P01 MABADILIKO YA MFUMO WA UCHAGUZI WA WABUNGE NA MADIWANI
A. MADIWANI
1. Diwani atakuwa na Elimu kuanzia walao shahada ya kwanza.
2. Diwani atachaguliwa na wananchi kwa kupigiwa kura
3. Mgombea atakayepata kura nyingi kuliko wote atahesabika kuwa ameshinda
4. Kama hakuna mgombea alieshinda, uchaguzi utarudiwa kwa wagombea wanaolingana kwa kuwa na kura nyingi zaidi.
5. Itaruhusiwa kuwa mgombea binafsi asiyetokana na chama cha siasa.
B.WABUNGE
1. Mbunge atakuwa na elimu walao kuanzia shahada ya kwanza
2. Mbunge atachaguliwa kutoka katika baraza la madiwani
3. Madiwani kwa kila baraza katika halmashauri wataruhusiwa kugombea na kumchagua mmoja wao kuwa Mbunge
4. Kila baraza la madiwani litachagua Mbunge mmoja
5.Baraza la madiwani litakuwa na uwezo wa kupiga kura ya kumvua ubunge kama wataona hamudu kazi
6. Mbunge alievuliwa ubunge ataendelea kuwa diwani
7. Baraza la madiwani litachagua diwani mwingine kujaza nafasi iliyoachwa wazi kwa kuvuliwa ubunge au kifo
8. Ukomo wa mtu kuwa Mbunge ni vipindi viwili
9. Hakutakuwa na wabunge wa viti maalumu
10. Hakutakuwa na wabunge wa kuteuliwa
11. Mbunge atawajibika kwa baraza la madiwani ambao nao wanawajibika kwa wananchi
12. Idadi ya Wabunge itakuwa sawa na idadi ya halmashauri zilizopo (185 Tanzania bara kwa sasa)
13. Kazi mojawapo ya Bunge ni kutunga sheria. Mabadiliko yoyote ya KATIBA, iwe yame-pendekezwa na
Bunge au serikali ni lazima yaidhinishwe na zaidi ya nusu ya Madiwani kwa kupiga kura katika mabaraza yao, kwakuwa Madiwani ndio wawakilishi wa karibu zaidi na wananchi na wanaweza kupata maoni ya walio wengi kwa urahisi na uharaka zaidi (hii ni baada ya kuunda upya katiba kwanza)
14.
C. SPIKA
Utaratibu wa sasa unafaa
D. MAWAZIRI
1. Waziri atakuwa na Elimu kuanzia walao shahada ya kwanza
2. Mawaziri hawata tokana na wabunge
3. Mawaziri hawata tokana na madiwani
4. Haitahusiwa mtu ambae ni Mbunge au Diwani kuteuliwa kuwa waziri.
Tanzania hufanya uchaguzi wa Wabunge na Madiwani kila baada ya miaka mitano. Kuna jumla ya majimbo 264 na jumla ya wabunge 393 (264+ 114+10+5)
Majimbo mengi ni makubwa kijiografia na mengine yana idadi kubwa sana ya watu. Kwa namna moja au nyingine, kipindi cha kampeni huisha bila baadhi ya wananchi kupata nafasi ya kumsikiliza mgombea.
Wakati mwingine mgombea huweza kuchaguliwa pasipo wananchi wake kumfahamu vizuri na hatimae hupelekea kupata wabunge wasio na tija.
Nashauri namna ya kuwachagua wabunge ibadilike na kuwa kama nilivyoeleza hapo juu.
i. Hii itachangia wananchi wachague mgombea wanae mfahamu vizuri na kuona anafaa kwakuwa zoezi litahusisha eneo dogo na idadi ndogo ya watu (KATA)
ii. Ni rahisi kurudia uchaguzi mdogo wakati wa kifo
iii. Ni rahisi kupima utendaji wa kiongozi kwakuwa na eneo dogo la uwajibikaji
iv. Kuwa na idadi ndogo ya wabunge kulingana na halmashauri zilizopo
v. Gharama ya kuendesha bunge itapungua kwa kiasi, na pengine itawezekana kuboresha malipo ya madiwani
vi. Gharama za uchaguzi na kampeni zitapungua. Mwananchi asie tajiri/na kipato kikubwa na mwenye karma au nia ya kuongoza ataweza kumudu kugombea na kufanya kampeni ndani ya kata hata ikimbidi kutembea kwa miguu au nyumba kwa nyumba😂
vii. Uwezekano wa kupata viongozi bora ni mkubwa sana
Hayo ni maoni yangu, kila mmoja anaweza kuwa na mtazamo wake. Pamoja na mambo mengine ambayo yapo katika Katiba, au wadau wengine watashauri lakini ningetamani kuona siku moja nchi yangu ikiwa katika muelekeo huu au unakaribiana na huu.
NAWASILISHA.
Nakaribisha kukosolewa, maoni, mapendekezo na mitazamo mingine pia. Asante.
why70278@gmail.com
Mbezi-Ubungo, Dar es salaam kwasasa (20240707)