Abdulrahman Kinana asamehewa, Bernard Membe afukuzwa rasmi CCM

Membe alikuwa anadai Halmashauri kuu pekee ndo ina mamlaka ya kumfukuza uanachama na si kamati kuu,sasa kuweka kumbukumbu sawa hao aliowataka wagonge msumari ndo hao wamehitimisha ili asije kujifaragua baadae!

Akijitahidi sana ku-survive nje ya CCM ni miaka mitano.

Kwanza,atapoteza marafiki wa muda mrefu.

Pili, atapoteza washirika muhimu na wa siku zote.

Tatu,atakosa kilichompeleka huko aendako.

Nne,ata-swallow his pride na kurudi alikotoka.

Imeisha hiyo!!!
Tano atapongezwa sana baada ya kumaliza kazi aliyotumwa.
 
Pinga sheria kandamizi ukiwa huru ili ukiwa mfungwa ikufae, walipokuwa kwenye sytem tuliwaambia tengenezeni katiba Bora ili siku mkiwa raia baada ya mfumo kuwatupeni itakusaidieni wakaweka pamba Leo wamekuwa raia nao wanalia.
Afrika mfumo ukishakutupa huna chako waweza fanywa chochote na waliopo kwenye mfumo hivo hivo.

Tatizo sio Katiba.

Katiba inasema kila raia ana haki ya faragha.

Mbona tunadukuliwa ????

Hiyo Katiba mpya itatumia lugha gani ili ieleweke, iwe enforced, iseme nini hiyo Katiba?
 
Kwani kuna habari gani?
IMG-20220331-WA0483.jpg
 


Halmashauri kuu ya CCM imemsamehe Katibu mkuu mstaafu kanali Kinana ambaye alipewa onyo kali na kuwekwa katika matazamio.

Halmashauri kuu pia imemfukuza kabisa yule mwingine ( Membe) ambaye hakufanya juhudi yoyote ya kuomba msamaha.
Membe alirudisha kadi yake CCM badala ya kutubu.

Maendeleo hayana vyama!

======

View attachment 1502881
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana

Akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM cha kumteua mgombea Urais wa Zanzibar, Rais Magufuli amsamehe aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana. Rais Magufuli amesema:

Ilikuwa mwezi wa wa pili Central Committee iliamua kutoa adhabu kwa baadhi ya wanachama wetu ambao walikiuka maadili na misingi ya chama chetu.

Kikao kile kilitoa mapendekezo ya adhabu kwa baadhi ya wanachama wetu kutokana na misingi na Katiba halali ya chama chetu. Lakini ni hivi karibuni baada ya miezi kama minne au mitano, mwenzetu mmoja ambaye ni Former Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi alijitokeza hadharani kule Arusha, na nafikiri shahidi ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha – akaomba radhi., akajutia kwa kitendo alichokifanya. Na kikubwa zaidi, ndugu yetu huyu aliomba radhi hadharani.

Ni kitendo kigumu sana kwa mtu kukifanya. Kinahitaji nguvu ya Mwenyezi Mungu tu kutubu hadharani. Mimi alinigusa sana. Nina uhakika hata ninyi wajumbe mliguswa sana. Alikuwa amepewa adhabu ya miezi 18. Hakukataa kutumikia adhabu ile.

Sasa niliona Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama tawala, chama chenye huruma. Chama chenye mapenzi mema. Chama dume. Niwaombe kwa huruma yenu kama itawezekana, huyu ndugu yetu ambaye amekubali mpaka sasa kutumikia adhhabu miezi mine, tumsamehe.

Kupitia kikao hiki napenda kusema Abdulrahman Omari Kinana amesamehewa rasmi. Niwashukuru wajumbe wa kikao hiki kwa huruma ya upendo.

Yule mwingine ambaye hata jina lake sitaki kulitaja yeye ameshaondoka moja kwa moja. Adhabu yake si mnaikubali?

Zaidi, soma:

1). Imevuja sauti inayodaiwa ni Maongezi ya Simu ya Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana kuhusu njama za kuichafua CCM

2). CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

3). Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja

Mwenye nguvu mpishe
 
Back
Top Bottom