MWAMPOSA NA BIASHARA YA UPAKO:
Ukisoma habari za yule Simoni aliyekuwa mchawi, neno linasema, “Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka” (Matendo 8:13).
Ukiendelea kusoma, neno linasema, “Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono na mitume, akataka kuwapa fedha akisema, Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu” (Matendo 8:18—19).
Kwa lugha nyingine, Simoni alitaka “kununua upako.” Yesu alipokuwa anawapa upako wanafunzi wake, alisema, “mmepata bure, toeni bure” (Mathayo 10:8b).
Ukishaona nabii au mtumishi anafanya biashara ya “kuuza upako,” huyo ni “mtumishi wa Shetani.” Roho Mtakatifu hawezi kuongoza watu kuuza upako kwani Biblia inasema, Roho Mtakatifu anagawa karama mbalimbali kwa kadri apendavyo (1 Wakorintho 12:4—11).
Ukiona watu wanauza “maji ya upako, mafuta ya upako, sabuni za upako, kitambaa cha upako n.k.,” hiyo inatakiwa ikuambie kuwa hao wanatokana na Shetani. Ukifatilia, huo upako hautokani na Roho Mtakatifu, bali Lucifer.
Kuna madhara makubwa sana ya kununua hivi vitu kwani unapovinunua, unajiunganisha na miungu yao na Shetani anakuwa na uhalali wa kufunga maisha yako. Kwenye Biblia hamna “biashara ya upako” ila hii ni mbinu ambayo watumishi wa Shetani wanaitumia kupata fedha nyingi.
Kuna mtu mmoja alinunua mafuta ya upako kwa nabii mmoja mkubwa wa uongo wa Nigeria na baada ya hapo, aliona mambo ya ajabu.
NDIO MAANA WENGI WANAOENDA KWA HUYU TAPELI WAMESHAKUWA BRAINWASHED , HAWAJAITAMBUI
NB: ZAMAN UCHAWI ULIKUWA LOCAL SANA , SIKU HIZI UCHAWI UNAENDA NA WAKATI , UVHAWI KATIKA SIKU ZA MWISHO UMEVAA VAZI LA DINI