A Program Note: Tutaweka Hoja Zetu Wazi

Namheshimu sana Dr SLAA ,naamini ni mapumziko ya muda tu ya kimkakati.mapambano ya kuing'oa ccm yapo palepale.viva UKAWA viva CDM.
Kweli kabisa mkuu
Wala kelele za chura hazimzuwi ngombe kunywa maji!
Chadema ni mpango wa mungu!
Wa Tanzania hatuhitaji ngonjera nyingi kwa muda huu!
 
Mimi napenda kuwa muwazi, ni muumini wadhati wa CCM, ila si mwanachama. Humu kwenye jamvi huwa tuaonesha hisia zetu zaidi, na pengine tunapindisha ukweli.Nilipo msikia mbowe kwa kauli iliyo onyesha wazi imeficha jambo zito ndani yake, kauli iliyo thibitisha hayo ni ile alipo sema chama lazima kisonge mbele bila kujali uwepo wa Slaa, Baregu na Mbowe. Kwa kauli hii inatosha kusema kuwa hata iledhamana mliyopewa na wananchi sasa inarudi kwa CCM. Silaha za kuzitumia tunazo
 
Mkuu
with serious note!

"Hatukukaa kimya kwa watawala walioshindwa wa sasa, na hatuwezi kukaa kimya kwa wanaotaka kuwa wa kesho" MM

Mkuu nimekuuliza una Agenda gani ya siri ambayo hutaki ifahamike?

KWANINI SASA NA SI WAKATI ULE?

Je wadhani watanzania wengi wa sasa wangali na akili za kushikiwa?

SIASA NA UANAHARAKATI NI VITU MBALIMBALI, NARUDIA TENA "HAKUNA ANAETAKA BIASHARA YA HASARA" NA UKITAKA UKWELI ZAIDI HAKUNA YEYOTE ALIYEWAHI KUWA CCM AKAWA MSAFI.

NA JE UNA MAANA MHESHIMIWA DR. SLAA WAKATI ANAGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA ALIPOTOKA CCM CDM HAWAKUWA NA MGOMBEA?

KAMATI KUU YA CDM SI WENDAWAZIMU, JE MZEE BAREGU NA PRO. SAFARI UNAWAZIDI MAARIFA?

TUNAAMBIWA TUITAZAME AIBU YETU KABLA YA KUISEMA YA WENGINE.

Wakatabahu
 
Mbona mnalialia kwani nyie mmejipangaje? Nyie tulieni atoe hoja.
Kati ya zitto na team mbowe nani wameisaliti cdm kimisingi

Tumetoka huko tunatafuta NJIA SALAMA ya kupita.Usiturudishe nyuma tena
 
Pasco your right 100% waache wasuse sisi tunaendelea hakuna namna ccm out 2015 nilazima kwa afya ya nchi yetu mama Tanzania .
 

Wewe endelea kuflash back .ngoja sisi tuingie field .maana wewe nakushangaa adui yupo mbele yako anasubiri pigo moja la mwisho ushinde vita .wewe unarudi unaanza kuflash back.ngoja baada 25 October tukirudi na ushindi tutakutunuku jina jipya .Mzee wa kuflash back .
 
Tusubiri tamko la kijasusi kutoka kwa wanaojifanya wenye chama hata kama wanaharibu. Huo ndo uwazi.

Tangu kipindi cha ZZK nilipata mshituko na CDM. Ni mwanachama ila macho yangu yanaangaza kila kitu kabla sijaamua kutenda.

mkuu ZZK mpaka leo wana muita msaliti wa chama, nimejifunza kitu kabla ya kumjia mtu juu ni vema nisikize pande zote mbili.la sivyo tutahukumu watu wasio na hatia
 
Hapana mkuu....si sawa kabisa....tuwe honest... wengine tuliwahukumu hatua kwa hatua....kwa mambo mengi.....hii case tusichanganye kabisa na wengine....tafadhali tuheshimu hilo.....
....huwa najiuliza iweje watu leo wanakua so sympathetic na Dr.Slaa alafu wanasahau yeye alivyosimamia kina Zitto kufukuzwa chadema.....na hapa wala Dr. hajafukuzwa hivyo...Ifike mahali tuwe fair bana....kama wanavyosema huko chadema hakuna aliye juu ya chama...hata awe dr.Slaa...
 
Hatuishi kwenye chama kwa sababu ulipigania ili ule matunda,wapo wengi duniani waliipigania kufyeka mapori,Lakini wanaokulamatunda niwajukuu!!

Chadema ni chama cha siasa,na siasa ni watu,tunahitaji watu kukisaidia chama kishinde madaraka,hatuhitaji mtu apiganie chama akusubiri kulipwa fadhila!!

Hata vitabu vya dini havisemi hivyo!
 

Katika mapambano vita vinapokuwa vikali ushindi ni karibu. Ninaamini kuwa uchaguzi wa mwaka huu 2015 unafungua historia mpya ya mapambano. Kama UKAWA watachukua nchi nao wakajifanya ni miungu tutawatoa kama tutakavyowatoa CCM. Mapambano na CCM yanahitaji silaha zote za maangamizi kama bomu la Nagasaki au Hiroshima. Baada ya kuwapiga kwa" nuclear bomb " lazima kutakuwa na makubaliano ya mustakabali wa nchi hii. Namkubali saaana Dr. na ninaheshimu maamuzi yake, lakini kipindi kilichosalia akubali tufumbe macho na pua tuvuke hadi ng'ambo. Kule ng'ambo kuna uponyaji utakaoponya nchi hii. Hakuna anayeweza kuzuia shauku ya watu wa nchi hii kupata ukombozi, hiki ni kipindi cha " leap forward".
 
MADA YENYEWE IKO HAPA TAFADHALI

PENDEKEZO LA MARIDHIANO

Mzee Mwanakijiji

CDM will go the same way NCCR did post-1995 election, specifically in 1997. Baada ya kushindwa uchaguzi hapo October 2015, CDM wataanza kulumbana na kutupiana mawe na kutimuana. Mwisho wa yote itakuwa kama Mrema na NCCR 1997 kule Tanga, Mkonge Hotel. Itachukua tena muda kuanzan kujenga any meaningful opposition wakati CCM wakitamalaki madarakani....

With Marando present in CC ya CDM (ambaye pia alikuwemo NCCR pale Mkonge Hotel 1997) and Apson eti mshauri wa mgombea wa CDM Lowassa the pattern is unfolding....CDM wanafuata script iliyoandikwa tayari.

CC:The Boss Pasco,
 
Only Blind and deaf will not see this wave!

Dr. Slaa is a hero but personal belief will not win you a political battle my brothers!
 
MM....kwavile Mungu kanipa akili....nitaitumia vyema.....haiwezekani tumpuuze Dr Slaa dakika hii.....wengine tunajua mapito yake....nitasimama nae......

Tuko pamoja mkuu. Moyo wangu umeumia sana. Nguvu ya pesa imevunja vunja misingi mikuu ya chama, hii hakubaliki. Kukaa kimya ni kubariki uharamia huu.
 

Hivi ni kwa nini CHADEMA wengi humu wanakuwa simple mind kiasi hiki? Hakuna tena logical reasoning zaidi ya kuongozwa na mihemko tu.
 
Mzee Mwanakijiji, tunasubiri kwa hamu kubwa kile mlichoandaa. Tuko wengi kuliko inavyodhaniwa, wale tuliokwazwa na kukatishwa tamaa na mabadiliko ya ghafla ya malengo ya msingi ya CHADEMA. Ukweli pekee ndio utakaokinusuru chama.
 
Last edited by a moderator:
Hayo ni mawazo yako na ofcourse ni sahihi kwako lakini mimi naona hayako sahihi !. Zitto tumeshaachana naye na this time tukishirikiana na vyama vingine katika UKAWA tutachukuwa utawala wa nchi hii.

Hao unaodai wanafikiria kula na wewe unayejiona ndio unafikiria maendeleo weight ya kura yako na zao inalingana !. Kura yako haina weight zaidi ya kura ya mtu mwingine. Its all about numbers and this time we have enough.....

WaTz wengi wakati huu, wameichoka CCM na wanaamini CDM na UKAWA na kwa kura zao tutawapiga chini CCM na kuunda serikali itakayoleta katiba mpya ya wananchi na kuweka mifumo itakayoleta haki kwa wananchi wote na hapo naamini maendeleo yanayoistahili Tanzania ndipo yatakapopatikana !

 

Mzee Mwanakijiji, nakumbuka kulikuwa na kanzi kako kanazunguka katika maeneo fulani, nilitumai kuwa mida hii katakuwa kamenusanusa zile kurasa tatno ambazo Dr Mwakyembe alikataa kuzisoma kwa kuogopa.

Sijui kama mbwenelehi walikimbia nazo au ka-nzi kanaweza kunusa. Ingekuwa vizuri ukitusaidia. Ni kama watu wanasahau Richmond ni nini, naona kuwa wanaweka jina moja tu wakati ilikuwa na majina mengi, au kwa kuwa RA alifungua vifungo vya gamba yeye amesahaulika? wengine je?

It sickens kusikia watu wanalalamikia fisadi mmoja wakati kuna wengine wengi tu.
 

MM KAA UKIJUA MBELE ZA HAKI wa saa 3 asubuhi saa 6 mchana na saa 12 jioni wote watalipwa ujira mmoja hakuna cha kujitetea eti mbona mimi nimefanya kazi tangu asubuhi na huyu kaja jioni halafu tunalipwa ujira sawa
 

Hakika umenena vyema sana mwamamichakato,mambo haya wanayotaka kuyaweka hadharani sasa ni kwa faida ya nani?Ninathamini sana michango ya wanachama wote wa CDM kuanzia viongozi wakuu na wanachama wa kawaida,ninaamini DR alishirikishwa hatua kwa hatua kwenye hili la kumpokea EL kama hawakuridhiana bado kulikuwa na nafasi ya kuendelea na maridhiano mpaka suluhisho lipatikane,leo hii naona malumbano yanaaza katikati ya mechi ikiendelea,kwa sisi wapenzi wa mpira kocha anaongea na players wake halftime wakiwa changing room,mkijibizana uwanjani katikati wakati mpira unaendelea ni kumpa adui yako nguvu ya kukupiga bao,tena la mkono alilosema Nape.Mzee Mwanakijiji nachelea kusema ya kuwa upinzani wetu bado sana na itatuchukua watanzania miaka nenda rudi kupata mabadiliko,nahisi wananchi tuko tayari ila viongozi wetu hamna dhamira ya dhati,nilifikiri wapinzani wakuu ambao wangevunja UKAWA na kumkataa EL ni CUF,jana nikamuona Duni Hadji(jembe)nikafarijika sana,ila ninaposoma hizi simulizi zenu nikakumbuka ile hadithi ya mwana mpotevu aliepewa sehemu ya urithi wake akaenda kutapanya na makahaba na ailiporejea kwa baba yake kutubu,yule nduguye muaminifu alikasirika aliposikia nduguye karejea na baba amemchinjia ndama alienona na amemfanyia sherehe,Dr hakupaswa kususa,muungwana hanuni kwa mashavu,hununa moyoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…