50 Greatest Tanzanians (minus politicians)

Mwandishi wa Riwaya A.E.Musiba vitabu vyake Njama, Hujuma, Kufa na kupona, Kikosi cha kisasi nimesahau kimoja.
 
Chief Mkwawa. Alipigana vita na wajerumani kwa silaha asilia na aliwauwa wanajeshi wajerumani waliokuwa na silaha bora. Alikimaliza kikosi chote cha wajerumani. Walimshinda waliporudi mara ya pili na alijiua mwenyewe. hawakumpata.

Muadhama Kardinari Lugambwa. Cardinari wa kwanza Muafrika.

Julius Mwasanyage. Mwafrika wa kwanza kupata degree ya uchumi.
Padre Alanus OSB. Alihamasisha wananchi kujenga barabara km 28 kwa kutumia majembe, sululu na moto kwa kupasulia mawe. 70,s
Asante mkuu,ila naomba reference ya mwaka na Chuo alichopatia hii Degree ya Uchumi ndugu hapo kwenye red,ili nijiridhishe kuhusu hilo.
 
Jerry Murro (Mwanahabari shupavu aliye thubutu kuumbua live askari wala rushwa na kufuatilia matukio ya serikali inavyo nyanyasa wananchi wake)
Saed Kubenea (Mwanahabari za uchunguzi anaye thubutu kuandika bila woga kile anacho kiamini hata kama kitamuudhi Vasco da Gamba)
 
Maxence Melo and co, for starting this great blog ambayo inatambulika na kuogopwa pia na serikali iliyojo madakani.

JF imekuea kisima cha habari na chachu ya mabadiliko katika nchi nzima. I'm almost sure waanzilishi na wamiliki wa JF wanapata vitisho na technical subbotage za hapa na pale for standing up for what they believed in, big up!

hii sio blog. Ni forum
 
FMES member JF wengi tulijiunga kwa sababu yake...na nondozz zake

Ayasifiae Maharage basi huyo hajala Njegere...

Hivi umewahi kusoma posti za huyu nguli anaeitwa Barantanda?
Haswa akiwa anashusha mambo ya kale?

Unaweza kububujikwa na machozi.
 
Kusherekea 50 years naomba mtuletee list ya 50 greatest Tanzanians (tukimtoa Nyerere na wanasiasa ambao tushawajadili sana)

Itakuwa si vibaya mkatuletea na sababu why these unsung heroes are great

Si lazma mje na list ya majina 50 lakini muhimu ni kutuambia kwa nini hawa watu japo hawaenziwi na watawala wetu lakini muhimu kuwajaua na michango yao kwenye historia ya Tanzania.


Personally nitaanza na Mashado Plantan ambaye nilikuwa simjui mpaka member mmoja humu alipoingia na jina lake na nikatafuta wasifu wake. Mashado was the original INVISIBLE wa enzi zake kwani alikuwa ni Mwafrika Mtanzania wa kwanza kuanzisha Gazeti lake lilikuwa linaitwa ZUHURA in the 1950's !


Muhimu wawe wanatoka from all walks of life kasoro wanasiasa.

we might learn a thing or two

Jamani mbona hawa tumewatupa tumelaaniwa

1. Mkwawa
2. Munyigumba
3 Mirambo (Napoleon of Africa) etc etc
 
  • Shaaban Robert (Marehemu sasa)- Sina haja ya kumsemea sana.


  • Thabiti Nassoro Lipangile (Marehemu sasa) - Huyu alikuwa mtanzania wa kwanza kuhimiza utumiaji wa teknolojia ya mianzi miti, akapewa heshima ya pekee kabisa wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere. Jaribu kufikiria hadi mwanzoni mwaka 2000 baadhi ya makalavati yalitengenezwa kwa kutumia treated timber hasa kwa barabara ziendazo vijijini. Teknolojia hiyo hakuendelezwa na zaidi imepigwa zengwe na "sisi hawahawa na imekufa kifo cha kawaida.
  • Niko Zengekara (Marehemu sasa) - Mwibaji wa kibao kiitwacho Solemba kilichopigwa na JUWATA Jazz Band, alikuwa ni mlemavu wa macho(Kipofu). Hata hivyo alikuwa mahiri sana awapo stejini
  • Mzee Mwanakijiji - It goes without saying.
  • Sembuli, Zamoyoni Mogella...Ntarudi, tena ngoja nilale niote ndoto flaniflan hivi.

Nico Zengekara alikua mahiri sana,Solemba ikigongwa mpaka kesho kutwa bado inavuta..ila Nico alikua ni Mtanzania au Mkenya?sina uhakika sana,japo alikua anafanya mambo juwata jazz!vipi kuhusu Mbaraka Mwinshehe?
 
John Okello mwanamapinduzi aliyeleta uhuru wa zanzibar kisha akafukuzwa kama kibaka na mwl nyerere akishirikiana na karume. Kardinali rev.Rugambwa,padre wa kwanza kuwa askofu mzawa Tanzania pia kuwa kardinali wa kwanza mwafrika na kuwa candidate wakwanza afrika kukaribia kupata kuwa papa wa kwanza kutoka afrika.
 
Said Kubenea(jamaa kawa chachu ya kufichua uovu wa serikali kwa miaka hii ya karibuni)
Bendera(kocha wa timu ya taifa iliyoshiriki mara ya kwanza na mwisho kombe la Afrika)
 
Shaban Robert&Amir Sudi(kwa kukuza kiswahili kutokana na mashairi/tenzi zao na vitabu vyao mf.Kusadikika)
 
Salum Abdallah - Mwana muziki
Shaban Robert - literature
Mathias Mnyampala - Literature
Siti binti Saad - mwanamuziki wa awali mwanamke
 
1. Brigedia bayeke aliyekwenda kuwashikisha adabu washenzi waliokuwa wanabaka dada zetu mikoa ya magharibi. Kuna watu wana madaraka ya juu na vyeo vya juu hawajali, tena wanashiriki kufanya kama yale aliyopingana nayo bayeke.
2. Jenerali ulimwengu, aliyekwenda kwenye mission ya hatari msumbiji akiwa kijana mdogo, kutokana na moyo wa uazalendo kwa nchi yake, na moyo wa kupigania uhuru wa mwafrika...malipo yake aliambiwa kuwa si mtanzania
3. Issa shivji
4. Kuna dada mmoja mwanasayansi amepata tuzo pale muhimbili hivi karibuni

Inasadikika BAYEKE alikuwa anatumia uchawi wa Kifipa kule
 
1. Sunday Manara
2. Kitwana Manara
3. Kasim Manara
4. Greyson Sembuli
5. KIBADENI alikuwa na picha yake kwenye vibiriti enzi hizo
6. Jela Mtagwa-Picha yake iliwekwa kwenye stempu, mara ya mwisho nilisikia mgonjwa, sijui kwa sasa.
7. Juma Kilaza
8. Salum Abdala
9. Marijani Rajabu
 
  • shaaban robert (marehemu sasa)- sina haja ya kumsemea sana.


  • thabiti nassoro lipangile (marehemu sasa) - huyu alikuwa mtanzania wa kwanza kuhimiza utumiaji wa teknolojia ya mianzi miti, akapewa heshima ya pekee kabisa wakati wa uongozi wa mwalimu nyerere. Jaribu kufikiria hadi mwanzoni mwaka 2000 baadhi ya makalavati yalitengenezwa kwa kutumia treated timber hasa kwa barabara ziendazo vijijini. Teknolojia hiyo hakuendelezwa na zaidi imepigwa zengwe na "sisi hawahawa na imekufa kifo cha kawaida.
  • niko zengekara (marehemu sasa) - mwibaji wa kibao kiitwacho solemba kilichopigwa na juwata jazz band, alikuwa ni mlemavu wa macho(kipofu). Hata hivyo alikuwa mahiri sana awapo stejini
  • mzee mwanakijiji - it goes without saying.
  • sembuli, zamoyoni mogella...ntarudi, tena ngoja nilale niote ndoto flaniflan hivi.

hayo mabomba ya mianzi ya lipangile, bora yaliwekewa zengwe, yalikuwa yanadumu mwaka mmoja tu yanaoza kama hakuna flow ya maji nalo pia lilikuwa tatizo, kuvujisha maji pindi yakianza kupita.
 
Hayati Morris Nyunyusa, si mchezo yule mzee hakuna kama yeye hadi tarehe 9 tutakasherehekea miaka hiyo 50 kwa kupiga ngoma kama yupo na ajitokeze
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom