Kuelewa Mikataba ya Nafsi: Makubaliano Tuliyofanya Kabla ya Kuja Duniani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,640
697,940
Umewahi kusikia juu ya mikataba ya kiroho? Inachukua sehemu kubwa katika kuamua jinsi tunavyojiumba kama watu tukiwa hapa Duniani.

Kabla ya kila kuzaliwa kwetu duniani, tumepewa chaguo. Ni chaguo la kuchagua kusudi la maisha yetu ya kiroho; tunaulizwa ni somo gani tungependa kujifunza wakati huu na jibu tunalotoa huamua maisha yetu hapa duniani.

Na mikataba ya nafsi hufanywa kulingana na somo tulilochagua. Tukiamua kujifunza subira, hatutazungukwa na watawa na wenye Hekima, bali na ndugu au jamaa ambao watatuudhi na kutukera hadi kufa.

Ikiwa tunataka kujifunza upendo, tutaona chuki kwenye kila pito letu, na ikiwa tunataka kupata hali ya kujiamini, basi mafarakano yatakuja na kutukanyaga kila mahali. Haijalishi ni somo gani tunataka kujifunza, tutapewa kinyume chake…daima!

Katika uwanna mkubwa wa miunganisho ya wanadamu, mahusiano fulani yanajitokeza, yakitoa ishara ambazo ni vigumu kuvunja.

Zinavuta hisia zetu kwa njia ambazo hatuwezi kueleza, zikiibua hisia ngeni sana, zenye mvuto ama msukumo wa aina yake, na kututikisa hisia zetu za ndani.

Hebu fikiria unakutana na mtu kwa mara ya kwanza na kuhisi mvuto wa ajabu. Au, kwa upande mwingine, chuki ya papo hapo na isiyoelezeka. Je hizi ishara zina uhusiano wowote na mikataba yetu ya kiroho kabla ya kuzaliwa?

Ni kama wimbo ambao mashairi yake huwezi kuyakumbuka kabisa, lakini wimbo huo ala na midundo yake vinakusisimua kwa namba ya pekee sana ndani yako. Haya hayatokei kwa bahati mbaya ni mwangwi wa maisha ya zamani yanayojirudia katika maisha yako ya sasa.

Karibu kwenye ulimwengu unaovutia na mara nyingi wenye misukosuko wa miunganisho ya kiroho. Katika safari hii ya kuelimishana, tutafunua kiini cha vifungo vya maisha ya kiroho, kuchunguza kile kinachosema nasi ndani mwetu, ishara na matokeo yake na kutambua ishara za mahusiano ya kiroho. Je, uko tayari kutafakari
 
Huu ni uelewa wa jamii za kipagani, watu wasiotafuta elimu ya vitu na wasiofanya tafiti.
FB_IMG_1698766368649.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chanzo cha habari hizi kujulikana ni kipi?

Naamini binadamu wote tumejukuta tumezaliwa, tuta zaa na sisi tutakufa, na tulio wazaa watazaa nao watakufa na kuendelea

Huvijui vizazi vyako 100 nyuma kama ambavyo vizazi vyako 100 mbele havitakujua kama uliwahi kuishi duniani

Je ufahamu huu ulifikaje kwa mwanadamu kujua kabla hajazaliwa aliingia mkataba ya kiroho ?
 
What you narrate as a self today ni experience uliyopitia jana....Ubongo wa sapien ni dynamic unabadilika kutokana na experience...prove me wrong
 
Duh dunia inaenda kasi sans yaani huyu yeye kaamua kuishi kwa kudhani dhani ue hatak mambo mengi
 
Ngonjera zisizo na ithibati yeyote! Sasa nina swali hapo, hiyo mikataba tuliingia ya kazi gani ikiwa hata kukumbuka jinsi ilivyokuwa ni ngumu! Ni sawasawa umsainishe mgonjwa wa akili mkataba kisha baadae akijapata akili umkumbushe kuwa ulisaini 😂😂
 
Chanzo cha habari hizi kujulikana ni kipi?

Naamini binadamu wote tumejukuta tumezaliwa, tuta zaa na sisi tutakufa, na tulio wazaa watazaa nao watakufa na kuendelea

Huvijui vizazi vyako 100 nyuma kama ambavyo vizazi vyako 100 mbele havitakujua kama uliwahi kuishi duniani

Je ufahamu huu ulifikaje kwa mwanadamu kujua kabla hajazaliwa aliingia mkataba ya kiroho ?
Yani mwandishi nipo halafu unauliza chanzo cha habari? Tena unasema kabisa hakijulikani?
Je unajua nini juu ya DNA!?
Je unajua nini juu ya umbilical cord !?
Je unajua nini juu ya vizazi?
Vipi kuhusu realm of eternity?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom