Upo sahihi kabisa. Kwanza angalia source ya utafiti wenyewe ni nani, utafiti umefanyika kwa njia gani, nchi ngapi zimehusishwa na questionnaire imekuwa framed vipi?
List ipo kwa ajili ya kuzisafisha nchi za wazungu na washirika wao kuonekana zina nafuu kwenye ubaguzi. Mfano, unapowauliza wapalestina kama wapo fresh kuishi na race nyingine unategemea jibu gani wakati white zionists ndio wageni kwao na wanawalipua kila siku lakini pia Palestine haitambuliki kama nchi kwanini kwenye huu utafiti tena wa wamarekani ghafla wameitambua wakati huohuo Israel yenye eneo kubwa na watu wengi haijaguswa,south Africa hakuna Apartheid leo na weusi wanaongoza sasa wameingiaje kwenye hiyo list,Egypt, Kuwait, Phillipines na Bahrain huo ubaguzi wanamfanyia nani alafu hata tukisema ubaguzi upo je ni kwa kiwango cha kufikia watu kufanya jinai na kuwakosesha minorities fursa za kiuchumi kama baadhi ya nchi za magharibi na mashariki ya kati.
Kinachoshangaza zaidi kwenye hio list hakuna Saudi Arabia, UAE wala Qatar(wote washirika wa Marekani) wakati ndio nchi ambazo visa vingi vya ubaguzi vinaripotiwa.
South America kuna Chile ambayo indigenous people(Mapuche) wamenyang'anywa ardhi na settlers wa kizungu, wakidai ardhi yao wanapigwa risasi. Kuna Brazil pia ambayo wakazi wa kwenye favela wengi ni weusi wa wahindi wekundu ambao bado wanatengwa kwenye nafasi za kazi na biashara matokeo yake wanakuwa wauza madawa tu.