2030: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki

2030: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki

Song: Wazo La Leo
Artist: Stamina Feat Fid Q
Studio: Bongo Records
Producer: P funk Majani
Song Writters: Stamina (verses) & Fid Q (chorus)

Intro...
U know what majani??nice to meet you homie
Its moro town baby,,,shorobwenzi
Verse 1. (Stamina)
Elimika nyangema, maisha hayaendeshwi na nguo
Pesa ni vazi la mgema, haliwezi kuwa na mpasuo
Vaa uaminifu,tupa boksi la kondomu
Hip hop haijengwi na bifu,underground usijaze fomu
Maisha ni kujipanga, mganga usigawe irizi
Viongozi msizuie ganja, huku mnachukua ushuru wa rizz
Ridhiki ina kamba, ivute ili ikupe noti
Mkulima rudi shamba,dec mbegu siku hizi hazioti
Maisha njia panda,mtembezi chagua pa kwenda
Uchumi vazi la bwanga,ukishuka uvishe suspenda
Shiba kwa nia,ukiwa mlafi wa malengo
Usikufuru we shukuru ukifaulu kila tendo
Punguza pupa,mpendaji uingie ndoani
Mapenzi yamevaa bukta,uswazi mapaja hadharani
Usilale kijinga,kwenye kitanda cha ushamba
Unaweza kuwa shabiki wa samba,na ukaishi mwembe yanga

Chorus. (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona,baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}

Verse 2. (Stamina)
Underground panga tenzi,ustar hauji kwa promo
Hakuna tajiri wa mapenzi,kapuku punguza ngono
Bora uitwe mfalme jua,kwenye utawala wa kishamba
Mapenzi yakikusumbua,tafuta daktari wa kitanga
Vazi unaloishi,mwenyezi yeye ndio disegner
Shetani akikushawishi, mvute kwake kama dayna
Dunia duara,jitahidi uizunguke
Mla bata starehe hasara,,wekeza hadhi isishuke
Huna undugu na bakhersa,niaje aje unakula unga
Mateja wanahitaji sensa,taifa la kesho linavunda
Dogo jifunze,heshima sio upaparazi
Mwambie na dada ajitunze,mlango wake asiuache wazi
Kama unajijua ni mchoyo,basi usingoje kupewa
Tafuta pesa kwa moyo,sio kwa ushindi wa ngekewa
Sharo mpe salamu,the great braza kanumba
Mwambie bongo sio tamu,na lulu bado wamemfunga

Chorus(fid q)
Hiki kijiko unachokiona,baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}

Verse 3. (Stamina)
Utamu wa ndafu ya harusi,sio wa ndoa we kilaza
Mbuzi atabaki mbuzi,hata mle hadi mkasaza
Nchi tayari imekonda,mwananchi tafuta ulaji
Life ngumu hadi omba omba,kidonda anafanya mtaji
ukipata mazuri,jipange kuikwepa hasara
kijana vazi la msuli,haliwezi kukuvisha busara
ukiishi kwa hisia,kila stone litakubanza
cha msingi ni kuweka nia,ujivue kuwa mtanza
kata ya kijiji,haibebi maji ya maendeleo
katibu tunza mkwiji,msuli ukishuka kimeo
uchumi umeshika tama,kwenye shavu la mlanguzi
raia usilaumu chama,shiriki kwenye uchaguzi
unaweza ukavaa kinga,ila ukafa kwa uaminifu
mzinzi usigawe ujinga,sambaza ujumbe wasifu
hakuna snitch kama pesa,ukiwa nae fanya vya maana
akiondoka atakutesa,utamsaka usiku na mchana

Chorus. (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona,baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}

UNAWEZA UDOWNLOAD HAPA

Stamina yupo juu sana ana stock home ya mistari kama mji mkuu wa sweden.
 
Last edited by a moderator:
Wimbo una ujumbe mzito sana, tatizo siyo radio version, ni vigumu sana kwa baadhi ya radio kucheza wimbo wenye dakika 13...

Roma ni zaidi ya mwanamziki, ndani yake kuna uanaharakati!
 
Mkuu tunaposema kubadirika hatuna maana aimbe takeu au miziki ya akina bob jr, tunamaanisha kuwepo na tofauti kati ya track zake hata ukisikiliza ukiwa mbali ujue hii ni track flani na ile ni flani.
Nyimbo za roma zinafanana. kila mtu ana style yake ya kushusha mistari lakini haimaanishi track zake zitafanana.
Mfano ukisikiliza nyimbo za darasa usikate tamaa na nishike mkono japo flow ni ile ile lakini utazitofautisha tu.
Any way ni mtazamo tu the kid is still doing good
hebu tafta punch lyn za ukweri Tamadunimusic.com humu watu wanafanya real hip hop achaneni na roma hana jipya kikawaida watu wakikuzoea mwishowe wanakuchoka huwezi kuimba kitu kimoja miaka yote hebu angalia yaliowakuta hawa Bonta na kala jeremiah wameimba sana siasa lakn mwishowe kala akabadirika na kuachia ngoma yake Dear God ambayo amezungumzia vitu vingi sana kuhusu Tz na maisha ya raia kiukweri 2030 bado sana kwa dear god
 
wimbo ni mkali kinoma sioni sababu ya kuufungiwa kwani aliyoyasema humo ni kweli tupu
 
Mi naamini kama kweli tunasikiliza ujumbe katika Nyimbo basi.KWA TANZANIA SASA HAKUNA MSANII WA HIPHOP MWENYE MASHAIRI YANAYOIGUDA JAMII MOJA KWA MOJA KAMA ROMA.

''Wanasema Tuzo sikustahili kwani tuzo ina sarafu ya nani?? vya kaisari Mpeni kaisari''

Solo alisha sema hato shiriki hata apewe meli na shell.
 
wimbo ni mkali kinoma sioni sababu ya kuufungiwa kwani aliyoyasema humo ni kweli tupu

Wafungie tu kwani wangapi wenye Vingamuzi na redio sikuhizi? Digtal age hii ni mwendo wa simu na ringtone sasa watafungia simu za watu? Ngoja itoke watu wanyonye, tatizi na yeye kakomaa anauza mwenyewe hakuna kusambaza.
 
hahahah...inaonesha wewe ni mke mdogo wa roma mpagani sijui mkatoliki unajua wewe mwenyewe mkewe..maana ulivyoshupaza shingo kama unataka kufa jaman....kwani ndoa yako lini utakayovishwa pete na huyo mvuta bangi...au michango ya kitchen yako haijakamilika ndo maana umepanic...ni pm namba yako basi nikusaidie japo laki tatu tu
Hivi unajua bangi baadhi ya mikoa ni mboga kama mchicha tu..nimekwambia kama kuna watu haja wasema na wewe unataka awaseme, mpelekee hayo majina komba au Vicky Kamata akawachane mbona simple tu mkuu..kama anatumia bangi na anaendesha maisha yake haji kukuomba unga ina kuuma nini? na siyo lazima wewe umkubali lakini wengi wana mkubali mfano hapa Arusha ukipiga wimbo wake wa Mathematics watu ni mzuka mwanzo mwisho kwa huu mpya sipati picha...
 
hii dude balaa, nipo nilisikiliza "pacho ni mwamba na bado anakata viuno.........pesa ndio ilimaliza bifu kati ya ruge na sugu....sio kulichoma kanisa ni kuuza bible dubai....." aaaaah huyu jamaa
 
UKWELI UNAMCHOMA MWENYE KULENGWA, Hakuna anacho chochea ila ukweli ndiyo unawachoma walio wengi wenye kuogopa kusema ukweli kwa kisingizio cha kulinda amani. AMANI hailindwi kwa kusema uongo na kukumbatia maovu kwa kuficha ukweli
 
Normally Roma ndo falsafa yake na mtindo unaomtofautisha na wasanii wengine me nadhan wauache tu coz anachongea kipo sahih si cha kubuni
 
hahahah...inaonesha wewe ni mke mdogo wa roma mpagani sijui mkatoliki unajua wewe mwenyewe mkewe..maana ulivyoshupaza shingo kama unataka kufa jaman....kwani ndoa yako lini utakayovishwa pete na huyo mvuta bangi...au michango ya kitchen yako haijakamilika ndo maana umepanic...ni pm namba yako basi nikusaidie japo laki tatu tu

Post yako ni matokeo ya upungufu wa hoja kichwani,
 
Back
Top Bottom