A Program Note: Tutaweka Hoja Zetu Wazi

A Program Note: Tutaweka Hoja Zetu Wazi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,095
Reaction score
43,307
Stay Tuned: Tunatarajia kutengeneza njia mahali hapa ambapo panaonekana hakuna njia. Siyo sahihi kuwaachia nchi na hatima ya nchi watu ambao hawakutoa hata tone moja la jasho kupigania mabadiliko ya siasa.

Iweje leo hii baada ya yote ambayo watu wamesimamia wengine kwa damu na wengine hata kwa uhai wao waje watu wavune wasichopanda kwa ahadi kuwa ati na sisi tutakula nao watakachovuna?

Kesho Inshallah, tutaweka hoja zetu wazi ili wao waamue kama wanataka kuungwa mkono nasi au la; hatutaki wao watuwekee masharti ya sisi kuwaunga wao mkono au kutupigisha mikwara ya kwanini tukae kimya ili wao wafanye wanalotaka.

Hatukukaa kimya kwa watawala walioshindwa wa sasa, na hatuwezi kukaa kimya kwa wanaotaka kuwa wa kesho!

MM

NB: Nitajaribu kutoa majibu ya hoja zilizotolewa na baadhi ya watu (ikiwemo ile mada ya Character X) kuhusiana na kuunga mkono hili la Lowassa.
 
Good luck on your mission...
Ila na wewe ulichangia 'kiburi hiki cha viongozi wa CHADEMA'

Hii si mara ya kwanza wanakiuka misingi wanayojifanya kuisimamia

si chadema ni chama cha demokrasia lakini uchaguzi tu wa mwenyekiti
watu hawakuruhusiwa? au umesahau?...
hii inayotokea inaitwa 'chicken come home to roost'

Mliponyamaza wakati haki za watu wengine zinanyimwa ndani ya CHADEMA na hadi kuunga
mkono 'watu wakiminywa'
kina Kafulila,Zitto na wengi wengineo the list is endless...haya ndo mavuno now
 
Mkuu MM pamoja sana Mkuu.

Tunatega masikio kusikia hilo Sharti ambalo naamini laweza kuwa Heshima kubwa kwa Chama chetu, Kwakweli wageni waje, tunawataka sana, Lakini kuja na kutuwekea masharti ambayo wanataka tuyafuate badala ya wao kufuata yetu, huo ni ukondoo..!!! Ni lazima tijitambue, Huwezi kumkaribisha mgeni mpaka chumbani bila masharti, kesho utasikia kalala na mkeo, utalalamika.

Wageni wanatakiwa kutambua, kunawatu walio-Struggle mpaka kuifikisha Cdm hapa ilipo, Hata kama wanapesa, wajue taasisi hiyo inehengwa mpaka kifika hapo ilipo kwa pesa za kuungaunga lakini iko ilipo mpaka kuwatamanisha. Nilazima watuheshimu..!!

BACK TANGANYIKA
 
Stay Tuned: Tunatarajia kutengeneza njia mahali hapa ambapo panaonekana hakuna njia. Siyo sahihi kuwaachia nchi na hatima ya nchi watu ambao hawakutoa hata tone moja la jasho kupigania mabadiliko ya siasa. Iweje leo hii baada ya yote ambayo watu wamesimamia wengine kwa damu na wengine hata kwa uhai wao waje watu wavune wasichopanda kwa ahadi kuwa ati na sisi tutakula nao watakachovuna? Kesho Inshallah, tutaweka hoja zetu wazi ili wao waamue kama wanataka kuungwa mkono nasi au la; hatutaki wao watuwekee masharti ya sisi kuwaunga wao mkono au kutupigisha mikwara ya kwanini tukae kimya ili wao wafanye wanalotaka.
Hatukukaa kimya kwa watawala walioshindwa wa sasa, na hatuwezi kukaa kimya kwa wanaotaka kuwa wa kesho!

MM

NB: Nitajaribu kutoa majibu ya hoja zilizotolewa na baadhi ya watu (ikiwemo ile mada ya Character X) kuhusiana na kuunga mkono hili la Lowassa.

Halafu isitoshe Fisadi Lowasa na wenzake ndiyo walikuwa wanatuma Jeshi la Polisi kuja kupiga na kujeruhi watu waliokuwa wamekusanyika, hivyo Fisadi Lowasa na wenz. wana damu ya wote walioumizwa, kulemazwa na hata kuuliwa na jeshi la Polisi hivyo kwangu mimi ni dhihaka kubwa sana klk zote kwa ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao leo hii kuona mtuhumiwa wao namba moja ndiyo anapigiwa kampeni eti ni mkombozi wao...
 
Good luck on your mission...
Ila na wewe ulichangia 'kiburi hiki cha viongozi wa CHADEMA'

Hii si mara ya kwanza wanakiuka misingi wanayojifanya kuisimamia

si chadema ni chama cha demokrasia lakini uchaguzi tu wa mwenyekiti
watu hawakuruhusiwa? au umesahau?...
hii inayotokea inaitwa 'chicken come home to roost'

Mliponyamaza wakati haki za watu wengine zinanyimwa ndani ya CHADEMA na hadi kuunga
mkono 'watu wakiminywa'
kina Kafulila,Zitto na wengi wengineo the list is endless...haya ndo mavuno now

Hapana mkuu....si sawa kabisa....tuwe honest... wengine tuliwahukumu hatua kwa hatua....kwa mambo mengi.....hii case tusichanganye kabisa na wengine....tafadhali tuheshimu hilo.....
 
01-Lowasa.jpg
 
Hekima,Busara,Heshima,Utu,Uzalendo,unyenyekevu,na Maono vyatakiwa sana wakati huu kuliko wakati mwingine wowote..Ugomvi wa baba na mama wenye hekima uishia chumbani si mpaka watoto na majirani wajue...Maridhiano yapewe nafasi kwa upendo na uzalendo kwa chama na taifa..tuinuke wamoja,tutembee wamoja,tukimbie mchakamchaka wamoja na tukaketi nchi ya ahadi pamoja!!!! Hakuna Lisilowekana kwa waaminio ktk haki,Kweli,Maridhiano na ushindi...
 
Tusubiri tamko la kijasusi kutoka kwa wanaojifanya wenye chama hata kama wanaharibu. Huo ndo uwazi.

Tangu kipindi cha ZZK nilipata mshituko na CDM. Ni mwanachama ila macho yangu yanaangaza kila kitu kabla sijaamua kutenda.
 
Hapana mkuu....si sawa kabisa....tuwe honest... wengine tuliwahukumu hatua kwa hatua....kwa mambo mengi.....hii case tusichanganye kabisa na wengine....tafadhali tuheshimu hilo.....

Nafikiri unamaanisha ya Zitto kufukuzwa
mimi sikulitaja hilo
mimi nalitaja la Zitto kuzuiwa kugombea uenyekiti
msingi wa demokraia ilikuwa wamshinde kwa hoja na kushawishi wanachama wasimchague
lakini sio kumzuia hata kugombea tu,wakati chama ni cha kidemokrasia

Huo ni mmoja wa mifano ambapo chama kiliuka misingi yake yenyewe tu inayojitangaza kuisimamia
na suala la Kafulila pia....tena Slaa huyu huyu ndo alikuwa jeuri kwa Kafulila...

Mkikiuka misingi kwa kuwatazama watu na kusema huyu ni sisimizi aende zake
na watu kama Mwanakijiji wakiona ni sawa...leo misingi hiyo hiyo inakiukwa tena
na sasa hivi ndio watu wanaamka kupinga...laiti mtu kama Mbowe angezoea kupingwa
toka mwanzo akileta kitu hakiko sawa..asingeleta haya ya sasa
 
Kuna mahali tutakuwa tunakosea sana. Kama kuna kuna hoja na iwekwe wazi ijadiliwe, lakini hili suala la eti 'wageni', na nini sijui, halitawajenga zaidi ya kuzidi kuwagaweni.
Naona ni mwanzo wa kufungua milango ya kubaguana, kuna watu watadai wanaostahili zaidi chamani ni wanachama waishio nchini kuliko waishio nje ya nchi. Itafika mahali kabla ya kugombea uongezi mtadai ili kukidhi vigezo lazima uonyesho ngeu au jeraha mwilini mwako ulilolipata katika harakati za 'kukipigania' chama au ulete ushahidi wa mtu wako wa karibu aliyeuawa katika harakati hizi. Kufikia hapo tayari mnakuwa mmeshasahau objective yenu ya kimsingi kwa sababu ya madaraka.
Misimamo mingine ni upofu tu kuendelea kuing'ang'ania, the true meaning of victory has hidden in the truth that, 'sometimes the better way to win is to loose'.
Nisiwachoshe bwana maana waingereza wana kamsemo kao kanasema "behavior is comfort zone". Hivyo basi maamuzi ni yenu, 'mfe mkiwa maadui au mshinde mkiwa mmeungana'.
Msitusumbue sisi na hiyo misimamo isiyoeleweka unless kuna ukweli mnatuficha.
 
Ni vizuri kufikiri mara mbili kabla ya kutenda! Mwisho wa siku ni muda ndio utakaoamua. Kusema ni sawasawa na dhahabu na kunyamaza ni sawasawa na fedha. Mwenye hekima wakati mwingine huamua kunyamaza na kuupa muda nafasi!!
 
Acha kupotosha, Zitto hakuzuiwa kugombea uenyekiti !.

Acha kuongea statement za jumla jumla ambazo umezibadilisha kwenye fikra zako kuwa facts baada ya kusoma propaganda mbali mbali na kuamini kwamba huo ndio ukweli !

Nafikiri unamaanisha ya Zitto kufukuzwa
mimi sikulitaja hilo
mimi nalitaja la Zitto kuzuiwa kugombea uenyekiti
msingi wa demokraia ilikuwa wamshinde kwa hoja na kushawishi wanachama wasimchague
lakini sio kumzuia hata kugombea tu,wakati chama ni cha kidemokrasia

Huo ni mmoja wa mifano ambapo chama kiliuka misingi yake yenyewe tu inayojitangaza kuisimamia
na suala la Kafulila pia....tena Slaa huyu huyu ndo alikuwa jeuri kwa Kafulila...

Mkikiuka misingi kwa kuwatazama watu na kusema huyu ni sisimizi aende zake
na watu kama Mwanakijiji wakiona ni sawa...leo misingi hiyo hiyo inakiukwa tena
na sasa hivi ndio watu wanaamka kupinga...laiti mtu kama Mbowe angezoea kupingwa
toka mwanzo akileta kitu hakiko sawa..asingeleta haya ya sasa
 
Hongera Mbowe ,kazi nzuri chadema sio chama cha mtu! Hongereni wana ukawa hapa sasa ndio wakati wa kuwajua wapenda mabadiliko ya kweli au wapenda mabadiliko maslahi! CCM mwanzoni walishawachezea faulo Kwa kutaka kuvunja umoja wenu wana ukawa kuelekea October 2015 ndio mana kulishaanza minyukano ndani ya ukawa lkn baada ya kuingia mgombea neutral ukawa imeimarika, ushauri ni kutomdharau doctor slaa kwa kauli za kejeli na pia Kwa doctor mwenyewe kukubaliana na hali halisi na kuachana na wapambe ambao Kwa wakati huu wanatumiwa na ccm. Hongera sana doctor Kwa kuwachunia clouds TV kwani wao ni tbccm2 wameona mambo hayaendi vizuri chadema wakajifanya wana upendo na wewe, siku zote walikuwa wapi?
 
Mimi ni kati ya watu waliopinga kwa nguvu nyingi ujio wa Lowassa CDM na mwanzoni nilichukia sana baada ya kudhihirika wazi kwamba amejiunga CDM na anakuwa mgombea Urais.

Baada ya kumsikiliza Mbowe, partly nilikuwa convinced lakini bado sikuwa tayari kuunga mkono Lowassa kupeperusha bendera. Lakini baada ya kutafakari kwa kama siku mbili hivi, nimeamua kuwa behind CDM na UKAWA kwenye hili !

