Abdulrahman Kinana asamehewa, Bernard Membe afukuzwa rasmi CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
36,637
2,000

Halmashauri kuu ya CCM imemsamehe Katibu mkuu mstaafu kanali Kinana ambaye alipewa onyo kali na kuwekwa katika matazamio.

Halmashauri kuu pia imemfukuza kabisa yule mwingine ( Membe) ambaye hakufanya juhudi yoyote ya kuomba msamaha.
Membe alirudisha kadi yake CCM badala ya kutubu.

Maendeleo hayana vyama!

======

25.jpg

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana

Akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM cha kumteua mgombea Urais wa Zanzibar, Rais Magufuli amsamehe aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana. Rais Magufuli amesema:

Ilikuwa mwezi wa wa pili Central Committee iliamua kutoa adhabu kwa baadhi ya wanachama wetu ambao walikiuka maadili na misingi ya chama chetu.

Kikao kile kilitoa mapendekezo ya adhabu kwa baadhi ya wanachama wetu kutokana na misingi na Katiba halali ya chama chetu. Lakini ni hivi karibuni baada ya miezi kama minne au mitano, mwenzetu mmoja ambaye ni Former Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi alijitokeza hadharani kule Arusha, na nafikiri shahidi ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha – akaomba radhi., akajutia kwa kitendo alichokifanya. Na kikubwa zaidi, ndugu yetu huyu aliomba radhi hadharani.

Ni kitendo kigumu sana kwa mtu kukifanya. Kinahitaji nguvu ya Mwenyezi Mungu tu kutubu hadharani. Mimi alinigusa sana. Nina uhakika hata ninyi wajumbe mliguswa sana. Alikuwa amepewa adhabu ya miezi 18. Hakukataa kutumikia adhabu ile.

Sasa niliona Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama tawala, chama chenye huruma. Chama chenye mapenzi mema. Chama dume. Niwaombe kwa huruma yenu kama itawezekana, huyu ndugu yetu ambaye amekubali mpaka sasa kutumikia adhhabu miezi mine, tumsamehe.

Kupitia kikao hiki napenda kusema Abdulrahman Omari Kinana amesamehewa rasmi. Niwashukuru wajumbe wa kikao hiki kwa huruma ya upendo.

Yule mwingine ambaye hata jina lake sitaki kulitaja yeye ameshaondoka moja kwa moja. Adhabu yake si mnaikubali?

Zaidi, soma:

1). Imevuja sauti inayodaiwa ni Maongezi ya Simu ya Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana kuhusu njama za kuichafua CCM

2). CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

3). Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja
 

Wuondruok

Senior Member
Jul 2, 2019
127
250
Kutubu bila kosa nako ni utumwa,ni heshima kufukuzwa kuliko kuomba msamaha kwa kosa ambalo halikuwa kosa ukabaki na heshima yako utahesabika ni shujaa asiyeendekeza njaa.

Siyo kila Vita inayokujia ni lazima ushindane, sometimes ni vema uka surrender kwa manufaa ya baadae. Lowassa mwenyewe karudi CCM ila pengine si kwa ajili yake binafsi bali pia kwa kizazi chake maana Siasa za kiafrica huwa hazina mipaka, hata maisha yako binafsi yataingiliwa kukudhoofisha.

MEMBE ujeuri utamponza maana kiuhalisia bado ana kundi lake kubwa CCM AMBALO lingemchagua pengine 2025 ambapo itakuwa ni kama gombania goli kwa watia nia ya Urais Kupitia CCM ila kwa sasa anajisumbua tu.

Ni imani yangu hata kipindi hiki IKITOKEA Kura ya maoni, MEMBE anaweza mpiga chini MAGUFULI maana CCM wengi wanaojifanya kumuunga mkono Rais ni wanafki kwakuwa ndo hao hao waliokuwepo nchi ikitafunwa na wachache.
 

tweenty4seven

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
11,657
2,000
Halmashauri kuu ya CCM imemsamehe Katibu mkuu mstaafu kanali Kinana ambaye alipewa onyo kali na kuwekwa katika matazamio.

Halmashauri kuu pia imemfukuza kabisa yule mwingine ( Membe) ambaye hakufanya juhudi yoyote ya kuomba msamaha.
Membe alirudisha kadi yake CCM badala ya kutubu.

Maendeleo hayana vyama!
Hivi nani alimpa sumu mangula,mana jirani yake siku ya tukio alikua bossccm kuna watu roho za kichawi zimewajaa
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,005
2,000
johnthebaptist,

Kinana hakuwa na option nyingine zaidi ya kuwapigia magoti; ana makandokando mengi mno hasa baada ya ile tume ya CCM ya kusaka Mali zao kumuweka red corner.

Angegoma basi file lake ningefika kwa pirato yawe mengine.
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
36,637
2,000
Kinana hakuwa na option nyingine zaidi ya kuwapigia magoti; ana makandokando mengi mno hasa baada ya ile tume ya CCM ya kusaka Mali zao kumuweka red corner.

Angegoma basi file lake ningefika kwa pirato yawe mengine.
Kuomba msamaha ni uungwana bwashee!
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,765
2,000
Mbona mnajitoa ufahamu kama mmezaliwa leo? Membe alifukuzwa na kamati kuu..
Kamati kuu haina mamlaka ya kufukuza. Inatoa pendekezo tu. Kama mtu keshajitoa mwenyewe, the so called mkutano mkuu hauna haja ya kumjadiri tena na hilo pendekezo linakuwa halina mantiki (overtaken by events...)

Simple logic ila zwazwa hawezi elewa hii
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom