe wa baraa la wawakilishi Zanzibar
Na
iii. Wajumbe 166 kutoka:-

(a) Vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
(b) Asasi za kijamii (NGO’s)
(c) Jumuiya za Dini
(d) Makundi ya wakulima
(e) Wafugani.
(f) Taasisi za elimu ya juu
(g) Wafanyakazi
(e) Makundi mengine yenye maslahi ya pamoja
(f) Makundi yenye mahitaji maalum.

Mwenyekiti wa tume ya katiba atasoma rasimu hiyo kwa mara ya kwanza ndani ya bunge maalum la katiba na kukabidhi jukumu hilo kwa Mwenyekiti wa bunge la katiba ili ijadiliwe na bunge hilo na hatimaye kuipitisha au kuirejesha ikafanyiwe marekebisho. Endapo Bunge maalumu la katiba litaipitisha rasimu ya katiba hatua itakayofuata ni kupigiwa kura ya maoni na watanzania wote.

o Kura ya maoni
Baada ya rasimu ya katiba kupitishwa na bunge la katiba itakuwa katiba iliyopendekezwa na itakabidhiwa kwa tume ya Taifa ya uchaguzi yaani NEC na tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC kwa ajili ya kuandaa na kusimamia kura ya maoni, kwa kupiga kura ya NDIYO au HAPANA. Ikiwa rasimu hiyo itakubaliwa na wananchi wa bar kwa 50% na visiwani kwa 50% katiba mpya itakuwa imeundwa, na kwa matarajio ya serikali katiba hiyo itaanza kutumika Aprili 26, 2014.


7. KWA NINI WAISLAMU WNASHIRIKI KATIKA MCHAKATO WA KATIBA?
Sababu kubwa ni wajibu wa waislamu kupigania haki ili kuwa na katiba nzuri inayolinda haki zetu. Kuwa na katiba inayolinda haki za waislamu kama sehemu ya watanzania ni njia bora zaidi ya hakikisho la haki katika mfumo w uendeshaji wan chi kama hii inayojiita ya kisekula. Kwa mfano, Katiba iliyopo imechangia kwa kiasi kikubwa kuwaathiri Waislamu kiimani, kiuchumi na kijamii. Waislamu tumekosa haki ya Mahakama ya Kadhi, haki ya kuwa na muwakilishi bungeni, haki ya kuwa na mfumo wetu wa elimu, haki ya kunufaika kwa misaada ya kishirika la kimataifa la waislamu OIC, haki ya usawa katika miliki ya ardhi, haki ya usawa katika uteuzi wa nagazi mbalimbali za uongozi wan chi, haki ya kuheshimiwa sheria za kiislamu n.k. Kutokana na udaifu w akikatiba uliopo, serikali kupitia amri ya Rais ilizifuta Mahakama za Kadhi mwka 1963 na ilipofika mwaka 1971 bunge lilipitisha sheria ya ndoa. Sheria hii inazidhalilisha sheria za Kiislamu kw akuhukumiwa na mahakama zisizo za kiislamu na pia kusimamiwa au kutafsiriwa na wasioziamini (wasiokuwa waislamu) na kusababisha kutolwea kwa taafsiri potofu.

Mwaka 1992 serikali iliingia mkataba wa maridhiano na Makanisa (MoU) kugharamia shughuli za kijamii, kiafya na kielimu za Wakristo bila ya kuwasikiliza waislamu au kutupa fursa kama hiyo sisi waislamu nk.
Aidha haki z amsingi za raia wakiwemo waislamu hutolewa na kuhakikishiwa (guarantee) na katiba. Kwa katiba iliyopo sasa haki hizi hazipatikana kwa uwazi, uhakika na kwa haki; na endapo mtu au serikali ikivunja haki hizo ni vigumu mno kuchukua hatua kwa mfano tokea mauaji ya Mwembechai, 1998 hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya wauaji. Kwa mantiki hiyo utaona wajibu wa kupigania mabadiliko ni MUHIMU SANA. Hofu yetu katika mchakato huu ni je, tume ya katiba itafanya uadilifu kwa wananchi wote bila kujali dini? Hofu hiyo si kigezo cha kuturudisha nyuma na kuwaacha wasiokuwa waislamu kuyasemea yanayowahusu waislamu. Hivyo bas waislamu lazima tushiriki kuhakikisha uadilifu, haki vinazingatiwa, waislamu wanasikilizwa na maoni yao yanazingatiwa.

o
Uislamu na katiba Mtume Muhammad (SWWALALLAH ALAYHI WASALLAM) aliandika waraka wa makubaliano ya namna ya kuishi kati ya waislamu na jamii mchanganyiko alipofika Madina. Makubaliano haya kwa lugha ya sasa yanaitwa katiba. Utaratibu huu ulimuwezesha Mtume (SWALALLAH ALAYHI WASALLAM) na waislamu kutekeleza Uislamu wao kwa uhuru na maelewano na jamii nyingine.

o
Mtazamo wa Fiq-hi na mazingira yaliyopo Waislamu kwa nyakati tofauti ima watakuwa wanaishi katika dola ya Kiislamu (Daarul Islaami) ama dola kama ya Tanzania ambayo si ya kiislamu. Katika dola ya Kiislamu, sheria zote za nchi chimbuko lake ni Allah (Subhaanahu Wataala), na katika dola isiyokuwa ya kiislamu ni kinyume chake. Waislamu tunaishi katika nchi hizi (Daarul harb) na katiba zake zinatuathiri sana kwa njia moja ama nyingine. Kwa sababu hiyo tunalazimika kushiriki katika kuundwa kwake kwa lengo la kuondoa kabisa na ikibidi kupunguza madahara yake kwetu na kwa jamii na wala si kwa lengo la kuipa nguvu mifumo dhidi ya mwongozo wa Allah (Subhaanahu Wataala). Hapana shaka Fatwa ya jumuhuri ya wanazuoni wa iq-h ulimwenguni, Fatwa za Kamati ya Kudumu ya ataawa na Uchunguzi ya Saudia, Fatwa ya Chuo Kikuu cha Al Azhar, Sheikh Al Uthayminyn, Ibn Jibriin, Nassur ad-Dyn Al-Albany n.k zilizopitisha kuwa inajuzu kwa waislamu kushiriki katika mambo mbalimbali (kama siasa, chaguzi nk) katika nchi za kitwaaghuti wanazoishi, zimezingatia hekma ya Qur’an na mafundisho ya Mtume (SWALALLAH ALAYHI WASALLAM).

o
WAjibu kwa viongozi wa Kiislamu Kila jamii hutaraji maelekezo kutoka kwa viongozi wao. Kwa hiyo wajibu wa kwanza kwa kiongozi wa umma wa waislamu ni kujitambua kwamba waislamu wanamtegemea awaelekeze jinsi ya kushiriki wa namna itakayoleta tija kwao nakwa taifa kwa ujumla. Kiongozi pia anapaswa kuwa na ung’amuzi wa nini kinachoendelea katika kijiji, mtaa, mji, kata, tarafa, wilaya na Mkoa wake kuhusu mchakato wa katiba.

8.
MAMBO YA KUPIGANIWA NA WAISLAMU KATIKA KATIBA MPYA

Sehemu A. MASUALA YA MSINGI KWA WAISLAMU.


i. UWEPO WA MWENYEZI MUNGU
Hapa tunapendekeza katiba mpya itambuwe uwepo wa Mwenyezi Mungu

Ibara ya 19 (1-3) inatoa uhuru wa imani na dini. Kwa kuwa katiba inatambua uwepo wa dini bas itambue pia uwepo wa Mwenyezi mungu isipokuwa tu kwamba kila mtu awe huru kuamini Mungu kwa mujibu wa imani yake. Ikumbukwe kuwa viapo mbalimbali hutolewa mahakamani, bungeni na serikalini kwa wabunge, majaji, mahakimu, watendaji wa serikali n.k.
Basi ni busara na uungwana Mungu huyo anayemuomba kwa kusema “Ee Mungu nisaidie” uwepo wake utambuliwe katika katiba.

ii. UBAGUZI WA KIDINI KWA SIKU ZA MAPUMZIKO UFUTWE
Upendeleo wa kidini uondolewe. Mfano;- Siku za mapumziko Jumamosi na Jumapili ni siku za ibada kwa Wakristo. Hivyo ni vyema Ijumaa nayo iwe mapumziko walau nusu siku ili kuruhusu waislamu nao wawe huru kwa ibada hasa sala ya Ijumaa. Pia upendeleo wa kidini katika pato la taifa uondolewe. Kama MoU unayoitaka serikali kutoa pato la taifa na kuipa dini hiyo huku dini nyingine zikinyimwa haifai. Katiba mpya ni vyema ikapiga marufuku suala kama hilo kutendwa na serikali.


iii.
KATIBA ITAMBUE NA KUIREJESHA MAHAKAMA YA KADHI.
Katiba mpya itambue na iweke utaratibu wa uwepo wa Mahakama ya Kadhi ambayo itaendeshwa na waislamu wenyewe kama moja ya Mahakama za nchi. Mashauri yote yanayohusu ndoa, talaka, mirathi, waqf, malezi ya watot, hibba (zawadi), wosia, biashara, bima kwa mujibu wa dini ya kiislamu yasikilizwe katika Mahakama ya Kadhi alimradi mhusika/wahusika ni waislamu. Pawekwe kipengele kinachozuia rufaa za Mahakama ya Kadhi kwenda kwenye mahakama za kawaida. Mahakama ya Kadhi iwe chombo chenye nguvu za dola na ipewe haki na uwezeshaji wa kifedha kutoka serilini ili kutekeleza majukumu yakekatika ueneshaji wa kesi. Ni dhahiri kuwa baadhi ya sheria za kiislamu ni sheria halali za nchi hii. Mfano sheria za ndoa na mirathi, seria hizi hazipati tafsiri sahihi kutokana na mamalaka zilizopewa jukumu la kuzisimamia kuendeshwa kinyume na misingi ya dini ya kiislau kwa asiyekuwa muislamu kuruhusiwa kutafsiri sheira za kiislamu. Hili pia linatokana na ujuzi finyu wa utambuzi matumizi ya hukumu za sheria hizi ambalo ni tatizo katika kusimamia haki zitokanazo na sheria za kiislamu. Kwetu sisi Waislamu kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria zakiislamu ni tendo la kiibada na kijamii, na vile vile kuhukumiwa nje ya misingi hiyo ni matendo yanayoingilia uhuru wetu wa kuabudu. Hivyo bas tunataka katiba mpya itambue na iweke utaratibu wa uwepo wa mahakama ya kadhi mahakama ambayo itaendeshwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu katika mambo yahusuyo waislamu bila ya kuingliwa na chombo chochote. Hakika hili ni eneo muhimu na nyeti sana kwa uislau tunataka tume ya katiba isipuuzwe kwa namna yoyote hitajio hili kw alengo la kulinda amani na kuheshimu imani na uhuru wa kuabudu kwa waislamu. Ni pendekezo letu piakuwa rufaa za mahakama ya kadhi zishughulikiwe bila ya kuhusisha mahakama za kawaida. Tunataka mtu ambaye amefunga ndoa ya kiislamu au anaishi kama Muislamu ninamtambua kuwa ni Muislamu iwe ni kigezo cha shauri lake la mirathi na ndoa kupelekwa katika Mahakama ya Kadhi na siyo ridhaa ya warithi au maoni ya mtu mwingine.

iv. ADHABU YA KIFO KWA MUUAJI IENDELEE KUTAMBULIKA KIKATIBA
Yapo madai yanayotolewa kutaka adhabu ya kifo ifutwe kwa kuwa eti ni kinyume na haki za binadamu. Kuondolewa kwa adhabu ya kifo kutaleta hali ngumu kwa jamii na hasa wanyonge kwa sababu:-
o
Mauaji ya raia wasio na hatia yataongezeka sana.
o Nchi zilizoondoa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji, bado haikupunguza idadi ya wahalifu wa makosa ya mauaji. Mfano, Afrika ya kusini waliiondoa na sasa wanajadili kuirudisha.
o
Hoja ya wapinga adhabu ya kifo kuwa
o
Kosa la kuua linaumiza na linakwenda mbali sana zaidi ya kwa Yule alieyeuliwa ndugu yake hivyo basi muuaji akiendelea kuishi kwa kulishwa na serikali kwa kodi za waliouliwa ndugu yao kutachochea mauaji na visasi zaidi, tunaamini salama yake na ya jamii ni muuaji naye kuhukumiwa kuuwawa kuzuia raia kujichulia hatua mikononi mwao.
o
Hoja ya kwamba adhabu ya kifo haimpi muuaji nafasi ya kujirekebisha haina mantiki kwani adhabu si sehemu pekee ya kujirekebisha bali ni hukumu kwa matendo ya mtu na katazo (detterance) kwa wengine.
o Pia hoja ya kwamba adhabu ya kifo inamdhalilisha mtuhumiwa nayo haina mantiki kwani hakuna adhabu ambayo inampa sifa mtuhumiwa; bali adhabu zote mfano kifungo, faini au viboko zinadhalilisha na dio maana zikaitwa adhabu na sio pongezi.

v.
KATIBA ITAMBUE HAKI YA WAISLAMU KUWA NA MFUMO WAO WA ELIMU.
Nchi mbalimbali duniani zinaruhusu watu wa dini mbali mbali kuwa na mfumo wao wa elimu ili kutoa nafasi ya kufundisha watoto wao imani, mila na desturi zao alimradi wanaingiza na mitaala ya kiserikali. Afrika ya Kusini, Uingereza, India na hata Marekani hufanya hivyo.
Waislamu tumeruhusiwa kuanzisha mashule yetu lakini yanadhibitiwa mitaala, vitabu, kanuni na sheria mbalimbali na Wizara ya elimu kiasi kwamba sisi ni waathirika wakubwa wa kufutiwa mitihani, kuhujumiwa hujuma mbali mbali pamoja na watoto wetu kuzuiwa kutekeleza dini yao katika shule na vyuo vya serikali. Mfano, sakata la wanafunzi wa Kiislamu ndanda Mokoani Mtwara kufukuzwa shule kwa kutekeleza uislamu wao. Katiba itamke wasi kuwa wananchi wana uhuru wa kuwa na mfumo wao wa elimu kwa mujibu wa dini yao. Tayari kuna shule na vyuo (academia) vinavyoenedshwa kwa mitaala ya Uingereza na hata kuendesha shule na vyuo kwa mitaala yao kama ilivyo kwa Vyuo vyao Vikuu? Kuendelea kulazimisha mfumo wa elimu wa pamoja ni kukiuka misingi ya haki za binadamu na uhuru wa mawazo (freedom of opinon).

Sehemu B. HAKI ZA MSINGI ZA BINADAMU
HAKI YA UHURU KAMILI WA IBADA NA UWAKILISHI KIDINI.

a) Katiba itoe haki na uhuru kamili wakuabudu
Katiba ya sasa inatoa uhuru wa kuamini na uchaguzi katika mambo ya dini (Ibara 19: 1-3) lakini haitoi uhuru wa kuabudu. Hii inafanya baadhi ya waumini kulalamika kwamba hawapati uhuru kamili wa kuabudu. Baadhi ya masuala yanayolalamikiwa ni pamoja nay a akina mama wa kiislamu jeshini, polisi, na baadhi ya masuala yanayolalamikiwa ni pamoja nay a akina mama wa kiislamu jeshini, polisi, na baadhi ya ofisi kutoruhusiwa kuvaa hajab, wanazuiliwa kuswali katika mashule, vyuoni na maeneo ya serikali nk. Katika uhuru wa ibada, sheria za kiislamu ziheshimiwe mfano mirathi, ndoa, talaka, waqf, biashara, bima n.k. zitambuliwe kikatiba kamasehemu ya ibada yetu. Hii itafanya mahakama ya kadhi iwe na maana kwani sheria zitakazotumika katika mahakama hizo zitakuwa zinatambuliwa na hivyo haitakuwa rahisi kuziondoa kama ilivyopata kutokea huko nyuma. Hili linajitokeza pale ibada hizi muhimu zinakandamizwa kwa vigezo vya haki za binadamu vya kimagharibi bila kuzingatia kwamba haki ya kuwa katika dini ni ya hiyari na kwamba mtu anaingia na kubaki katika dini akijua iko hivyo.

b)
UWAKILISHI WA KIDINI BUNGENI
Katiba itamke uwepo wa viti maalum vya uwakilishi wa makundi ya dini hasa Waislamu na wakristo Bungeni. Bunge ndio mhimili wa dola unaowakilisha maoni na matakwa ya wananchi. Hali ilivyo hivi sasa yanapojitokeza mambo yanayowahusu waislamu na wanadini wangine bungeni maoni yao hayapati nafasi walakuzingatiwa.


c)
TUNATAKA UWAKILISHI WA KIDINI KATIKA BARAZA LA MADIWANI
Katiba itamke kamatulivyopendekeza katika uwakilishi wa Waislamu na wakristo bungeni kwamba katika serikali za mitaa pia kuwe na uwakilishi kama huo.


d)
SHERIA YA UGAIDI IFUTWE
Katiba mpya ipige marufuku sheria ya ugaidi ya mwka 2002 na utungwaji wa sheria kama hizo zinazopelekea kuvunjwa kwa haki za msingi za binadamu na ambazo utekelezaji wake unaleta manyanyaso na madhara makubwa kwa Waislamu kama ilivyo sasa nchini Tanzania.


e)
Haki za binadamu ziendane na maadili ya Dini nay a Kitanzania
Tunataka katiba mpya isiruhusu mambo ya kishetani kama vile ulawiti, dnoa za jinsia moja, uto9aji wa mbimba, uhuru wa kupindukia wa motto dhidi ya wazazi wake na mfano wa hayo kuwa ni miongoni mwa haki za binadamu. Zipo kampeni zinazoshinikizwa na makundi yanayojiita watetezi wa haki za binadamu na hata baadhi ya nchi za nje kama vile Uingereza kutaka kushinikiza kuingizwa mambo hayo katika katiba mpya.


f) Katiba mpya itoe ainisho sahihi la ndoa na familaia
Kutokana na shinikizo la ushoga dhidi ya nchi yetu ni muhimu katiba iamke wazi maana ya ndoa. Katiba itamke hivi ‘ndoa ni baina ya mwanaume na wanawake au mwanaume na mwanamke.
Ndoa kati ya watu wa jinsia moja zisiruhusiwe na iwe ni kosa la jinai iwapo watu wa jinsia moja watabainika kuoana au kuishi kama mke na mume ili kulinda maadili yetu.

g)
Nafasi mbali mbali za uteuzi serikalini na mashirika ya dini zizingatie uwiano wa kidini kati ya Wakristo na Waislamu.
Katiba mpya iweke utaratibu kuwa nafasi zote za uteuzi serikalini na katika idara zake, uwakala wa asasi za serikali nk zizingatie uwiano ulio sawa baina ya dini za waislamu na wakristo, ili kuondoa manung’uniko kuwa kuna ubaguzi katika uteuzi wa nafasi za uongozzi serikalini.
Hii itasiadia kuweka misingi ya usawa katika utumishi wa umma na kuondoa hisia za udini. Salama ya nchi hii kwa kiasi kikubwa inategemea kuaminiana na kuheshimiana baina ya dini hizi kuu mbili, hivyo basi uwiano katika uteuzi ukilindwa kikatiba itakuwa ni kujenga msingi imara wa amani, haki na kuaminiana.

h)
Urekebishwaji wa vifungu vya haki za binadamu ndani ya katiba.
Pia tunapendekeza kuwepo taratibu makhsusi za urekebishaji wa vifungu vya haki za binaadamu katika katiba. Utaratibu wa sasa wa vifungu hivyo kurekebishwa kama vifungu vingine vya Katiba ni hatari kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa haki za binaadamu katika maisha yetu.
Vifungu kama vile vinavyohusiana na haki ya kuishi, kuchagua na kuchaguliwa, kuabudu, kufanya kazi, kutokubaguliwa, uraia na kumiliki mali visibadilishwe mpaka iwepo ridhaa ya wananchi kwa njia ya kura (referendum). Haki nyingine za Katiba zisibadilishwe mpaka zaidi ya asilimia 75 ya wabunge kutoka pande zote za Muungano waridhie na pia iwepo haki ya wananchi wasioridhika na mabadiliko hayo kuyapinga katika Mahakama Kuu ya Katiba ndani ya siku tisini toka marekebisho hayo yalipofanyika. Muswada wowote wa kurekebisha kifungu chochote kinachohusu haki za binadamu lazima usambazwe kwa wananchi kutoa maoni yao ndani ya siku 90 kabla haujawomwa Bungeni. Ili kulindwa kwahaki zabinadamu na kuwepokwa uwazi tunapendekeza sheria zote kandamizi maarufu kama sheria 40 zilizoorodheshwa na tume ya jaji nyarali zifutwe. Adhabu ya kifo kwa makosa makubwa kama mauwaji ya makusudi iwepo katika katiba mpya na iwe ni moja kati ya mambo ambayo hayawezi kubadilishwa bila referandamu (kura yamaoni).

i) Mahakama Kuu ya Katiba na haki za binadamu
Tunataka katiba mpya iruhusu uwepo wa mahakama Kuu ya Katiba ambayo itapewa uwezo na nguvu za kisheria wa kutafsiri vipengele mbali mbali vya katiba na pia kubatilisha sheria yoyote itakayotungwa ambayo inapingana na katiba.
Mahakama hii pia izuie marekebisho ya katiba yanayokinzana na misingi ya Katiba yenyewe. Na ili hili liwe na mantiki, Katiba itamke wazi kwamba baadhi ya vifungu vya Katiba kama vile vinavyohusu Muundo wa Dola, Muungano, haki za binadamu makhsusi zinazorekebishika kwa ridhaa ya wananchi ndio utakuwa msingi mkuu wa katiba na kawamba haiwezi kubadiliswa bila kuwa na ridhaa ya wananchi kupitia kura ya maoni (referendum). Pawepo na mahakama Kuu ya Katiba ambayo itakuwa na hadhi ya muungano na pia pawe na Mahakama ya rufaa ya Katiba ambayo pia itakuwa ya muungano. Mahakama Kuu ya Tanganyika na Mahakama kuu ya Zanzibar kamailivyo Mahakama ya Rufaa ya Tanganyika zisiwe sehemu ya Muungano.

j)
Mahakama za hakimu mkazi
Mahakama za Hakimu Mkazi zifutwe na badala yake ziwepo Mahakama za wilaya ambazo zitaendeshwa na Mahakimu wa Daraja la Pili ambao watakuwa na uzoefu wa kuwa mahakimu wa mahakama za mwanzo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano.
Mfano wa sasa hivi wa kuwa na mahakama za wilaya na mahakama za hakimu mkazi ambazo zinaharibu mamlaka sawa hauna tija. Na pia mfumo wa kuwapa uhakimu mkazi wahitimu wa chuo wasiokuwa na uzoefu wowote unakwaza utoaji haki. Ni bora mahakumu kama hao wkanzia mahakama za mwanzo.

k)
Haki ya kumiliki Ardhi
Haki ya kumili Ardhi iwe ni haki ya raia. Mgeni anaweza kuruhusiwa kumiliki ardhi kwa kushirikiana na mzawa tu na kwa masharti kwamba hamilik zaidi ya asilimia 45 ya ardhi hiyo ya pamoja na kwamba umiliki wake uwe ni kwa ajili ya uwekezaji na si makazi. Pawepo na ukubwa maalumu wa ardhi mtu mmoja atakubaliwa kumiliki. Zaidi ya hapo raia awe na haki ya kukodisha ardhi anayoimiliki kwa muda usiozidi miaka kumi na tano. Hii inakusudia kuondoa uwezekano mtu mmoja au kikundi cha watu kumiliki na kuhodhi eneo kubwa la ardhi na kuacha jamii kubwa ya watanzania wakikosa haki ya kumiliki ardhi.. Ikumbukwe kuwa ardhi haiongezeki bali watu wanaongezeka. Mamlaka ya Raisi ya kutwaa ardhi kwa maslahi ya umma iweke wazi mambo yanayohesabika ni maslahi ya umma na itoe muda maalumu kwa mtu asiyeridhika kutaka rufaa dhidi ya uamuzi wa kutwaliwa ardhi yake katika Mahakama ya Ardhi. Katiba ielekeze Sheria za mipango miji zitenge maeneo ya dini (ibada) kwa kuanisha maeneo ya waislamu, wakristo na dini zingine kama vile majumba ya ibada, makaburi n.k na sio kutaja kiujumlajumla “eneo la kidini” kama ilivyo sasa. Kitendo cha kutaja kujumlajumla “eneo la Kidini” bila kuanisha dini gani kinafanya makundi ya dini moja kuhodhi maeneo makubwa kuliko makundi mengine na hivyo kusababisha manugu’niko.

Sehemu C. MUUNDO W ASERIKALI NA MUUNGANO


i. Tunapendekeza nchi yetu iwe na serikali tatu, yaani serikali ya Muungano, serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar Pendekezo hili linalenga kutrejesha katika dhamira ya uasisi wa Muungano kama unavyojidhihirisha katika hati ya Muungano ya 1964 ambao ulibainisha wazi kuwepo kwa muungano wan chi mbili n aserikali tatu. Hili pia linalenga kuondoa malalamiko ya mara kwa mara ya kila upande kuona unaburuzwa au kuonewa ndani ya mfumo wa serikali mbili tulionao hivi sasa. Vile vile litatibu kilio cha Watanzania kujiamulia mambo yao na kile cha watangayika kufuatiwa serikali yao. Mfumo wa sasa wa himaya tatu katika serikali mbili kuna matatizo mengi kiutendaji na kisiasa hasa katika himaya ya Tanganyika ndani ya serikali ya Jamhuri. Kwa mfano, nafasi kama ya Waziri Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali zinazua utata kama ni nafasi za muungano au Tanyanyika. Maana, hadhi ya Waziri Mkuu haitambuliki Zanzibar na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar nako kuna Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Pia wabunge wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano chini ya mfumo huu wanpata nafasi ya kujadili na kutoa maamuzi juu ya masuala ya Wizara za Tanzania Bara kama vile Wizara ya elimu wakati wabunge wa Tanzania Bara hawana nafasi hiyo katika Wizara za Zanzibar.

ii. Tunapendekeza Urais wa serikali ya muungano uwe ni wa kupokezana kwa Tanganyika na Zanzibar. Ili kuondoa manugu’niko kama tulivyoeleza hapo juu sisi waislamu tunaona kwamba umefika wakati sasa nafasi ya uongozi wa Rais wa serikali ya Muungano iwe ni ya kupkezana. Tunataka utaratibu huo sasa uwe rasmi kikatiba.

iii. Mambo yaliongezwa katika orodha ya mambo ya Muungano yaliyopo katika hati ya Muungano yajadiliwe upya Masuala yatakayokubalika kuwa ya Muungano yasirekebishwe isipokuwa kwa ridhaa ya wananchi wa sehemu zote za Muungano kwa njia ya kura ya maoni (refere’ndum). Ili kulinda maslahi ya Zanzibar kutokana na idadi yao, kura zitazingatia uwiano wa sehemu mbili za Muungano na sio idadi ya watu. Katika masuala yanayoweza kukubalika kama masuala ya Muungano, Katiba ya Jamhuri ya Muunganoa na Katiba za Tanganyika na Zanzibara zitamke bayana kwamba iwapo kutakuwa na ukinzani wowote kati ya katiba ya Jamhuri na Katiba za Zanzibar na Tanganyika kuhusiana na masuala ya Muungano, katiba za nchi hizi zitakuwa batili kwa kiwango cha ukinzani kwenye vifungu husika. Hili litalinda uwezekano wa kuwepo migogoro inayotokana na moja kati ya nchi hizi kurekebisha katiba kwa namana inayoweza kuvuruga sura ya Muungano. Mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya hivi karibuni yanaweza kutoa picha ya uwezekano huu.

iv.
MALIASILI NA MUUNGANO
Kwa maoni yetu masuala ya madini na mafuta hayana sababu yoyote ya kuwa masuala ya Muungano. Ni bora yakabaki katika serikali husika ili kuondoa malalamiko kwamba sehemu moja ya muungano inataka kujinufaisha na maliasili zilizopo katika sehemu nyingine.

Vi URAIS WA TANGANYIKA
Tunapendekeza kwamba Uraisi wa Tanganyika uwe wa kupokezana kuzingatia makundi makubwa ya kijamii waislamu na wakristo. Kwa muda mrefu katika serikali ya Tanzania, has katika kipindi cha mfumo wa chama kimoja, kumekuwa na kanuni, japo hazikuandikwa, za kupokezana uraisi kati ya wailsamu na wakristo. Utaona kwamba Raisi w aPili Mwinyi ambaye ni muislamu. Mwingyi akarithiwa na Mkapa mambaye ni Mkristo naye akarithiwa na Kikwete ambaye ni Muislamu. Kwa mazingira yetu ambayo uwiano wa idadi kwubwa ya watanzania ni aidha waislamu ama wakristo na ukizingatia mvutano wa chini chini unaojitokeza kati ya wanadini hizi kuu mbili nchini kuhusiana na uwakilishi katika dola, ni busara kama mfumo huu aliotuachai mwalimu ukaendelezwa na ikibidi kulindwa kikatiba. Mfumo huu pia unaweza kuwa msingi wa kulinda umoja wetu na uvumilivu.

Vii,. BARAZA LA MAWAZIRI NA UBUNGE

Tunapendekeza Baraza la Mawaziri lisitokane na wabunge kama ilivyo sasa. Hii inatokana na ukweli kuwa mara kwa mara kumetokea mgongano wa kimaslahi kwa mawaziri kupleka miradi mingi ya maendeleo katika majimbo yao ili kujijengea uhalali wa kuchaguliwa tena. Vile vile pendekezo hili linalenga kutenganisha utendaji wa mihimili miwili ya serikali na bunge. Hailet maana nzuri wabunge kuwa sehemu ya serikali (executive) kwani ile dhana ya mgawanyo wa madaraka ambayo ni muhimu katika kuhakikisha utendaji na ufanisi haionekani kuleta tija inayotengemewa katika mfumo huu tulionao wa mawaziri kuwa sehemu ya bunge.


viii. SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

Ili kutoa nafasi Aidha iwapo Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano atatoka upande mmoja wa Muungano bas swa katika pande zote za Muungano,ni bora nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iwe ya kupokezana kati ya Tanganyika na Zanziar. Naibu wake atoke upande wa pili. Katibu wa bunge pia iwapo atatoka upande mmoja wa Muungano naibu wake atoke upande wa pili wa Muungano.

ix. SPIKA WA GUNGE LA TANGANYIKA

Katika serikali ya Tanganyika kwa yale mambo ambayo si ya mungano tunapendekeza bunge la Tanganyika liwe na spika wake kwa kuzingatia uwiano kama tulivyopendekeza kwa nafasi ya urais wa Tangayika au uwepo utaratibu mwingine mallum unaofanana na huo.
Nafasi ya katibu wa bunge pia iwe kama katibu ni wa dini moja basi naibu wake awe kutoka dini nyingine.

x. WIZARA ZASERIKALI

Ili kuleta ufanisi na kumpunguzia Raisi majukumu na madaraka, ni bora muundo na idadi ya Wizara zikatamkwa moja kwa moja ndani ya Katiba badala ya utaratibu wa sasa wa wizara na idadi yake kutegemea matamshi ya Raisi.


xi. MAKAMU WA RAISI
Tunapendekeza kama serikali ya Tanganyika itakuwepo, nafasi ya Makamu wa raisiwa Tanganyika isiwepo na badala yake pawepo na Raisin a Waziri Mkuu tu. Utaratibu wa sasa wa kuwa na mgombea mwenza ambaye anakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano uondolewe na badala yake kama Raisi anatoka Zanzibar Raisi wa Tanganyika awe kwa mnafasi yake ni Makamu wa Raisi wa jamhuri na kinyume chake.
Ingawa kuna uwezekanao wa Raisi wa Muungano kutoka chama tofauti na chama cha Raisi wa upande wa muungano utakaostahili kutoa Makamu wa Raisi, mfumo huu ni mzzuri na wa lazima maana utakuwa umelinda maslahi na uwakilishi wa watu wengi katika upande wa Muungano unaohusika. Hilii pia itawzekana maana serikali ya Muungano itakuwa inahusika na masuala machache ya muungano wakati masuala mengi yakishughulikiwa na serikali zinazounda muungano.

xii. MANAIBU WAZIRI
Tungependekeza pia nafasi ya naibu Waziri kwa upande w serikali ya Tanganyika isiwepo maana inaongeza gharama bila sababu. Katibu Mkuu wa wizara anatosha.
Kwa upande wa serikali ya Muungano, nafasi hiyo iwepo ili kuleta uwakilishi sawa kutoka pande mbili za muungano. Na pale Waziri akitoka upande mmoja wa muungano, naibu wake atoke upande wa pili wa muungano.

xiii. SERA RASMI YA NCHI
Tunapendekeza sera ya nchi yetu iwe nisera ya kujenga ustawi wa jamii yaani “welfare state policy” badala ya sera ya ujamaa ambayo kivitendo haipo tena. Pendekezo hili linazingatia ukweli kuwa sasa nchi yetu ni ya kibepari. Hivyo basi sisi waislamu tunaona kuwa ni heri sera ya nchi yetu iwe ni kuimarisha ustawi wa kijamii yaani ili kuifanya serikali iweze kuwajibika zaidi kwa wananachi kuwawekea ustawi wa maisha yao.

xiv. BAADHI YA MSHARTI YA KUSAJILI VYAMA VYA SIASA YAONDLEWE
Kwa kuwa kila mtu ana uhuru w akujiunga au kutojiunga na chama chochote cha siasa alimradi havunji seria,masharti yafuatayo ya uanzishwaji wa vyama vya siasa yaondolewe;-

i. Sharti la kwamba chama cha siasa lazima kiwe na wanachama kwa Zanzibar na Bara liondolewe kwani linanyima uhuru na uchaguzi wa kujiunga na wengine kwani ridhaa ya mtu.
ii. Sharti lakuwa na wanachama mikoa 10 bara na 2 Zanzibar liondolewe kani linaleta ulazima kwenye jambo ambalo kimsingi ni hiari. Chama kisicho na wanachama kiachwe kife chenyewe kwa kukosa wanachama.
iii. Vyama vya kidini viruhusiwe ili wananchi waamue wenyewe kwa sera za chama na katika sanduku la kura. Hili linawezekana na kuna mifano hai kam avile Ujerumani, Australia, Uingereza, Cananda, DRC Congo, Denmark, Ufaransa, Italia, Rwanda, Ubeligiji, Afrika ya Kusini n.k kuna vyama vya kidini na wala hakuna matatizo yoyote.

xv. MAMLAKA YA RAISI Y APUNGUZWE
Japo mamlaka ya kutosha kwa Raisi ni muhimu kwa maslahi ya umma ili kumuwezesha kutekeleza majukumu yake makubwa kama Mkuu w aNchi na Dola, ni bora, kwa lengo la utawala boara na kulinda zaidi maslahi ya umma, madaraka ya Raisi yakapunguzwa katika maeneo yafuatayo;-

-
Raisi asiwe na mamlaka ya kuweka watu vizuizini bila ya kufikishw amahakamani na Kuhukumiwa kwa kuthibitihswa shutuma dhidi yake.
- Mamlaka ya Raisi ya kusamehe wafungwa yawe ni kwa mujibu wa vigezo maalumu vinavyotamkwa na sheria ya Bunge na iwe katika utaratibu ulio wazi.
-
Mamlaka ya Raisi ya kuunda idara mbalimbali za serikali pamoja na kteua wakurugenzi yatekelezwe kutokana na mapendekezo yatakayotolewa na Kamisheni ya Ajira na Idara za Serikaliitakyoundwa kw auwiano wa kimakundi ya kijamii.

xvi VYOMBO VYA UTEKELEZAJI WA SHEIRA, UPELELEZI NA UENDESHAJI WA MASHITAKA

a) Mkurugenzi wa mashtaka
Mamlaka ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) yanahitaji Kupunguzwa ili kuleta ufanisi na uwazi zaidi katika mfumo wa utekelezaji wa sheria. Kwa maoni yetu, pale kesi ya jinai itakapoanzishwa na taasisi nyingine au mtu binafsi, DPP asiwe na uwezo wa kudihinisha kesi hiyo kwenda au kutokwenda mahakamani, kuondoa mashitaka mahakamani wala kuingilia isipokuwa tukama atatoa sababu za kisheria zitakazomridhisha hakimu aJaji anayesikiliza kesi kwamba kuna mwnendo unaowezakupelekea haki kutokutendeka.
Katiba na sheria tulizonazo kwa sas zimetoamamlaka makubwa sana kwa Mkurugenzi wa Mahsitaka, kwani kwa mamlaka aliyonayo anao uwezo wa kuingilia au kufuta kesi yoyote iliyo mahakamani bila kulazimika kuto sababu yoyote na hakuna atakayemzuia kufanya hivyo. Hii imeleta maswhli na malalamiko mengi kuwa wapo watu wanaofaidika na mamlaka hayo makubwa ya DPP kutoweza kufikishwa Mahakamani kwa matendo yao.

b)
Taasisi ya kuzuia na kupambana narushwa (TAKUKURU)
Tunapendekeza ofisi ya Kikosi cha Kuzuia na Kuondoa rushwa Tanzania (Takukuru) itamkwe ndani ya Katiba na iwe na mamlaka kamili na huru katika kusimamia sheria ya kuzuia rushwa bila kuingiliwa na ofisi ya DPP. Utaratibu wa sasa wa baadhi ya makosa kuhitaji ridhaa ya DPP kabla ya kupelekwa Mahakamani yanaleta matatizo kutekelezaji na yanapunguza uhuru wa Takukuru. Ni bora pia, ili kuondoa muingiliano, sheria ya Takukuru ijihusishe na makosa makhsusi ambayo hayatamkwi katika Sheria ya Makosa ya Jinai (Penal Code). Na lau baadhi ya makosa katika Penal Codeyanastahili kuwemo katika sheria ya Takukuru , sheria ya penal Code irekebishwe kuyahamishia makosa hayo katika sheria ya Takukuru.

c)
Ofisi ya Mkurugezi na Mdhibiti Mkuu wa serikali (CAG)

Ili kuzuia ubadhilifu wa mali za umma ni bora ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali iwe na uwezo wa kutoa ushauri kwa mamlaka zinazohusika na mashitaka ya kushitakiwa au kumfungulia mashitaka yeyote atakayonekana kuwa na makosa kwenye taarifa hesabu za serikali. Na endapo vyombo husika vitakataa ushauri bila kuwa na sababu ya msingi kwa mtizamo wa Mkaguzi Mkuu, Sheria impe nguvu kulipeleka suala Mahakama Kuu ili iamue kam akuna haja ya kesi hiyo kufunguliwa.


d) Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Tunapendekeza utaratibu wa sasa wa Raisi kuunda tume ya Uchaguzi ubadilishwe badala yake iundwe na Chombo cha Kikatiba kitakachokuw akatika muundo unaozingatia uwiano wa maslahi ya kisiasa na kijamii. Hili litaondoa malalamiko kwamba Raisi anaunda Tume ya Uchaguzi kwa kuzingatia maslahi ya chama chake.


e)
Muundo w aTume ya Uchaguzi uwe wa kitaifa kuanzia chini hadi juu
Muundo w atume kipande unawafanya viongozi wa Serikali wa Kuteuliwa na Raisi kuwa watendaji wa misimu wa Tume na hivyo kuzua malalamiko mengi kwamba haifanyi kazi kw auhuru.


f)
Matokeo ya Kura za Urais
Katika iruhusumatokeo ya uchaguzi w aRaisi kupingwa katika Mahakama Kuu ya katiba.Ili kulinda usalama wan chi kesi hiyo itapaswa kufunguliwa ndani ya siku kumi na tano toka matokeo yalipotangazwa na kusikilizwa ndani ya siku thelathini.
Mara baada ya kesi hiyo kufunguliwa, Katiba itamke kwamba Raisi aliyemaliza muda wake atakaimu nafasi ya Raisi ili kutoa nafasi kesi kusikilizwa kwa uhuru. Pia Katiba iamke wazi kwamba, kabla kesi hiyo haijafunguliwa, Mahakama Kuu ya katiba itafanya upembuzi wa ushahidi uliopo kuona kama kuna sababu zozote za msingi za kufunguliwa kwa kesi. Utaratibu kuwa uamuzi wa mwisho hata kama kuna malalamiko ya msingi yanazua wasiwasi kuw ahaki haitendeki.

g)
Mgombea Binafsi.
Mgombea binafsi aruhusiwe katika nafasi zote isipokuwa nafasi ya Raisi. Mfumo wa sasa uanolazimisha mgombea kuwa na chama cha siasa unawanyima wananchi wasio na vyama vya siasa kushiriki katika uongozi wan chi wka kutumia haki yao yakuchagua na kuchaguliwa. Kwa upamde wa Raisi,mantiki ya kutaka wagomea wawe na vyama vya siasa ni kutoa nafasi ya kutosha kwa wananchi kutathimini sera vyama vyenye mgombea Urais ambazo ndizo zitakazotekelezwa na serikali itakayoundwa na Raisi atakayeshinda. Na pia kutoa nafasi kwa Tume ya Uhaguzi kutathimini sifa ya mgombea.Yawezekana mtu akajitokeza kuwa mgombea Uraisi na akawa na Sera inayopingana na Katiba na maadili ya nchi. Kuwa na chama cha siasa kutaifanya Tume kuchulia kwamba sera za mgombea ni kama zilivyo katika Katibana Sera ya chama chake.

h)
Mfumo wa serikali za majimbo urejeshwe
Katiba isiwe na nafasi za Mkuu wa Mkoa, Wilaya na badala yake kuwe na uongozi wa majimbo na viongozi wa majimbo hayo watoke katika majimbo hayo na wapiigiwe kura na wananchi wa majimbo husika.


i)
Uhusiano na Jumuiya za Kimataifa Usiwe na Kibaguzi
Katiba itamke kuwa Tanzania inaweza kujiunga au kuwa na uhusiano wa kibalozi, uanachama au vinginevyo na jumuiya yoyote yakimataifa pasi na kujali kama jumuiya hiyo ni ya kisiasa, kiuchumi, kijamii au za kidini alimradi kufanya hivyo itathibitika kuwa na maslahi kwa watanzania au sehemu ya watanzania.
Ni kwa msingi huu waislamu w aTanzania tunataka Tanzania ijiunge na OIC kama ambavyo ina uhusiano wa kibalozo na Papa ambaye ni kiongozi wa Dola ya Kidini ya Vatican ya Kanisa katoliki. Kama hili la kujiunga na OIC haliwezekani, bas iwe pia Ubalozi wa Vatican nchini Tanzania usiwepo kwa sababu ni ubaguzi wa kidini.

j) Mali za viongozi zihakikiwe kabla nabaada ya kutoa madarakani na CAG.
Katiba iweke utaratibu maalum kwa mali za viongozi kuhakikiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali (CAG) wakati wakuingia madarakani na wakati wakutoka badala ya tume ya Maadili ya Viongozi.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba wajumbe wa tume ya Maadili wengi wao wanaweza wasiwe na ujuzi wa kutathimini na kuhakikisha mali hivyo atumike CAG. Na iwe ni kosa la kisheria kukaidi utaratibu huo.

k)
Rasilimali za maeneo husika ziwanufaishe wenyeji wa maeneo husika
Katiba itamke kiwango ambacho wananchi wa maeneo yenye rasilimali kama vile gesi, madini n.k wanatakiwa wapatiwe kutoka kwa muwekezaji ili kuzuia kuhamisha mali kutoka eneo hilo kwenda kwingine au hata nje ya nchi bila wenyeji kunufaika.


I)
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uwe wa Mkataba
Katiba itamke kuwepo kwa Muungano wa mkataba na mambo yote ya Muungano yaliyoongezwa kutoka kwenye mkataba wa awali wa mwaka 1964 yapitiwe upya na pande zote husika.


HITIMISHO

Ndugu muislamu hii ni sehemu tu ya yale ya msingi kwa waislamu; yako mengine ambayo yanaweza kuongezwa wakati wa utoaji wa maoni, tafadhali muislam uwe huru kuyatoa mbele ya tume alimuradi hayapingani na maoni yetu ya msingi, vinginevyo pata ushauri zaidi toka kwa jukwaa la katiba la waislamu JUWAKATA;-
Simu ya M/Kiti wa Jukwaa – 0785 955 859/0715955859 Simu ya Makamu M/Kiti wa Jukwaa – 0784 863539 Simu ya M/Kiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanznaia – 0689 378747 Simu ya Makamu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu – 0715 631183

Sisi waislamu hatupaswi kutofautiana katika mambo ya msingi kwa ajili ya dini yetu. Tupo wanachama wa vyama mblimbali vya siasa, lakini tukiingia msikitini imamu wetu ni mmoja, hii ni fundisho kuwa sisi ni ummah mmoja. Tetea itikadi yako ya kisiasa alimuradi haipingani na dini yako. Itikadi ya kisiasa haipaswi kwenda kinyume na uislamu wako. Tafadhali jitambue na uutambue uislamu wako na uwe tayari kuutetea popote.

Baaada ya maelekezo haya, tunamuomba kila muislamu sasa kujifunga kibwebwe na kusimama kutekeleza jukumu lake kwa uwezo wake wote. Nia zetu ni njema katika kushiriki mchakato wa mabadiliko ya katiba Tanzania na Allah (Subhaanahu Wataala) ni shahidi wa nia zetu. Tunashirki ili kuona kwamba katiba inazingatia matakwa yetu nay a wengine yasiyo na madhara kwetu na haitoi nafasi ya mtu yoyote kunyanyaswa.
Ni wazi tutakapo simama na kudai haya tuliyoyasema tutasikia mengi kutoka kwa wale wote wasioutakia mema Uislam na waislamu.Wajibu wako wewe Muislamu kuitetea dini yako kwani kuna ujira mkubwa kesho mbele ya allah (SW). hautokuwa na udhuru wowote utakaposhindwa kusimama kuutetea uislamu wako kupitia mabadiliko ya katiba. Tumedhulumiwa kiasi cha kutosha ni wajibu wetu sasa TUSEME TUMECHOSHWA KUDHULUMIWA, TUNATAKA HAKE ZEETU NDANI YA KATIBA MPYA.

TAFADHALI SASA TIMIZA WAJIBU WAKO


Imeandikwa na:

Jukwaa la Waislamu la Kuratibu Mabadiliko ya Katiba
Tanzania (Juwakata) Dar es Salaam, Tanzania.
 
Juzi juzi tu huyu Ponda kazua kituko baada ya kuwashawishi wenzake kutojisajili kwenye madaftari ya wakazi katika zoezi la vitambulisho vya taifa akiwaambia hiyo ni sensa na ni janja ya serikalikuwahesabu kimtindo. Sasa watu wale wale waliogoma kuandikishwa, wapo bize kuwakimbilia makarani kila wanapowaona mitaani wakiwaomba wawaandikishe.

Nyie muigeni Ponda, mnyarwanda huyo atarudi kwao wakati nyie kwenu hamtambuliki.

Hii adhabu ya kifo sijui kwa nini inashabikiwa na uislamu. Hapa kigezo ni kisasi na si vinginevyo. Fuatilia akili ya Ponda anayoitumia kuwasemea walioamua kukubali awasemee halafu jiulize hili; KWA LEVEL YETU YA INTALLIJENSIA, NI MARA NGAPI MTU AMEHUKUMIWA KWA KOSA AMBALO HAKUFANYA?

Ponda yeye anataka ukihukumiwa leo kesho unyongwe bila kujali ubora wa hukumu. Ni kawaida ya mujahidina hawa na ndio utaona huko uarabuni anahukumiwa mwanamke kwa uzinzi ilhali wanaume aliozini nao wamo katika group la warusha mawe kwenye utekelezaji wa adhabu ya kifo.

Ponda na wenzio, Tanzania si MWANACHAMA wa VATICAN, bali ina uhusiano wa kibalozi na Vatican. Hii ni sawa tu na Tanzania ilivyo na uhusiano wa kibalozi na jamhuri ya kiislamu ya Iran. Sasa sijui ulinganifu wa madai yenu na mifano yenu uko wapi.

Jamani eeh, mwenye akili na aitumie isioze. Hivi Wakristo wanasali Jumapili kwa kuwa Jumapili ni siku ya mapumziko au Jumapili ni siku ya Ukristo? Jumapili was just named PUBLIC HOLIDAY, kwa hiyo Wakristo wameamua kuitumia kufanya DONIMICA lkn hawa wasiojua maana ya jambo wanaona kuwa serikali imeifuata siku. Sio hivyo Ponda usiye na hoja, ni Wakristo wameamua kuitumia Jumapili kusali. Hakuna sehemu kwenye Bible imeelekezwa tusali jumapili, tunasali kila siku ila kwa kuwa Jumapili ni siku ya mapumziko, tunafanya Dominica. Hata ukihamishia siku ya mapumziko iwe jumatatu, sisi tutafanya Dominica. Ukiwa na akili utagundua kila siku ya mapumziko tunafanya Dominica. Mwaka mpya hata uwe jumakumi, tunafanya Dominica.
 
Chonde chode jamani msije choma tena makanisa tu, manake mkishaanza hivi tu, ujue kishanuka

Somalia, Nigeria, Palestina, Iraq, Iran, Zanzibar (just mentioning few). Freedom of worship not of warship
kwa miaka ya karibuni ni kweli baadhi ya makundi ya kidini yamekuwa hayafuati si sheria za nchi wanamoishi tu bali hata sheria mama za dini zao ...ambapo nadhani ni Upendo na Umoja!

Katika hali kama hii, wengi wetu hatuna jinsi ya kuchukulia hii hali zaidi ya ku-generalize kwa maana ni vigumu sana kuwaamini hawa watu wana nia gani hasa (kati ya nzuri au mbaya - ku-utilize au misuse) hizi taarifa. Mfano mtu ambaye anasema kama Waislamu ni 70% na kutaka asilimia hiyo hiyo ionekane kwenye ajira za umma, shule nk.

Kwa kifupi ni kuwa kuwa na kipengele kinachojua dini za watu sio kitu kibaya maana kuna baadhi ya minority groups pia nazo zaweza kuwa identified katika huu mlolongo badala ya kutegemea taarifa za kwenye Weekpedia, BBC, Al-Jazeera na CNN. Ni bora kiwepo tu maana wengine wanaofia lakini inaweza kuishia kwenye 'quantitative' badala ya 'qualitative'.

Dawa ni chungu lakini inatibu hivyo siku za mbeleni ni lazima kitajumuishwa, ni bora kuwahi tu. isije kuwa kama story ya Mh. Magufuli na jengo la TANESCO-Ubungo kuwa hata asipolibomoa yeye labda wapindishe sheria

 
Hii ni "extreme writting", huyu mtu ameandika kama mtu anayeongea kwa mdomo.
Nimenukuu hapa "Kutokana na Katiba iliyopo imechangia kuwaathiri Waislam kiimami, kiuchumi na kijamii. Waislam tumekosa....haki ya uwakilishi Bungeni, haki ya kuwa na mfumo wetu wa elimu, haki ya kuwa na usawa katika miliki ya ardhi, haki ya usawa katika uteuzi mbalimbali za uongozi wa nchi, haki ya kuheshimiwa sheria za kiislam n.k".
MTIZAMO WANGU: muda si mrefu hawa watu wataandamana wakidai: kuangalia TV, kujengea makaburi na sehemu za kitalii, kucheza mpira wa miguu, n.k ni kinyume na sheria za Kiislam.
 
Nimesoma maoni yao yote naona hakuna kipya, na Bado wanalalamika na hata wakichukua maoni yao yote na kila kitu waongoze wao bado watalalamika, hawa watu hawawezi kufikiri na ndio maana hawaachi kulalamika. Angalia Watu wanaokipigia kura ccm ni wao, na niwao wanao lalamika ccm imewabagua Na hata iwe vipi ccm inategemea saana kura zao kwakua inalijua kundi hili kuwa linawatu wasiojitambua, Sasa angalia wanavyoshindana kuanzisha makundi, wenyewe wenye akilizao wanasomesha watoto kwenye shule nzuri wao wako kwenye mambo yasiyo natija, kesho ooh nafasi sawa bila elimu, wapo karine ya 10 bado,
Juzi juzi tu huyu Ponda kazua kituko baada ya kuwashawishi wenzake kutojisajili kwenye madaftari ya wakazi katika zoezi la vitambulisho vya taifa akiwaambia hiyo ni sensa na ni janja ya serikalikuwahesabu kimtindo. Sasa watu wale wale waliogoma kuandikishwa, wapo bize kuwakimbilia makarani kila wanapowaona mitaani wakiwaomba wawaandikishe.

Nyie muigeni Ponda, mnyarwanda huyo atarudi kwao wakati nyie kwenu hamtambuliki.

Hii adhabu ya kifo sijui kwa nini inashabikiwa na uislamu. Hapa kigezo ni kisasi na si vinginevyo. Fuatilia akili ya Ponda anayoitumia kuwasemea walioamua kukubali awasemee halafu jiulize hili; KWA LEVEL YETU YA INTALLIJENSIA, NI MARA NGAPI MTU AMEHUKUMIWA KWA KOSA AMBALO HAKUFANYA?

Ponda yeye anataka ukihukumiwa leo kesho unyongwe bila kujali ubora wa hukumu. Ni kawaida ya mujahidina hawa na ndio utaona huko uarabuni anahukumiwa mwanamke kwa uzinzi ilhali wanaume aliozini nao wamo katika group la warusha mawe kwenye utekelezaji wa adhabu ya kifo.

Ponda na wenzio, Tanzania si MWANACHAMA wa VATICAN, bali ina uhusiano wa kibalozi na Vatican. Hii ni sawa tu na Tanzania ilivyo na uhusiano wa kibalozi na jamhuri ya kiislamu ya Iran. Sasa sijui ulinganifu wa madai yenu na mifano yenu uko wapi.

Jamani eeh, mwenye akili na aitumie isioze. Hivi Wakristo wanasali Jumapili kwa kuwa Jumapili ni siku ya mapumziko au Jumapili ni siku ya Ukristo? Jumapili was just named PUBLIC HOLIDAY, kwa hiyo Wakristo wameamua kuitumia kufanya DONIMICA lkn hawa wasiojua maana ya jambo wanaona kuwa serikali imeifuata siku. Sio hivyo Ponda usiye na hoja, ni Wakristo wameamua kuitumia Jumapili kusali. Hakuna sehemu kwenye Bible imeelekezwa tusali jumapili, tunasali kila siku ila kwa kuwa Jumapili ni siku ya mapumziko, tunafanya Dominica. Hata ukihamishia siku ya mapumziko iwe jumatatu, sisi tutafanya Dominica. Ukiwa na akili utagundua kila siku ya mapumziko tunafanya Dominica. Mwaka mpya hata uwe jumakumi, tunafanya Dominica.
 
Hapa nisawa na uchukue mpunga ulushe kenye kundi la kuku, watushambuliaje! nimeptia comment za watu mbalimbali wote kila mtu anaponda na kutukana kwa kadri ya uwezo. SWALI: je yanakuhusu? MAONI: kama yanakuhusu toa mchango wa maana. over!!!!!!!!!!!!!!
 
1. Mahakama ya kadhi
2. Mfumo kristo unaokandamiza waislam uondolewe
3. Nyama ya ng'ombe ichinjwe na waislam pekee
4. Siku ya ijumaa watu wasiende kazini kama jumapili AMA SIVYO Jumapili pia watu waende kazini
5. Mabasi ya mikoani yaache kupiga nyimbo za kikristo peke yake safarini bali yawe yanapiga na kaswida

ONGEZEA MADAI MENGINE KISHA TUYACHAMBUE KWA KINA..... Kiroho safi jamani
 
Nadhani nitapinga hiyo no 5.......anaeamua nyimbo za namna gani zipigwe ndani ya basi ni nani? Na kama nyimbo hazikuvutii usipande hilo basi.......hujalazimishwa....basi ni mali ya mtu binafsi......ingekuwa ya serikali sawa........
 
1. Mahakama ya kadhi
2. Mfumo kristo unaokandamiza waislam uondolewe
3. Nyama ya ng'ombe ichinjwe na waislam pekee
4. Siku ya ijumaa watu wasiende kazini kama jumapili AMA SIVYO Jumapili pia watu waende kazini
5. Mabasi ya mikoani yaache kupiga nyimbo za kikristo peke yake safarini bali yawe yanapiga na kaswida

ONGEZEA MADAI MENGINE KISHA TUYACHAMBUE KWA KINA..... Kiroho safi jamani

shule ya secondary ya kinondoni wanafunzi wawe wanafaulu kama st Mirian ya Bagamoyo
 
kwakua madai hayo wanaidai serikali ambayo imeundwa na dini zote.....sisi wakristo hatuna haki ya kuwajibu madai yao....kilichopo ni kuelimishana......kuvumiliana, kusamehe na kumrudia mola wetu katika kipindi hiki kigumu cha kuchonganishwa baina yetu kwa manufaa ya wachache.

Tayari dini hizi tumeshaoleana, na bado tunaoana...chuki hizi tujue ni watu wachache kwa manufaaa yao...waislamu wengi niwajuao ni watu wazuri sana, kama ilivyo kwa baadhi ya wakristo......wachache wasitugawe.
 
hii thread haina tija, haya ni marufidio, kuna thred zipo zimeorozesha madai ya waislam kwa asilimia kubwa, huu unaoleta wewe ni ushabiki mods please...!
 
1. Mahakama ya kadhi
2. Mfumo kristo unaokandamiza waislam uondolewe
3. Nyama ya ng'ombe ichinjwe na waislam pekee
4. Siku ya ijumaa watu wasiende kazini kama jumapili AMA SIVYO Jumapili pia watu waende kazini
5. Mabasi ya mikoani yaache kupiga nyimbo za kikristo peke yake safarini bali yawe yanapiga na kaswida

ONGEZEA MADAI MENGINE KISHA TUYACHAMBUE KWA KINA..... Kiroho safi jamani

umesikia huko Pakstan leo Waislamu wa SUNI wamewaua waislamu wa madhehebu ya Shia 90 katika bomu la kujioa MUHANGA.

Wanadai nini kwa Waislamu wenzao?
 
Nadhani nitapinga hiyo no 5.......anaeamua nyimbo za namna gani zipigwe ndani ya basi ni nani? Na kama nyimbo hazikuvutii usipande hilo basi.......hujalazimishwa....basi ni mali ya mtu binafsi......ingekuwa ya serikali sawa........

Fafanua na hizo unazoafiki moja baada ya nyingine basi!
 
umesikia huko Pakstan leo Waislamu wa SUNI wamewaua waislamu wa madhehebu ya Shia 90 katika bomu la kujioa MUHANGA.

Wanadai nini kwa Waislamu wenzao?

Hivi kuuwa binadamu mwenzako nako ni IBADA au SUNA? Nauliza tu jamani mnao juwa!!!
 
Back
Top Bottom