Tuna vifurushi viwili tu na kitu ya hivyo inabidi tufanya uchaguzi wa kimojawapo : Kifurushi cha kwanza ni cha CCM kikiwa na magufuli ndani yake, na Kifurushi cha pili ni cha UKAWA kikiwa na Lowassa ndani yake !. Mimi ninachagua kifurushi cha UKAWA kwani alternative yake ni mbaya zaidi !

Stay Tuned: Tunatarajia kutengeneza njia mahali hapa ambapo panaonekana hakuna njia. Siyo sahihi kuwaachia nchi na hatima ya nchi watu ambao hawakutoa hata tone moja la jasho kupigania mabadiliko ya siasa. Iweje leo hii baada ya yote ambayo watu wamesimamia wengine kwa damu na wengine hata kwa uhai wao waje watu wavune wasichopanda kwa ahadi kuwa ati na sisi tutakula nao watakachovuna? Kesho Inshallah, tutaweka hoja zetu wazi ili wao waamue kama wanataka kuungwa mkono nasi au la; hatutaki wao watuwekee masharti ya sisi kuwaunga wao mkono au kutupigisha mikwara ya kwanini tukae kimya ili wao wafanye wanalotaka.
Hatukukaa kimya kwa watawala walioshindwa wa sasa, na hatuwezi kukaa kimya kwa wanaotaka kuwa wa kesho!

MM

NB: Nitajaribu kutoa majibu ya hoja zilizotolewa na baadhi ya watu (ikiwemo ile mada ya Character X) kuhusiana na kuunga mkono hili la Lowassa.
 
Stay Tuned: Tunatarajia kutengeneza njia mahali hapa ambapo panaonekana hakuna njia. Siyo sahihi kuwaachia nchi na hatima ya nchi watu ambao hawakutoa hata tone moja la jasho kupigania mabadiliko ya siasa. Iweje leo hii baada ya yote ambayo watu wamesimamia wengine kwa damu na wengine hata kwa uhai wao waje watu wavune wasichopanda kwa ahadi kuwa ati na sisi tutakula nao watakachovuna? Kesho Inshallah, tutaweka hoja zetu wazi ili wao waamue kama wanataka kuungwa mkono nasi au la; hatutaki wao watuwekee masharti ya sisi kuwaunga wao mkono au kutupigisha mikwara ya kwanini tukae kimya ili wao wafanye wanalotaka.
Hatukukaa kimya kwa watawala walioshindwa wa sasa, na hatuwezi kukaa kimya kwa wanaotaka kuwa wa kesho!

MM

NB: Nitajaribu kutoa majibu ya hoja zilizotolewa na baadhi ya watu (ikiwemo ile mada ya Character X) kuhusiana na kuunga mkono hili la Lowassa.

Hautapata wakuwagawanya nyie inaonekana mnapigania maslahi binafsi .sisi lengo letu ni ccm itoke madarakani .msitufanye watanzania wajinga .pelekeni njaa zenu huko.wewe unaona njaa zako .uone watanzania wangapi wanakufa kwa kukosa madawa shauri ya ccm.chadema wangapi wamekufa ukilinganisha na watanzania waliokufa kwa mtapia mlo na kukosa tiba.suseni sisi tunaendelea hakuna namna ccm out 2015 nilazima
 
MM
Ni vizuri kutoa ya moyoni. Ukimya wa Dr haulipi. Wengi tunasononeka.

Ombi langu kwako: Kwa namna yoyote mtakavyotoka, ni vema mlenge kuimarisha umoja ndani ya CDM na UKAWA kwa ujumla. Kinyume na hapo mtakuwa mmeipa kick ya uhakika CCM.

Nasubiri hoja zako.
 
Kweli naamini zile hela za CCM zimekufikia..mtu aliyenipa taarifa kuwa umenunuliwa na CCM kuvuruga nilijua utani sasa nimeamini..Ndugu zangu tegemeani maandiko mengi kutoka kwa huyu mtu kuanzia kesho...kama ungekuwa na nia ya dhati ungejua adui yetu ni CCM..ungetumia busara ya kubaki kimya kama ulivyobaki kimya wakati anasulubiwa Zzk..Arfi..Kafulila and the like..Wanachadema wanahitaji kuficha tofauti zao sasa ili kuitoa Ccm
 
Back
Top Bottom