A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

kwa mwenye ushahidi wa uhakika aupeleke polisi au aongee na vyombo vya habari. tuache unafiki.

MOD: FUNGA HII THREAD!!!!!!!!!!!!!! HATUWEZI KUJADILI SWALA BASING ON RUMOURS / TETESI

Apeleke ushahidi wapi?? POLISISIEM!? unanengua wewe, tulishashtuka longtime kitambo,imebaki na sisi raia tuunde chombo chetu cha usalama kwani vingine vyote vimebaki ni usalama wa nyinyiem na baba mwanaasha. shame on you VAMPIRES!!!!,your days are numbered!
 
julius mtatiro
michezo ya usalama wa
taifa italiingiza taifa hili
kwenye machafuko. Nasema
waziwazi kuwa
waliomchukua dr. Ulimboka
nyumbani kwake ni usalama wa taifa na igp anawajua,
na rais anajua mchezo wote.
Hii mijizi na miuaji isidhani
hatuna akili timamu.
Ikumbukwe kuwa vyombo
vyote vya ulinzi na usalama viko chini ya rais
aliyechaguliwa kwa tiketi
ya ccm. Katika hili ccm
hawakwepi lawama. Na
kama ilivyokuwa kwa
wakoloni "creating their own destruction" na ccm
inapitia njia hiyohiyo.
Inajichimbia kaburi
waziwazi.. Onyo tunalotaka
watawala walijue ni kuwa
wanaharakati
hatutakubali ccm ife kwa
njia ya kudhuru, kutisha na
hata kuua watu. Mtindo huu utatufanya tuchukue
maamuzi magumu mno,
vyombo vya dola visione
tumekaa kimya, amani hii
ndani ya tanzania
hailindwi na usalama wa taifa uchwara wasiojua
nani kala hela za epa ila
wanajua nani anaongoza
madai ya haki ya
wafanyakazi wa sekta
fulani. Dr ulimboka na wadau wote
tusikate tamaa, mapambano
ya kuitengeza tanzania ya
wananchi na siyo ya
viongozi na wahuni
wachache ndio unashika kasi. Tunafuatilia uvunjaji huu
wa haki kwa ukaribu sana. Julius mtatiro,
0717 536 759.

Updates
julius mtatiro akijibu topic kwenye fb anasema...
Joseph, hujui jambo lolote
kuhusu mambo hata
na;michezo hii, nasisitiza hujui
a, b wala c, mie nazijua,
nimeishi maisha hayo na
mimepambana na usalama wa taifa mars nyingi, i know it and
they know that i
know.....nimewahi hata
kupewa kadi ya ccm kwa
nguvu.....hawa ni wanyama,
nitakupa uzoefu hapa. Kama hujawahi kutiwa misukosuko
na hawa wanyama huwezi
kujua nachoongea. Hata cuf
ikiongoza dola kesho ,
madaktari hawapaswi
kunyimwa haki za msingi. Mie nachojua, anayeua kuna mama
na watoto na wagonjwa ni
fisadi na mwizi fulani ambaye
anadiriki kuficha bilioni 500 nje
ya nchi, fedha alizowabia
masikini, fedha ambazo zingewalipa madaktari
mishahara mizuri....wewe
unadhani madaktari ndo
wanaua wagonjwa?..

ulikuwa wapi wewe siku zote ..unajitokeza leo kwa mgongo wa dr.ulimboka ..chama chako cuf kimekushinda kinakufa..acha kutuharibia amani yetu watanzania wewe..nenda kajenge chama chako huko usijenge kwa kushawishi watu wavunje amani..uandamane mwenyewe. Alafu una ushahidi gani kama ni usalama wa taifa wamefanya hivyo.. Nafikiri elimu yako haikusadia mtatiro.
 
Watawala waliua manabii ili kuzuia ujumbe wa manabii lakini, walikuja manabii wengine na ujumbe ukawafikia watu.Ya Ulimboka yanapita tu lakini tutafika.Nchi imeuzwa.
 
Mnakumbuka yale mauaji ya Gen Kombe 1996? Ilikuwa aibu tupu! Mkewe Rose aliyekuwa eye witness wakati Kombe anamiminiwa risasi kwenye shamba la mahindi hakuitwa kama shahidi pale awali kwenye kesi ya wale askari waliomuuwa wakifikiri eti ni jizi la magari liitwalo Mr White.

Baadaye sana, baada ya Waziri wa ndani, Ali Ameir Mohamed kumtembelea Rose na kumuahidi mapesa ndiyo akaitwa kama shahidi lakini alifundishwa ya kusema.
 
Mtatiro anawajua vizuri watu wa TISS sijui kapata wapi ujasiri huo tena?

anawafaham mana wakat mi nipo chuo first year ye alikua fourth year udsm, alikua mwanaharakat wa ukweli, so i blv he z sayin the truth.
 
-Miaka saba imepita,
tangu ulipoibuka,
jemedari kujikita,
harakati kuongoza.
-Hatamu ukazishika,
kuongoza tafakari,
imetosha kupigika,
kwa maslahi kiduchu.
-Daktari sio punda,
wa kubebeshwa mizigo,
na mgongo kumpinda,
daima akitumika.
-Wito isiwe ni fimbo,
ya kutodai mafao,
msitupiwe makombo,
wengine wakila kuku!
-Pamoja mkashikana,
kudai haki zaidi,
na sime mkatiana,
mkasimama imara.
-Sumaye akawajia,
kwa makeke na mikwara,
mwishowe akachukia,
kuambiwa iwe noma.
-Uli hukutetereka,
na mwenzio Kigwangwala,
wala hamkutishika,
kucheleweshwa hitimu.
-Hukuwa mbinafsi,
japo walikuandama,
ukazikosa nafasi,
ajira serikalini.
-Wengi walifaidika, kwa majitoleo yako,
ijara kuongezeka,
japo hukuifaidi
-AMO, CO na nesi, wote walichekelea,
nao wakajinafasi,
kupitia jasho lako.
-Maisha yakasogea,
na siku zaendelea, wapo walokusahau,
na wala siwalaumu.
-Mwaka huu ukaanza,
na mambo yake ni mapya,
Njelekela kajiponza,
Interns kuwachokoza.
-Kaka zao wakaguna,
mbona mnawaonea,
wakaamua kwa kina, na utangazwe mgomo.
-Ulimboka hukulemba,
unahodha ukashika,
vuguvugu likatamba,
nchi ikatikisika.
-Pinda katoa vitisho,
watu wakamtazama,
likamtoka na jasho,
hadi kwenye meno yake.
-Mwisho kadai suluhu,
ahadi akazimwaga,
na mrejee kazini,
yote yatatekelezwa
-Kumbe ni danganya toto,
hakuna lililojiri,
mazingira na kipato,
vyote vikatelekezwa!
-Madokta wakagoma,
Rais akawasihi,
na wao wakamsoma,
wakarejea kazini.
-Siku tisini zapita,
madai yajadiliwa,
mwisho tamko lapita,
hakuna pesa hazina.
-Madokta wajadili,
hili haliwezekani,
huu ni udhalili,
fani yetu kutendewa.
-Wakaitisha mgomo,
juni ishirina tatu,
usokuwa na kikomo,
huu ni aina yake!
-Kortini wakaenda,
serikari wasikivu,
kuuzuia mgomo,
wajifiche udhaifu.
-MAT wakaishitaki,
na kujitoa akili,
ya kwamba ni jumuia,
iloitisha mgomo.
-Walipokuja ng'amua,
ya kuwa wamepotoka,
Ulimboka wamsaka, na kumtia nguvuni.
-Walimpiga vigongo,
na taya wakamvunja,
wakamponda ubongo,
ili akome fikiri.
-Na mbavu wakamvunja,
msituni wambwaga,
maskini kajikunja,
wakadhani amekufa
-Ujumbe kwao majuha ,
waliyoyatenda haya,
damu ya Dokta Uli,
haitamwagika bure.
-Amani tunda la haki, hailetwi kwa mtutu,
kwa vile wastahiki,
madokta watashinda.
-Na daima mkumbuke,
mabavu yana mipaka,
mamlaka yenu yote,
yatoka kwa wananchi.
-Daktari Ulimboka, ninakuombea heri,
Mungu akupe fanaka,
na afya njema daima.

MWENYE HAKI DAIMA ATASTAWI KAMA MTENDE, NAAM, KAMA MWEREZI WA LEBANONI!
 
Mhxx, watakufa wamesimama hawa wauaji. Ukiua kwa upanga,utakufa kwa upanga.Mwisho wao ni mbaya sana,
 
Busara itumike zaidi. tutawale hisia zaidi. Mungu alitupa macho mawili, masikio mawili na mdomo mmoja, ili tuone mengi, tusikie mengi na tuseme machache.
"Mungu ibariki Tanganyika, Mungu ibariki Zanzibari, rip Tanzania"

Alitupa na mikono miwili na vidole kumi,ili tushike keyboard tuandike saaaana!
 
Big up Sunday Charles aka Julius Mtatiro kwa points zako wachane hao wachane!
 
polisi imemkamata gaidi wa al shabaab haitashindwa hawa wahuni wachoma makanisa na kuteka watu. Mia
 
Mi naiona hii hali inaashiria kutoweka kwa amani tanzania, sijui hawakufikiria athari ya kufanya unyama huu kama ilivyowatumia viongozi wa dini Igunga na inavyoendelea kupandikiza chuki za kikanda na udini,miongoni mwa watanzania. Athali zake ni mbaya zaidi ya kuhalalisha utawala uliochokwa na Watanzania

natamani kina Dk.Slaa watangaze tahir square yetu mara moja shughuli ya kumuondoa Kikwete ianze.
 
Umetisha sana mkuu, Mungu atamsaidia na atapona kwa uwezo wake Inshaallah.
 
Ndugu nadhani cc wapambanaji wote hakika ni jukumu letu kupiga magoti na kumwombea Dr. Ulimboka Mungu amponye maumivu, majeraha na daima serikali inahusika na hl. Pia niombe madaktari wote waungane na wagome kabisa hadi 1: madai yao yatakapotekelezwa, 2: walio mfanyia unyama Dr. Ulimboka wamekamatwa na kunyongwa.

i like that
 
Mbona hili wala sio siri tena ... Jamaa alimpigia simu wakamalize maongezi LEADERS CLUB!!! Ulimboka akaondoka na Rafiki yake mmoja! Wakati wanongea na huyo Jamaa hakueelwana ... Jamaa akapiga simu kwa hao wanjeshi walikuja kumburuza na kumchukua ... wakamuacha Rafiki wa ulimboka na huyo jamaa mwingine kwa kusema hatuwahitaji nyie tunamuhitaji Dr ulimboka ....!!Rafiki wa Ulimboka ... Akapiga simu kwa waaharakati wa Haki za Binadamu ..Hellen Kijo Bisimba at al .. na usiku huo wakaanza kumtafuta na kuripoti vituoa mbalimbali vya Polisi ...lakini Kila kituo wakidai ... hamjui huyo mtu .... labda waje asubuni .... na subuhi? Wapata habari toka kituo cha polisi tegata .... kaokotwa mtu ....blabalahhhh!!Source. Hellen Kijo Bisimba!!

MWISHO WA UBAYA NI AIBU,Serikali ya ccm aibu kwenu kwa kuwaua wanaodai haki zao za kimsingi.
 
Back
Top Bottom