Song: Wazo La Leo
Artist: Stamina Feat Fid Q
Studio: Bongo Records
Producer: P funk Majani
Song Writters: Stamina (verses) & Fid Q
(chorus)
Intro...
U know what majani??nice to meet you
homie
Its moro town baby,,,shorobwenzi
Verse 1. (Stamina)
Elimika nyangema, maisha
hayaendeshwi na nguo
Pesa ni vazi la mgema, haliwezi kuwa
na mpasuo
Vaa uaminifu,tupa boksi la kondomu
Hip hop haijengwi na
bifu,underground usijaze fomu
Maisha ni kujipanga, mganga usigawe
irizi
Viongozi msizuie ganja, huku
mnachukua ushuru wa rizz
Ridhiki ina kamba, ivute ili ikupe noti
Mkulima rudi shamba,dec mbegu siku
hizi hazioti
Maisha njia panda,mtembezi chagua
pa kwenda
Uchumi vazi la bwanga,ukishuka uvishe
suspenda
Shiba kwa nia,ukiwa mlafi wa malengo
Usikufuru we shukuru ukifaulu kila
tendo
Punguza pupa,mpendaji uingie ndoani
Mapenzi yamevaa bukta,uswazi mapaja
hadharani
Usilale kijinga,kwenye kitanda cha
ushamba
Unaweza kuwa shabiki wa samba,na
ukaishi mwembe yanga
Chorus. (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona,baada ya kula
kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya
ngono
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu
ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi
wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha
angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa
vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo
vyako-{hilo ndo wazo}
Verse 2. (Stamina)
Underground panga tenzi,ustar hauji
kwa promo
Hakuna tajiri wa mapenzi,kapuku
punguza ngono
Bora uitwe mfalme jua,kwenye utawala
wa kishamba
Mapenzi yakikusumbua,tafuta daktari
wa kitanga
Vazi unaloishi,mwenyezi yeye ndio
disegner
Shetani akikushawishi, mvute kwake
kama dayna
Dunia duara,jitahidi uizunguke
Mla bata starehe hasara,,wekeza hadhi
isishuke
Huna undugu na bakhersa,niaje aje
unakula unga
Mateja wanahitaji sensa,taifa la kesho
linavunda
Dogo jifunze,heshima sio upaparazi
Mwambie na dada ajitunze,mlango
wake asiuache wazi
Kama unajijua ni mchoyo,basi usingoje
kupewa
Tafuta pesa kwa moyo,sio kwa ushindi
wa ngekewa
Sharo mpe salamu,the great braza
kanumba
Mwambie bongo sio tamu,na lulu
bado wamemfunga
Chorus(fid q)
Hiki kijiko unachokiona,baada ya kula
kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya
ngono
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu
ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi
wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha
angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa
vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo
vyako-{hilo ndo wazo}
Verse 3. (Stamina)
Utamu wa ndafu ya harusi,sio wa ndoa
we kilaza
Mbuzi atabaki mbuzi,hata mle hadi
mkasaza
Nchi tayari imekonda,mwananchi
tafuta ulaji
Life ngumu hadi omba omba,kidonda
anafanya mtaji
ukipata mazuri,jipange kuikwepa
hasara
kijana vazi la msuli,haliwezi kukuvisha
busara
ukiishi kwa hisia,kila stone litakubanza
cha msingi ni kuweka nia,ujivue kuwa
mtanza
kata ya kijiji,haibebi maji ya maendeleo
katibu tunza mkwiji,msuli ukishuka
kimeo
uchumi umeshika tama,kwenye shavu
la mlanguzi
raia usilaumu chama,shiriki kwenye
uchaguzi
unaweza ukavaa kinga,ila ukafa kwa
uaminifu
mzinzi usigawe ujinga,sambaza
ujumbe wasifu
hakuna snitch kama pesa,ukiwa nae
fanya vya maana
akiondoka atakutesa,utamsaka usiku
na mchana
Chorus. (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona,baada ya kula
kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya
ngono
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu
ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi
wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha
angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa
vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo
vyako-{hilo ndo wazo}