Kinana Baba yake ni Msomali na Mama yake ni Mtanzania nadhani alizaliwa Nduruma Arusha na alikuwa Monduli wakati huo Chuo cha Taifa cha Uongozi (CTU) akiwa akiwa Kamisaa wa Siasa (Political Education Officer).
Warya Kinana amechelewa kujitetea....Kila kitu kipo wazi,atajificha wapi wakimueleza kuwa wanawafahamu hata wale vijana wa Ngaramtoni wanaowatuma kuwinda hao Wanyama?Ugomvi hapa sio nani mmiliki wa SSA bali mzigo unaosafirishwa na SSA ni wa nani?......Bado Tanzania tuna safari ndefu hawa viongozi wetu ndio wanaofanya kila uovu.Kinana si Mmiliki tu wa Sharaf pia ndiye mtu ambaye anahusika na hizo Nyara zilizokatwa Singapore!
Ukishangaa ya musa uatayaona ya firauni. Unashangaa kinana kuwa na meli?
duh, JF ina data si mchezo, nimeperuzi na kujifunza mambo kibao kwenye hii topic, watu wanatembea na mafaili ya data. thanks
Mhhh nchi za wenzetu mtu anajiuzuru kwa kashfa ya namna hii, ila kwetu mhhh si unaona mzee vijisenti wamemlinda weee mpaka Mungu kamuumbua na kesi ya kugonga bajaj, sasa wamtetee na hapo
Nakumbuka Kinana aliwahi kusemekana kuwa sio raia wa Tanzania wakati fulani. Ikabidi aachane na siasa na kwenda kusoma Marekani. Sijui kama ameshaupata uraia. Lakini hata kama hajaupata, kuhakikisha tu kuwa anashiriki kwenye kampeni za Rais kama mwenyekiti wa Kampeni kunampa madaraka ndani ya chama chake na kumfanya mtu muhimu kwa Taifa. Kaaaazi kweli kweli.