Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,069
- 34,839
666-NYAYO ZA KUZIMU-4-
"mama Marinda tukimbie!.."
alinong'oneza mama Utopi,
"mie siwezi tena,miguu inaniuma!"
"jitahidi jamani,huoni wanazidi kuja!..
Na wanasikia harufu yetu!!"
alizidi kusisitiza mama Utopi huku wakiwa bado wamejificha na wale wazee wapo hatua kumi tu toka walipo...
"tupige tu ukunga watu waje watusaidie"
"usiku wote mzito huu nani atajitoa nje ya nyumba yake?...
Twende mama Marinda...twendeee!!"
alimshka mkono na kuanza kukimbia,alikua mbele ya mwenzake na aliutumia mkono wa kushoto kumkokotea...
Wale wazee hawakuonekana wakikimbia,walisimama tuli huku macho yao yakiwa yanawatizama wakina mama Marinda wanaokimbia,hawakufika umbali mrefu,mkono wa mama Marinda ulimponyoka mama Utopi,kama gunia la ulezi alidondoka chini!!.
"mama Marinda...amka twendee!..amkaa!!...
"siwezi!...siwezi!!..miguu yangu imefungwa na majani mama Utopi!..siwezi kuitoa!!...
Mama Utopi nisaidieee navutwaa!"
mama Utopi alijitahidi kumpa mkono mama Marinda lakini hakufanikiwa,Mama Marinda alivutwa haraka kwa kasi ya ajabu,sauti yake ya kuomba msaada ilizidi kupotelea msituni,na mwishowe haikuskika kabisa.Mama Utopi hakua na cha kufanya,aligeuka
na kuanza kukimbia kwa kasi zaidi....machozi yakimtoka na moyo ukidunda kwa nguvu kutokana na uoga na hofu nzito iliyomshika,aliona umbali wa kufika nyumbani umeongezeka,na kila akijitahidi kuongeza kasi ilikua kama ni kazi bure,mapafu yalimbana...na alihisi kama hapati pumzi,ilimbidi asimame kidogo apate kuhema,hakua na amani kabisa,alikua anatizama kila
pande kuthibitisha usalama wake,machozi yalizidi kumtoka alipofikiria mwenzake aliekua nae muda si mrefu hayupo tena,ilikua ni kama mchezo wa kuigiza alipomshuhudia mwenzie akivutwa na majani na kupotelea kabisa,alitupia macho upande wa kulia,aliona mwanga wa taa umbali wa kama hatua ishirini na tano toka alipo,akili yake ilimuambia kwamba pale ni kwa mama kadogo,haraka bila kupoteza muda aliamza kukimbia akielekea upande huo.
Alifungua kwa pupa geti la makuti la ile nyumba,aliingia ndani na kuanza kupepesa pepesa macho aone wapi atapata msaada,ghafla alisikia sauti kali iliyompasua wake moyo..
"wow! Wow!..wow!"
alistuka mno kuona mbwa watatu wakimfuata,alianza kurudi nyuma kwa tahadhari huku akiwaangalia mbwa wanaomsogelea,kwa nguvu aliropoka kuomba msaada..
"mama Kadogoo!!..mama Kadogoo!"
sauti hiyo ilimstua mama Kadogo aliekua ndani amelala na mumewe,na zaidi aliogopeshwa na sauti kali za mbwa zilizofika vizuri masikioni mwake,alimuamsha haraka mumewe,ilikua kidogo kazi nzito kwani alikua ametekwa vilivyo na usingizh mzito,ila kwa bugudha za kutosha alizozifanya zilifanikisha kuondoa mang'amung'amu ya mumewe,
"nini mama Kadogo?"
"nimesikia sauti nje ya mwanamke inaniita..na huskii mbwa wanavyobweka kwa nguvu??"
aliuliza mama Kadogo,
bila kuchelewa baba Kadogo alichukua panga lake chini ya kitanda kisha akatoka nje kwa kasi,alipofika nje alishuhudia mbwa wake wakiwa wanamparua parua mmama ambaye alikua bado hajamfahamu ni nani,aliwaamrisha mbwa wake waache lile tendo na haraka walitii amri,alimsogelea yule mtu na kugundua ya kwamba ni mama Utopi,aliloa damu kutokana na majeraha makubwa aliyosabishiwa na wale wanyama,alikua anagugumia kwa maumivu na huku akitetemeka.
* * * * *
USIKOSE SEHEMU 5 INAYOFUATA.!