2030: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki

Aliyeichoma masahafu pengine halijui kanisa so kuchoma makanisa ni ---- kuuza bible dubai
 
Ni ya kawaida sana nimeisikiliza mara nyingi, nadhan karopoka and is so direct sanaa haiko ivyo..hakuna jipya hapo.

hili ni bonge la ngoma, linaweza likawa tatizo kwako mana amewachana magamba.
 
Kasikilize Miss Tanzania na Homa ya dunia za Solo Thang ndo utaelewa mkuu sixgates alikuwa anamaanisha kitu gani.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Homa ya dunia!??? unafahamu alikokua ana copy hayo mashairi!?
 
Waliozoea nyimbo za wanaoimba "hakunaga,nataka kulewa,mpenzi jini,mawazo,follow me,nimpende nani, n.k" watauchukia wimbo huo kwani wao wanapenda nyimbo zinazohamasisha ngono tu. Kimsingi Roma amejitahidi kugusa yale yanayoisibu jamii moja kwa moja.Ni kweli wasanii wengine kama Solo Thang na wimbo 'miss Tanzania' ameonesha maudhui ila kwa mafumbo kiasi kwamba vichwa ngumu vinaweza kuambulia ujumbe kidogo sana.Maana ya sanaa ya Hip hop siyo tu kutengeneza maneno kiufundi ila kujua namna hadhira watakavyoupokea ujumbe na kuelewa...Kuna mstari anasema "RPC usitume polisi,ili kuwazima CHADEMA,itakulilia damu ya Mwangosi,Iringa semeni amina" Huu ni ujumbe ulionyooka bila kificho.Anaongezea..."uchafu wa Mrisho,usiwe usafi wa Benja..." Je,si kweli kwamba kuna madhaifu fulani ya Mrisho then,watu wanasema afadhali Benja aliendesha vizuri uchumi na mahusiano ya kidini,huyo Benja aliiba vingapi na kusainishwa mikataba inayoligharimu taifa hadi leo, mfano Kiwira coal mining,EPA na kashfa ya BOT?
 
Kasikilize Miss Tanzania na Homa ya dunia za Solo Thang ndo utaelewa mkuu sixgates alikuwa anamaanisha kitu gani.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

au akasikilize 'tunasonga' dogo&pina au 'mitaa ya kati' imam abbas au 'kesho yetu' one the incredible.
 
mbona mmeuweka humu huo wimbo waungwana, tabia c nzuri hii mwenyewe kakataa, au ndo tukuone we fundi sana? tunanyimana ugali hivi hivi
 
kuna line inasema "carolina kadisco chuo kikuu kwa sababu kamnyima penzi profesa, carolina atafanyaje wakati alikua anatumia fedha za kujikimu kutunza familia"
VERI VERI TRUE
 
Roma ajawai kutoa ngoma mpya,sijaona kipya kabisa hapo,ukisikiliza tangia anatoka hadi sasa anaimba kitu kilekile na flow ni ileile ya makelele..zaidi ni muendelezo wa kutumia majina ya watu maharufu kuyataja negatively ili apate atenshen...labda kipya ni kawachana waislam which is so bad.
Pole sana kwa mawazo yako ya kibaguzi!kwa taarifa yako ROMA ni Muislam na R.O.M.A ni kifupi cha jina lake na ndugu zake
 
Halafu jamani wasanii wetu wanaumia sana..tunaishia kuwasifia huku tunawaibia kazi zao kwa kudownload kwenye mitandao!!kwanini kama umeipenda usiinunue!!tuwapende na kuwatakia mafanikio wasanii wetu kwa kuwaunga mkono!!hii kuweka link ya free download na huku yeye mwenyewe alikataza inavunja sana moyo!!
 
Hata yale viongozi wetu wanayo ogopa kuyaongea kwakutimuliwa madarakani,ROMA yeye anayaongea bila kuogopa. Big up sana.
 
Sasa mnataka mafumbo au ujumbe? Mavumbo kwenye unyago na ktch part! Sio kwenye mambo ya msingi, mnataka watumie mafumbo ili wanchi wakawaida wasijui nini ama adress? Tena ningependa hataangetaja majina ya walio ficha pesa uswisi etc, Roma keep it up mchango wako unaonekana dogo!
 
Amejaribu hata kuwafananisha makongoro na ridhiwani baba miaka 25 ikulu na baba miaka 7 ikulu levo zimeachana mbaya

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Me huu wimbo nimeukubali 100% na roma ni jembe la hp hop ndan ya tz hakuna.hp hop sikuimba uongo kama siasa za ccm,na kila alicho imba ndio ukweli wenyewe.wewe riz1 atalingana na makongoro? Anakwambia trafiki hasira za nyumbani usilete barabarani,na kunawatu wamelisiti mwaka wa nne wanaitafuta c wakati mwalimu anaenda mjini na baiskeli kununua chaki,je hiyo c ataipata lini? Walimu waendelee kuuza visheti wanae wasife njaa.hiyo ndio hp hop hata usa 2pac na wenzie waliimba juu ya haki ya mtu mweus naleo obama ndani ya mjengo.hp hap na harakati za kweli nasio wabana pua we unacheza wakati max zinashushwa ili wanafunz wafaulu!! Unaimba mapenz unayajua? Eti michezo wakati yanga wamefukia fisi golin na simba wana bundi!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom