2026 FIFA World Cup - Special Thread

Kiukweli sikuona upendeleo game ya Morocco na France labda useme waliichezesha hivyo kujisafisha kupitia Marefa wa Argentina. Leo kwa jicho langu maamuzi yalikuwa sawa ila still bado hoja yako itasimama sababu waliochezesha leo wanayokea wapi.
 
Najua uko kwenye denial stage pale unapokuwa unapitia maumivu
Lakini bahati mbaya ni kwamba hakuna chochote unachoweza kubadili kwa hizo conspiracies zako.
Huwezi kubadili World Cup aliyobeba Argentina
Huwezi kubadili the fact yupo robo fainali
Huwezi badili record za Messi
Mi nilidhani kwa sababu we ni mshabiki wa Ronaldo ungekuwa unatetea record zake kutwa unapuyanga na story za kuokoteza kuhusu Messi na Argentina.
Umehamia kwa Mbappe na France ili tu upate faraja. Pole sana
 
Mkuu kuanzia sasa naanza kukuangalia kwa jicho la tofauti...uchambuzi wako umeleeweka mnoo
 
Lengo sio kubadili chochote.

Lengo ni kuita "koleo" pale napoona koleo na sio kuita koleo "kijiko" kikubwa.

Ni kama tukio la goli la mkono alilofunga Maradona mwaka 1986, tukio hili ambalo ni widely known ingekuwa ushahidi au ukweli kuhusu fraud nje na ndani ya kiwanja ukithibitika unaweza kubatilisha matokeo au ubingwa basi Argentina wasingetambuliwa kama mabingwa wa 1986.

Lakini records zinawatamhua kuwa walikuwa mabingwa, sio kwasababu ni goli halali (dunia yote inatambua hivyo)

Ila ni kwasababu tayari imekwisha tokea.

Swali ni je, mtu anayezungumzia utata wa hilo goli kutumika mkono anaweza badili chochote?

Jibu ni Hapana.

Je kwasababu hawezi badili chochote hapaswi kuzungumzia uovu huo?

Jibu ni hapana pia
 
Wabongo bwana!! Hicho ndicho mnachoweza
 
Kama ni hivyo elezea uovu wote usiwe selective
Unavyoiandama Argentina na Messi utafikiri ndio timu au mchezaji pekee duniani aliyewahi kufaidika na maamuzi yenye utata
Ronaldo na Ballon D'or ya 2013?..Ribbery analalamika mpaka leo
Malalamiko kuhusu Madrid au Man U kubebwa? husemi kisa ni timu zako
Halafu unadai eti Ronaldo kashinda kila kitu cleanly....kwamba mpira tumeanza kuangalia leo??...au wewe pekee ndo mtu anayefatilia mpira ???
 
Hata nikielezea uovu wote bado Messi anabaki kuwa on top na hili wewe unalijua.

Kilichofanyika jana kwenye mechi ya France na Morroco kufuatia swala la FIFA kuweka marefarii wote kutoka nchi ya Argentina.

Ndio kitu hicho hicho walichofanya FIFA 2013 kwenye Ballon dor ya Ronaldo.

Marefarii wa Argentina walitumika kama ufagio wa kuwasfisha FIFA na Argentina dhidi ya ulanguzi walioufanya kwenye mechi dhidi ya Egypt.

2013 Ronaldo aliwahi kutukanwa na raisi wa FIFA na kufanya Portugal na mashabiki wa Ronaldo wamchukie Raisi huyo.

Na mbaya zaidi alienda mbali kwa kusema Messi ndio bora zaidi kwani Ronaldo hana chochote zaidi ya usela wa kuweka mitindo ya nywele.

Hicho kitu kilimjengea uhasama mkubwa na ili kuua soo ndio akaja na hizo drama za kuongeza muda wa kupiga kura.

Hii automatically ilienda kumsafisha kwasababu automatically ilikuwa na tafsiri ya kwamba imewekwa hivyo ili kumpa advantage Ronaldo kwenye mechi yake dhidi ya Sweden.

Ndio maana hata hawa marefarii wa Argentina niliwaona ni muendelezo uleule wa kimkakati ambao FIFA wamefanya.

Kwenye malalamiko yangu yote kuhusu kubebwa na favor anazopewa Messi nimejikita zaidi kwenye hili kombe kuliko ishu zingine kama Ballon Dor.

Kwasababu hata wewe mwenyewe sidhani kama uko tayari nijadili Ballon Dor ya 2010, na sidhani kama utakuwa na utetezi wa aina yangu nilioutoa kuonesha FIFA walikuwa wana restore imani ya wadau wa soka kuonesha kwamba hawana upande katia ya Messi na Ronaldo.
 
Blatter aliongea ukweli mashabiki wa Christiano mkakasirika. Christiano kitu pekee anachomzidi Messi ni kutengeneza nywele kwa mitindo tofauti πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…