Abdallah Majura auza radio station

masare

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,210
1,322
Sasa ni rasmi kituo cha redio 91.2 ABM Radio cha Dodoma kilichokua kikimilikiwa na galacha wa fani ya utangazaji wa Radio ndugu Abdallah Majura kimeuzwa kwa Mtumishi wa Mungu Apostle Boniface "Bulldozer" Mwamposa na kwa sasa zinapigwa nyimbo za Gospel 24/7.

Ieleweke kwamba ndugu Abdallah Majura anamiliki pia radio station nyingine kwa jina la A24 Radio inayosikika Dar Es Salaam na Zanzibar.

Ninatumaini Mtumishi Mwamposa atatumia nafasi hii ya umiliki wa kituo cha Radio "kuwakamata" wakristo pamoja na wasio wakristo kama ambavyo amefanikiwa kwenye matamasha anayoyafanya Dar Es Salaam.

*INUKA UANGAZE*
 
Hahaha! Kuna watu wakikusikia watakuita pepo.
Nawataka waje hapa

Tumuweke kwenye mizani ya Biblia huyo tapeli mwamposa kutoka Mwanzo hadi ufunuo

Kama hatujamkuta ni mwizi tu,

Nilimuuliza Mfuasi mmoja wa mwamposa , aliyenunua mafuta maji ,

Kama ni nabii wa kweli mwenye upako kwa Maji na sio mjasiriadini ,kwann asiyawekee upako maji ya kwenye mto mkachota bure. Au msiende na maji yenu akayabariki , maana Mungu si amemtuma na Mungu amesema tumepewa bure tutoe bure

Hata Manabii wa zaman kina Isaya,Yeremia mwana wa hilkia , Ezekiel kuhani, musa, Amos,Obadia , Nehemiah , hatukuwahi kusikia wanafanya biashara kwenye matatizo ya watu.
 
Back
Top Bottom