Heshima Mbele.
Happy New Year Kwenu Nyote.
Nasema Wenye vichwa vyepesi wataichukulia nyimbo kiuwepesi, watajadili Beat, Rhyme na Length. Watajadili wasifu binafsi wa alieimba (Roma), wataingiza Siasa pia.
Tutasahau lengo haswa la Msanii, mistari iliopo kwa hii nyimbo ndio lengo na ni msaada sana kwetu.
Naomba kuzungumzia mistari michache tu mingine mtaijadili binafsi.
1. "Tenda wanapeana kindugu, mwanangu kua uyaone"
Wengi wetu sisi ni watu wazima, tumeshakuwa lakini bado baadhi yetu hatujayaona. Hatujayaona labda kwa kuwa tumelelewa kitajiri sana na kwa connections au labda tumelelewa kimaskini sana na kiuoga hatuthubutu kuhoji. Hatujui thamani ya maisha yetu endapo Gold na Tanzanite zisingetoka kinyemela. Au Wanyama wetu wangeuzwa kihalali, Kodi zingelipwa on time na kwa halali etc. Kama hatujui haya wala hatujui tofauti ya Mtanzania na Msomali kirasilimali.
2. "Tazama Gongolamboto mtoto kamzaa mtoto na atalelewa na nani baba ake mmefunga keko"
Katika hali ya kawaida huwa serikali inakimbilia kumfunga mwanaume kama amejamiana na under age, ni kosa kweli na alistahili adhabu. Lakini je mmeshawahi jiuliza, yule mtoto atalelewa na nani?? Atamfahamu Baba? Je Baba akiwa Hai mpaka siku ya kutoka atakuaje?? Ataendeshaje maisha yake binafsi na ya mtoto au family?? Si ni majukumu million lazima a-opt shortcut (mbaya zaidi ya kuzaa na underage).
Kwanini tusingejiuliza na role ya mtoto wa kike hapo??
Kwanini tusingedisegn more fruitful penalty?? Community service inayozalisha both ways, kwa mtuhumiwa na serikali.
Kwanini elimu isitolewe (ya kweli sio hii wanayohubiri) kwa vijana wajue nini madhara ya kuzaa utotoni.. Msiseme haiwezekani angalieni mataifa mengine.
Hizi ni Punch mbili tu ziko miiingi zenye ujumbe mkubwa zaidi kila angle.
Hip Hop ni tamaduni, usiangalie flow kwenye hili angalia ujumbe na wakati tuliomo.
Asante Roma, 2030 ni Bonge la Nyimbo. Tunashukuru kukubali iweke Hulkshare.
Udini Wa Ma-Presenter, Sisi Wapagani Unatuumiza.