A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

Asingekubali kwenda leaders kuzungumzia mgomo. Halafu hawakuelewana maneno gani?
Kuna kitu hapo!
 
Hakika Roho yangu inaniuma sana kwa kitendo alichotendewa Dr Ulimboka. Mungu akuponye . Ila nimesikia ITV wakisema amepata Brain concursion kama ile ya Marehemu Kanumba. Ehe Mungu mjalie mja wako apone. Hivi kumpiga huyu Dokta ndio Madaktari wataacha kudai haki yao? Naona tunatafuta mgogoro usio na tija kwa wananchi wanyonge.
 
Ukweli utapatikana, kwa sasa majibu hayatakuwa na uhakika. Can be YES or NO.
 
Tuungane Watanzania wote kuupinga udhalimu huu ikiwezekana tufanye maandamno ya kuilaani serikali kwa unyama huu.
"Ndugu zangu,

Najaribu kutuliza mawazo ili angalau niweze kuwapa kidogo tulipofikia na tunakoelekea juu ya suala hili. Kwa kweli haivumiliki ukimwona ulimboka kwa jinsi alivyotendewa na hali aliyonayo; kwa wale wanaojua hali za kitabibu, "this is a very unstable condition that demands permanent watch 24/7".

Kwa taarifa tulizokusanya, ulimboka na mwenzake waliitwa na Afisa mmoja (Jina linahifadhiwa) ili kuzungumza mambo (fulani) na wakiwa wanaendelea na mazungumzo bila kuwa na mwelekeo wa muafaka, jamaa akawasiliana na watu (fulani) kwa simu. Ghafla wakajitokeza "ASKARI" wakawataka yule (Afisa) na Dr (aliyeongozana na Ulimboka) waendelee na shughuli zao na kuwambia "Tunamtaka huyu". Wakatumia nguvu, wakamburuta na kumtia kwenye gari jeusi na kuondoka naye wakidai wanampeleka Polisi.

Huku wakiwa wanamtesa, walimlazimisha mambo kadhaa (kwa sasa tusiyataje) wakaenda naye asikokujua, wakampiga sana kwa ngumi, mateke na magongo na wakati mwengine wakitumia Bunduki zao. Wakiwa wanampiga pia walikuwa wakisema kuwa amewatesa/wasumbua sana na kuwa anajifanya mjanja mbele ya (Srk) na hivyo wanamalizana naye; akapoteza fahamu...

Wakamtupa eneo la mapori huko Tegeta hadi alipookotwa na wananchi asubuhi na kukabidhiwa mikononi mwa Wanaharakati waliompeleka Hospitali Muhimbili.

Wakati akipokelewa MOI tayari baadhi ya wanaharakati walishafika eneo lile, kumbe kati ya walimpokea alikuwamo kijana anayesadikiwa kuwa ni "Askari". Huyu aligundulika baada ya mda mfupi akiwa amejificha chooni akiwasiliana kwa simu na watu aliokuwa akiwaambia " Hajafa. Bado anahema.... na maneno mengine yaliyoashiria kuwa waliofanya 'kazi' ile hawakukamilisha 'maagizo'. Vijana wakamfundisha adabu kwa hasira na kumkuta akiwa na Redio Call, ambayo baada ya muda mfupi Polisi FFU walifika na gari na vifaa vya vurugu wakiisaka ile Radio.


Nashindwa kuendelea....."
NB: Haya ni maelezo ya mwanaharakati Albanie Marcossy aliyehusika kumsaka kama nilivyoyanukuu Mabadiliko Group.
 
Katika taarifa ya habari mtu aliyekuwa akimtafuta mfululizo kwa siku tatu ni mtu wa Ikulu aitwaye kwa jina moja David na baadaye aliondoka kumfuata huyu David na baadaye akatekwa infront of him. Kwa mwenye akili anajua tu hii ni plan from some where


wacha kuleta chokochoko hao vitarishi vya waarabu wasio na uchungu wa nchi yao unafikiri wanastahili kupata nini ???

Wanataka kurudisha masulatani huku wakitumiwa na uamsho kuleta vurugu , kamwe hatutowawacha waarabu hao
 
This should be th eturning point of removing CCM and its weak governement. Kila mtu ana haki ya kudai haki yake, why killing innocent people? I cant believe this.
 
Yale yale ya Kariuki wa Kenya.

Kweli Jasusi hawa jamaa wanaiga mambo ya nyang'au wa Kenya walipomuua J.M. Kariuki na kumtupa kwenye msitu wa Ngong!!Hii hatari sana kwa Tanzania inaelekea amani ndio inatoweka sasa!They are turning the country into killing fields.!!
 
Nchi inatia kinyaa...bora syria...inajulikana kuna machafuko kuliko tanzania
 
Julius Mtatiro
MICHEZO YA USALAMA WA
TAIFA ITALIINGIZA TAIFA HILI
KWENYE MACHAFUKO. NASEMA
WAZIWAZI KUWA
WALIOMCHUKUA DR. ULIMBOKA
NYUMBANI KWAKE NI USALAMA WA TAIFA NA IGP ANAWAJUA,
NA RAIS ANAJUA MCHEZO WOTE.
HII MIJIZI NA MIUAJI ISIDHANI
HATUNA AKILI TIMAMU.
IKUMBUKWE KUWA VYOMBO
VYOTE VYA ULINZI NA USALAMA VIKO CHINI YA RAIS
ALIYECHAGULIWA KWA TIKETI
YA CCM. KATIKA HILI CCM
HAWAKWEPI LAWAMA. NA
KAMA ILIVYOKUWA KWA
WAKOLONI "CREATING THEIR OWN DESTRUCTION" NA CCM
INAPITIA NJIA HIYOHIYO.
INAJICHIMBIA KABURI
WAZIWAZI.. ONYO TUNALOTAKA
WATAWALA WALIJUE NI KUWA
WANAHARAKATI
HATUTAKUBALI CCM IFE KWA
NJIA YA KUDHURU, KUTISHA NA
HATA KUUA WATU. MTINDO HUU UTATUFANYA TUCHUKUE
MAAMUZI MAGUMU MNO,
VYOMBO VYA DOLA VISIONE
TUMEKAA KIMYA, AMANI HII
NDANI YA TANZANIA
HAILINDWI NA USALAMA WA TAIFA UCHWARA WASIOJUA
NANI KALA HELA ZA EPA ILA
WANAJUA NANI ANAONGOZA
MADAI YA HAKI YA
WAFANYAKAZI WA SEKTA
FULANI. DR ULIMBOKA NA WADAU WOTE
TUSIKATE TAMAA, MAPAMBANO
YA KUITENGEZA TANZANIA YA
WANANCHI NA SIYO YA
VIONGOZI NA WAHUNI
WACHACHE NDIO UNASHIKA KASI. TUNAFUATILIA UVUNJAJI HUU
WA HAKI KWA UKARIBU SANA. JULIUS MTATIRO,
0717 536 759.

Updates
Julius mtatiro akijibu topic kwenye fb anasema...
Joseph, hujui jambo lolote
kuhusu mambo hata
na;michezo hii, nasisitiza hujui
A, B wala C, mie nazijua,
nimeishi maisha hayo na
mimepambana na usalama wa taifa mars nyingi, I know it and
they know that I
know.....nimewahi hata
kupewa kadi ya CCM kwa
nguvu.....hawa ni wanyama,
nitakupa uzoefu hapa. Kama hujawahi kutiwa misukosuko
na hawa wanyama huwezi
kujua nachoongea. Hata CUF
ikiongoza dola kesho ,
madaktari hawapaswi
kunyimwa haki za msingi. Mie nachojua, anayeua kuna mama
na watoto na wagonjwa ni
fisadi na mwizi fulani ambaye
anadiriki kuficha bilioni 500 nje
ya nchi, fedha alizowabia
masikini, fedha ambazo zingewalipa madaktari
mishahara mizuri....wewe
unadhani madaktari ndo
wanaua wagonjwa?..

2.....usalama
wanajua....jukumu la kumlinda
ULIMBOKA lilikuwa mikononi
mea vyombo vya dola, chochote
kilichomkuta wanakijua wao.
Michezo hii ya kitoto una mwisho wake.....jambo lingine
ni kuwa Mimi ni kiongozi wa
kawaida wa wanadamu,
kiongozi mkubwa ni mungu
peke yake. Na hawa
wanaojidai kutishia maisha ya ya wenzao ni waoga,
hawajiamini na wana hofu.
Wanajua siku moja
watakufa....tusitishiwe wala
kutishika, kila mtu atakufa.
Nasisitiza kuwa waliomteka ULIMBOKA ni usalama wa taifa
na serikali ya kikwete inajua
kila kitu. Kama kuna mtu
anaona nakosea sana kusema
hata akawaambie usalama
wake kunifuata pia mie.

3.Joseph, wakati naongoza vyuo
vikuu vyote kupitia TAHLISO
kama katibu mkuu nimekutana
na mikasa hiyo mara kadhaa,
serikali hii isiyojiweza inakosa
NEGOTIATION POWERS na inakimbilia njia nyepesi za
kuwanyamazisha wanaotetea
haki ambazo zinatishia uwepo
wa mashangingi ya wakubwa.
Sema kwa bahati mbaya
ULIMBOKA aliji-underestimate sana, aliona ataishi kwa
usalama tu huku akipigania
haki za watanzania masikini.
Kumbe hakuwa na uzoefu
michezo hii. Wakati fulani
nikiongoza move ya kutetea wanafunzi masikini wapate
mikopo kuna vyuo vilikuwa
vikifungwa kwa migomo kila
kona, serikali nyepesi ya CCM
ikaacha kushughulikia utatuzi
wa mambo ya wanafunzi wakajibidiisha kuuaminisha
umma kuwa tatizo la vyuo
vikuu siyo mikopo ila ni mtu
mmoja au wawili
wakiongozwa na mtatiro.
Wakaanza kunisaka kila kona, kila nilipoona usalama wangu u
hatarini nilijisalimisha kwao
nikiwa na ndugu au rafiki
zangu, walishindwa wanifanye
mini. Ukiwa unaongoza
harakati kama hizi za ULIMBOKA utapata marafiki
wengi usalama w taifa,utapata
wasichana wengi wazuri kama
malaika ili mradi uwekwe
kwenye target. Utapigiwa simu
nyingi na watu uwajuao na usiwajua ilimradi wakuombe
muonane mahali fulani,
utabembelezwa na viongozi
wengi wakuhonge milioni
kadhaa usaliti mapambano ya
kudai haki, utaahidiwa kusomeshwa nje, kupewa
kiwanja au nyumba karibu na
bahari na hata kuahidiwa vyeo,
lengo ni uache kuongoza
mapambano. Sitarajii tena
kusikia kiongozi yeyote wa mapambano ya kudai haki
anaitwa mahali na watu
asiowajua halafu anakwenda
kirahisi tu. Sitarajii mtu
anayeongoza mapambano ya
kudai halo aingie na kula chakula kila mahali bila
utaratibu. Sitarajii viongozi w
mapambano wauawe kwenye
wasichana warembo kama
malaika wanaotegeshwa ili
kuzima nuru ya mabadiliko. Ukijua unapambana na serikali
dhalimu isiyo na "POWER OF
NEGOTIATION" kwa sababu
serikali yenyewe ni nyepesi
lazima utambue maisha yako
yamo hatarini. Ni lazima hawa wanaotaka kuwaua viongozi
wa harakati wapate tabu,
wafunge safari waje
majumbani, watuulie
majumbani, au watuteke kwa
nguvu mbele ya ndugu na kwa nguvu, isiwe kirahisi namna hii.
Na jambo la mwisho la
kukumbuka ni kuwa
WATAWALA
WANAJIDANGANYA mno, siyo
rahisi kuikoa serikali nyepesi. Haiwezekani hospitali
inayotibu wagonjwa elfu
hamsini haina AMBULANCE
inayogharimu tzs 20 milioni,
wakati waziri mmoja ana
shangingi la milioni 200. Hata ndiyo wanayopigania
madaktari na tutawaunga
mkono hadi mwisho.
 
hizi chochoko za mabwana zako wa kiarabu na kisultani ziwacheni ,hii ni serikali ya kiafrika ya watu weusi na kamwe hatuwezi kuchezewa na vitimbakwiri vya kiarabu na kisultani.

Tutawashughulikia vizuri hao wenye chapa ya uamsho

Alishindwa Kaburu Botha na De clerk itakuwa nyie?
 
Yale ya OUKO wa Kenya hadi akateketezwa kwa Tindikali. SIAMINI kama nchi hii kuna unyama kama huu. Wahenga walisema ukitaka UBAYA DAI CHAKO: hivyo ndivyo tunavyotattua migogoro kazini? Sasa hizi sheria za KAZI ameandikiwa nani ikiwa tutakimbilia kuangamizana kwa njia kama hii. Pole Dr Ulimboka. Get well Soon.
 
nadhani wewe tu ndo hujamwelewa mkuu, hebu soma tena hiyo. Anazungumzia ishu ya dr. Ulimboka.

sote tumeguswa na hili tukio ila heading haijakaa sawa ukilinganisha na content mkuu!
 
Daah yaani ikulu ihusike na upuuzi huu huyu dr ni kainzi tu na hii cyo move ya serikali jamani mko dunia gani nyie cku hz kuna teknolojia km serekale ingetaka kumuondoa kiulaiiiniii angeondoka na ingekuwa poa tu mnaleta za abunuasi hapa

Wewe unauita upuuzi kwa sababu unataka tuamini kuwa hivyo, lakini unajua fika kuwa si upuuzi. Unamwita Dr. Ulimboka kuwa ni ka nzi, je unajua kuwa mtikisiko tu wa mbawa za kipepeo unaleta matetemeko...tena makubwa? Tafakari!!
 
Back
Top Bottom